Kuna nini kizuri katika meza ya Bwana?

Mwandishi: 
Jari Rankinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Katika ushirika mtakatifu tunakutana na Yesu, na hili ni nzuri kwetu kwa njia nyingi. Mkombozi wetu ana utume: Anasamehe. Hivi ndivyo Yesu anafanya katika ushirika mtakatifu. Anashirikisha kile alichopata katka mauti yake. Kifo chake kilipatanisha dhambi za watu wote na kuleta msamaha kwa wingi kama watu watakavyohitaji.

Dkt. Martin Luther aliijua Biblia kwa uzuri sana. Kwa swali ”Kuna nini kizuri katika Ushirika Mtakatifu” anajibu: “katika sakaramenti hii dhambi zetu zote zinasamehewa” tunapata uzima na baraka, kwa maana penye msamaha wa dhambi kuna pia uzima na baraka.”

Kila anayeamini yale Biblia imeahidi anakuja katika ushirika mtakatifu na kupokea mwili na damu ya Yesu kwa ondoleo la dhambi. Biblia imeahidi kwamba katika ushirika matakatifu Yesu anatoa msamaha wa dhambi. Hii inaweza kuonekana tu nyepeso na rahisi . Lakini huruma za Mungu ni rahisi. Ila Mara nyingi tunazifanya tu kwa ngumu.

“Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele na nitamfufua siku aya mwisho.”
(Yohana 6:54 SUV)