Kama nimebatizwa ya pili?

Mwandishi: 
Jari Rankinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Biblia inafundisha kwamba ubatizo hauitaji kurudiwa. Unatolewa thamani hubaki hivyo daima. Hii haibadiliki hata kama tunamkataa Mungu baada ya ubatizo wetu. Tunaweza wakati wote kumrudia Baba yetu anatusubiri sisi.

Hata hivyo kuna wale wanaotaka kubatizwa tena au wameshabatizwa tena. Na kuna wale wanaobatiza watu tena. Wengi wao wanaweza kufikiri kwamba kama mtu akibatizwa akiwa mtoto si ubatizo halisi. Haya ni madai hatari. Hii inamaana kwamba hujabatizwa na wewe si Mkristo. Wengine wanasema kama mtu wakati wa ubatizo hakuelewa mara moja maana ya kubatizwa kwamba huo sio ubatiso halisi. Lakini ubatizo ni tendo la Mungu ambalo halitengemei ni kiasi gani mtu anaelewa. Hatukuelwa ni nini kilitokea wakati Yesu alikufa juu ya msalaba kwa ajili- hatukuepo wakati lilitokea lakini lilikuwa ni tendo la Mungu na wokovu wetu.

Hivyo basi ubatizo hautakiwi kurudiwa, mtu anayepokea ubatizo mara ya pili anafanya kosa. Yetote ambaye amekosa anatakiwa kutubu kwa Mungu na kuomba msamaha. Na Mungu anasamehe wote wanaotubu kwa sababu Yesu alizipatanisha dhambi za watu wote.

“Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.“
(Efeso 4:5 SUV)