Ubatizo, Ushiriki Mtakatifu

Mwandishi: 
Jari Rankinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Mchungaji anamwaga maji juu ya kichwa cha mtoto na kumbatiza yeye katika jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Na kama hili halikufanyika kwa mtoto, linaweza kufanyika hata kwa mtu mzima, kwa nini?

Tunabatiza kwa sababu Yesu aliamuru tufanye hivyo. Alisema kupitia ubatizo mtu anakuja kuwa mwanafunzi wake na kupata kile alichonacho. Kupitia ubatizo tunakuwa watoto wa Mungu, na kama zawadi tunapata msamaha wa dhambi,na uzima wa milele. Biblia inasema tulivikwa ndani ya Kristo wakati wa ubatizo. Kimbilio letu ni ndani ya kile Yesu anafanya kwa ajili yetu.

Ni asili yetu kushangaa ni kwa jinsi gani maji yanaweza kufanya mambo makubwa kama haya. Mungu ameahidi kutenda wakati mtu anabatizwa. Ameahidi kumchukua mtu kama mtoto wake,kumsamehe na kumwokoa. Mungu amechagua njia hii kutufanya sisi wake kwa kile Yesu amefanya. Hakika kuna Hekima kubwa kwa kazi Mungu aliyofanya kwa njia ya Yesu Kristo.

"Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkawabatize kwa jina la Baba, na Mwana na Roho mtakatifu”.
(Mathayo 28:19-20, SUV)

Mwandishi: 
Jari Rankinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Nilibatizwa miaka mingi iliyopita. Hii ina maana gani sasa? Je ina maana yeyote? Kwa mimi ubatizo una maana kubwa wakati nikiwa mtoto nilibatizwa sikuwa na la kufanya sikujua, wala kufanikiwa au kubadilisha. Hata kama ni kitu kidogo. Kama nikiwa ndani ya kutokamilika, kutokujua au kuwa mzuri- nilikuwa wa kutosha kwa Mungu. Nilikuwa mwenye haki kwa sababu Yesu alikufa kwa ajili yangu na alizipatanisha dhambi zangu. Ilikuwa hivyo na iko hivyo sasa. Hivi ndiyo ubatizo unavyonikumbusha mimi.

Vipi kama kila asubuhi tungeweza kusema sisi wenyewe ubatizo una maana gani, kama nilivyo mimi ni mali ya Mungu na ninakwenda mbinguni kama nilivyo, ninawezakupata suluhisho kwa Yesu. Sasa hii inaleta furaha na heshima. Hili ni jambo ambalo linaleta nguvu na kuishi kama mkristo na kuishi kwa mapenzi ya Mungu hata kama kwa kiasi kidogo.

Biblia inafundisha kwamba tumeokolewa kwa neema. Kwa kuokolewa kwa neema ina maana kwamba tunaweza kuwa mali ya Mungu pasipo kuwa na kuchangia na kuipata mbingu kama jinsi tulivyo na yote hii ni kwa sababu ya kazi ya Yesu msalabani. Kila mtu aliyebatizwa na kuamini katika Yesu ataokolewa kwa neema.

“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu."
(Efeso 2:8 SAV)

Mwandishi: 
Jari Rankinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Biblia inasema hivi ili uokolewe unahitaji ubatizo la imani. Hatuwezi kudharau ni nini Mungu alisema kuhusu hilo. Vinginevyo tutakuwa katika hatari ya kuacha kazi yake ya ukombozi. Kwa hiyo lazima tuwabatize watoto wetu na kuchukua ubatzo sisi wenyewe kama bado hatujabatizwa.

Biblia inataja kwamba baadhi waliookolewa pasipo kubatizwa, katika siku ya ijumaa kuu, Yesu alisema kwa Yule mwaalifu aliyetiwa karibu yake kwamba atakuwa pamoja naye paradiso. Huyu jamaa labda alikuwa hajabatizwa. Mungu anaweza fanya kazi hata nje ya vyombo vya neema ambavyo Ametuambia kuvitumia anaweza kuokoa hata bila ubatizo. Lakini mtazamo huu wa kiuungu hauturuhusu sisi, kudharau ubatizo ambao ametuhamuru sisi tuupokee. Kama wakristo tumefungwa katika mafundisho ya Agano jipya.

Katika ubatizo tunakuwa wakristo na watoto wa Mungu. Wakati linapokuja suala la mtoto asiyebatizwa amekuja tunaweza kusema tu kwamba yeye yuko mikononi mwa Mungu wetu mwenye Rehema.

“Aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa.”
(Marko 16:16 SUV)

Mwandishi: 
Jari Rankinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Wewe unayependa mambo ya imani na hujabatizwa unaweza shangaa kama utatakiwa kubatizwa. Ndiyo ni lazima, kutana na mchungaji au mfanyakazi wa usharika wa kanisa la Kilutheri watakushauri kwenda katika shule ya maungamo. Kama wewe ni wa kati ya miaka kumi na tano (15) unaweza kuudhuria kambi ya maungano. Pamoja na mchungaji mnaweza kwenda moja kwa moja katika mafungu muhimu ya imani na baadaye unaweza kubatizwa,au ungelipenda kubatizwa lakini si rahisi labda uko chini ya umri au wazazi wako hawapendi wewe ubatizwe. Unaweza kuamini katika Yesu ijapokuwa hujabatizwa. Nenda katika ubatizo mara moja kama ulivyoamua.

Nini kama una mtoto mdogo ambaye hajabatizwa? Ni lazima huyu mtoto abatizwe- ndiyo fanya mawasiliano na mchungaji au mfanyakazi wa usharika na mmpange ubatizo.

“Petro akawaambia, tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpaate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapoke kipawa cha Roho mtakatifu kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu walio mbali na kwa wote watakaitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”
(Matendo ya mitume 2:38-39 SUV).

Mwandishi: 
Jari Rankinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Biblia inafundisha kwamba ubatizo hauwezi na hauitaji kurudiwa. Unatolewa mara moja na una thamani wakati wote. Hii haibadilishiki hata kama tunamkataa Mungu baada ya ubatizo wetu. Tunaweza wakati wote kumrudia Baba yetu anatusubiri sisi.

Na wakati tunamrudia hatuitaji ubatizo mpya. Hata kuna wale wanaotaka kubatizwa tena au wameshabatizwa tena. Na kuna wale wanaobatiza watu tena. Wengi wao wanaweza kufikiri kwamba kama mtu akibatizwa akiwa mtto si ubatizo halisi. Hii ni mapingano halisia na hii ina maana kwamba hujabatizwa na wewe si mkristo. Wengine wanasema kama mtu hawezi kuelewa mara moja maana ya kubatizwa, kwamba, kaka/dada alivyobatizwa, hivyo unaweza kuwa si ubatizo halisi. Lakini ubatizo ni tendo la Mungu ambalo halitengemei ni kiasi gani mtu anaelewa. Hatuwezi kuelewa nini kilitokea wakati Yesu alikufa juu ya msalaba kwa ajili yetu na hatuwezi kuishi wakati ulitokea lakini imebakia ni tendo la Mungu na wokovu wetu. Hivyo basi ubatizo hautakiwi kurudiwa, mtu anayepokea ubatizo mara ya pili anafanya makosa, makosa ambayo kweli yanatakiwa kutubiwa kwa Mungu na kuomba msamaha. Na Mungu anasamehe wote wanaotubu kwa sababu Yesu alizipatanisha dhambi za watu wote.

“Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.“
(Efeso 4:5 SUV)

Mwandishi: 
Jari Rankinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Wakristo wanashiriki meza ya Bwana kama Yesu alivyoamuru. Wakati wote wanaposhiriki, maneno ya Yesu yanayofanya Ushirika mtakatifu yanasomwa. Yamechukuliwa kutoka katika maandiko matakatifu ya Biblia ambayo yanawaambia nini kilitokea Yerusalemu wakati wa usiku kabla ya kifo cha Bwana Yesu. Yesu na wanafunzi wake walisherehekea sakramenti, na Yesu aliwaambia kuendelea kufanya hivyo baadaye.

Katika maneno ya ushirika mtakatifu yanasema kwamba mkate ambao tunaumega ni mwili wa Bwana Yesu na Mvinyo ni agano jipya katika damu yake. Katika injili kutokana na Mathayo, Yesu alisema pia hii ni Damu yangu kwa hiyo mwili na Damu vipo pale katika ushirika mtakatifu.Ina maana kwamba Yesu yupo ndani ya mkate na katika mvinyo kwa njia maalum. Tunakutana naye na y eye anakutana na sisi. Wakati unafikiri wapi ningetakiwa kwenda kupata ukaribu na Yesu, nenda kwenye ushirika mtakatifu. Huu ni muujiza mkubwa wa ushirika mtakatifu. Yesu yuko pale na anafanya kazi nasi.

Katika ushirika mtakatifu mara nyingi unaweza kufikiri au kuhisi kwa uhakikakama kweli nitakutana na Yesu. Lakini mawazo yetu hayawezi kumzuia Yesu kuja karibu yetu. Yeye yupo palepale alipoahidi kuwa haijalishi ni kwa jinsi gani tunafikiri. Aliahidi kuwa kwenye ushirika mtakatifu-Mkate ni mwili wake, ana mvinyo ni damu yake.

"Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa Mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni mle; huu ndio mwili wangu. Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki, kwa maana hii ndio damu yangu ya agano, imwagikayokwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi."
(Mathayo 26:26-28, SUV)

Mwandishi: 
Jari Rankinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Katika ushirika mtakatifu tunakutana na Yesu, na hii ni nzuri kwetu kwa njia nyingi. Mkombozi wetu ana utume: mmoja tu anasamehe, hivi ndivyo Yesu anafanya katika ushirika mtakatifu. Anashirikisha kile alichopata katka mauti yake. Kifo chake kilipatanisha dhambi zote za watu na kuleta msamaha kwa wingi kama watu watakavyohitaji.

Dr. Martin Luther aliijua Biblia kwa uzuri. Kwa swali la nini kizuri katika Ushirika Mtakatifu alijibu “katika ushirika mtakatifu dhambi zangu zote zinasamehewa” tunapata uzima na Baraka, kwa maana penye msamaha wa dhambi kuna pia uzima na Baraka.
 Kila anayeamini nini Biblia imeahidi anakuja katika ushirika mtakatifu na kupokea mwili na Damu ya Yesu kwa ondoleo la dhambi zake. Biblia imeahidi kwamba kwenye ushirika matakatifu Yesu ametoa msamaha wa dhambi. Hii inawezekana kuonekana tu njia nyepesi na rahisi. Lakini rehema za Mungu ni rahisi. ila Mara nyingi tunazifanya tu kwa ngumu.

“Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele na nitamfufua siku aya mwisho.”
(Yohana 6:54 SUV)

Mwandishi: 
Jari Rankinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Ushirika mtakatifu ni kwa wakristo wote waliokwisha kubatizwa. Katika Kanisa la Kilutheri wale wote waliokwisha kwenda katika shule ya maungamo na wameshabarikiwa wanaweza kupokea ushirika mtakatifu. Hii ni kuonyesha ni vipi washirika wanahakika na kuelewa maana ya ushirika mtakatifu na kujua tofauti ya ushirika mtakatifu na chakula cha kawaida na kinywaji pia. Watoto waliofundishwa wanaweza kupokea ushirika mtakatifu pamoja na wazazi wao au wazee wao. Na kila mmoja anaweza kuja madhabahuni kupokea Baraka.

Wakati mwingine unaweza kujihisi vigumu kwenda kwa ushirika mtakatifu, mmoja ajiskia kama hastahili vya kutosha kupekea sakramenti, kwamba lazima awe mzuri na mwenye imani imara. Hivyo sivyo inavyotakiwa iwe, ushirika mtakatifu si kwa ajili ya uzuri wetu tulionao au kwa wale waliofanikiwa kaika maisha. Zaidi ni kinyume , ushirika mtakatifu ni kwa wale wote wanohitaji msamaha wa dhambi. Katika ushirika mtakatifu rafiki na mkombozi ana rehema kwa wale wote walioshindwa. Ushirika mtakatifu ni kwa wale wote wanaohitaji msamaha wa dhambi. Si kwa wale wote wanofikirii hawamwitaji Yesu Kristo.

Biblia inatuonya sisi juu ya kwamba mtu anaweza kula na kunywa mwili na damu ya Yesu kwa hukumu yake mwenyewe. Baadhi ya watu ambao onyo hili wamepewa, kwa asili ni wale ambao wanatumia kupokea ushirika mtakatifu kwa njia ya kwamba hawajui kama ni ushirika mtakatifu. Wanakula na kunywa na wakati mwingine wanaweza kulewa. na mkate na mvinyo unaweza kuliwa na kunywewa bila utaratibu. Kwa upande mwingine Paulo aliandika kwamba ambaye anapokea ushirika mtakatifu na hajui ni mwili wa Kristo, atakuwa anakula na kunywa hukumu yake mwenyewe. Onyo hili mara nyingi limekuwa likieleweka hivyo, Na kukataa ushirika mtakatifu wale wote ambao si wema, na imani zao ni dhaifu. Lakini si sababu

“Maana kila mlapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.”
(1 Korintho 11:26 SUV)