Biblia

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Biblia ni kitabu muhimu cha Ukristo. Kulingana na imani yetu, Mungu anatuzungmzia katika Biblia, anatwambia sisi ni nani, nafasi yetu ni ipi mbele za Mungu, nafasi yetu katika dunia ya Mungu na Mungu anatarajia nini kutoka kwetu.

Agano la kale na Agano Jipya, sehemu zote mbili zina uhusiano wa karibu, na zimetolewa kwetu na Mungu kupitia watu. Hutengeneza Biblia nzima: Inaanza na kuumbwa kwa binadamu, ikifuatwa na anguko lake na jinsi Mungu aliandaa njia ya kumrejesha kwa kumtoa mwanae kwetu. Biblia inaanza na uumbaji na umaliza nayo− Kutakuwa na hukumu ya mwisho, dunia tunamoishi sasa itapotea, Mungu ataumba dunia mpya mahali atapeleka wote wamwaminio Kristo.

Bibilia nzima imeandikwa na watu lakini wakati huohuo tunaamini Biblia nzima ni neon la Mungu. Mungu ametupa neno lake katika hali ambayo iko katika hali ya unyonge kwa njia nyingi- Angeandika ujumbe wake kwa moto au atume malaika wake walitangaze. Lakini ilikuwa katika unyonge pia wakati mtoto alipowekwa katika hori la ngombe katika Bethrehemu. Hii ndiyo inaonekana kuwa njia Mungu anayofanya kazi. Japo si njema kwa wenye hekima na matajiri, ni hazina ya wanyonge na masikini.

Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.
(Zaburi 119:105)

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Maneno ya ajabu ya kwanza ya Injili ya Yohana hutuambia maneno ya Biblia: Mungu aliuumba dunia kupitia Kristo. Yalitekwa na giza ambayo hakuna mwanadamu hata mmoja anayeweza kumtafuta Mungu kamwe kwa nguvu zake. Huwezi kukaribia, huwezi kusikia sauti yake, huwezi kumwomba ushauri wake. Hali hii ilibadilishwa Kristo alipozaliwa katika dunia hii: “Nuru imengaa gizani.”

Kulinga na imani ya Kanisa letu, Kristo ndiye nuru ya ulimwengu na njia pekee ya kwenda kwa Mungu. Mwanga huja kwetu katika Biblia, neno la Mungu. Mungu hazungumzi nasi moja kwa moja lakini Roho wake Mtakatifu huzungumza kwa neno lake ambalo ni hai na lenye nguvu.

Bado hatuwezi kumkaribia, hatuwezi kusikia sauti yake bado wala kuuliza ushauri wake. Lakini tunao nuru ya neno lake, na mwanga huu hutuongoza nyumbani kwa mwanga.

Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. (Yohana 1:14)

Ee Mungu, niangazie nuru yako na katika mapito yangu. Nizaidie nimfahamu mwanao Yesu.
Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Kuna vitabu vitakatifu kadhaa kuniani. Biblia ni mmoja wapo. Kwa nini ni Biblia na wala si vingine, kwa mfano mojawapo kitabu ambacho cha zamani kuliko Biblia?

Sasa, tunaelekea katika somo ambalo ninaponyoka fikra na mawazo ya binadamu. Wakristo hawawezi kutumia fikra za binadamu kuwahakikishia wale ambao wana mashaka kuwa Biblia tu ndio neno la Mungu na wala si kama vitabu vingine vinavyo dai kichwa hiki. Hatujalinganisha mkusanyiko wa vitabu vyote vya zamani na baada kufikiria, kuchagua mojawapo kama vile unaponunua simu mpya. Walimu wa zamani wa Kilutheri walisema katika maneno makali. Ni hali ya Biblia kuwa inamtibithishia musomaji kuwa kwa uhakiki ndiyo neno la Mungu. Kwa njia hii mamlaka ya neno la Mungu hayategemei na maamuzi yanayotolewa na Kanisa, kwa mazungumzo ya kueleweka au utafiki wa kisasa. Haitegemei chochote ila ukuu na nguvu za Mungu.

Hii ndio sababu msomaji wa Biblia anaweza kuhakikishiwa kwamba Mungu anamzungumzia.Msomaji mwingine anaweza asikubaliane na mawazo haya. Kulingana na imani yetu, hii inamaanisha kwamba nuru ya Mungu haifikii moyon wa kila mtu.

Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa.
(1 Wakorintho 1:20-21)

Mungu, umenipa fahamu zangu zote. Nizitumie vema kwa faida zangu na wengine.
Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Ndio. Ila ni kosa kubwa kupima hili kutumia vipimo vya wanadamu.

Kwa karne nyingi, Wakristo ambao walikosa kukubaliana mambo mengine angalau walikubaliana kuwa Biblia ni kweli na ni neno la Mungu. Hawakukubalina tu juu ya tafsiri ambazo zinatolewa kwake. Kama Karne moja na nusu iliyopita, uchunguzi wa historia na sayansi ulianza kuuliza juu ya ukweli wa Biblia na Wakristo walijibu kwa njia tofauti. Wengine walianza kutibithisha kuwa Biblia ni neno la Mungu kwa kukataa habari mpya kinyume na Biblia. Wakristo wengi bado hufanya hivi.

Walipokea tu, mawazo ya namna hii hutuongoza katika kufikiria katika njia ifwatayo: Ili iwe neno la Mungu Biblia inahitaji kuendana na akili na sayansi ya elimu. Kujaribu kuchukua msimamo huu huchukua nguvu zetu zote, na tuna uzoefu mkubwa juu ya jambo hili.

Uweli wa neno la Mungu hautegemei mawazo ya kibinadamu wala elimu. Uweli wa Biblia umejengwa juu ya ukweli kwamba Mungu anajitambulisha na mapenzi yake kwetu katika mfumo wa maandishi. Ni jambo la imani, ambalo ni zawadi kutoka kwa Mungu. Kwa sababu fulani wapitaji katikati ya soko la Thessalonika walitambua wito wa Mungu katika mazungumzo ya watu . Paulo anaelewa kuwa hii ni kazi ya Mungu.

Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.
(1 Wathesalonike 2:13)

Mungu wewe si kisiwi na neno lako si bure. Usinyamaze kwangu pia lakini naomba nisikie sauti yako.
Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Njia nzuri ya kusoma Biblia ni kuanza kusoma mojawapo ya vitabu vya injili kutoka mwanzo hadi miwsho. Changuo linaweza kuwa ngumu kwa sababu injili zote zina tabia zao mbali mbali. Ukichagua uzuri wa Marko usiorembeka− mistari yake mikafu huifanya ifutie. Au ukichagua injili ya Yohana na kuingia katika urembo wenye joto ambao inaoaka rangi? Chaguo lolote ambalo utaamua, anzia injili, some zote na halafu halafu endelea na Agano jipya kwa mpangilio. Kitabu kimoja kwa wakati moja tangu mwanzo hadi miwsho, kila siku kulingana na uwezo wako.

Kwa mfano ukisoma Agano jipya mara mbili unaweza kuendelea na Agano la Kale. Vitabu wa kwanza vya Musa vinaweza kupatikana kwa uraisi lakini baada ya hivyo unaweza kushangaa juu ya amri ambazo zilipewa kwa watu ambao si Wayahudi. Ikifika upande wa manabii, jambo la maana ni kujifunza lini na katika mazingira gani kitabu kiliandikwa. Kwa hili utahitaji msaada zaidi. Ila si usumbufu wa bure- Agano la kale nimejaa hazina ambazo zinafaa kupatikana!

Kila neno la Mungu limehakikishwa;Yeye ni ngao yao wamwaminio. (Mithali 30:5)

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Biblia hutafsiriwa katika njia mbalimbali, lakini si tafsri zote huleta sifa kwa wandishi. Ni rahisi kupata matokeo sahihi ukitilia maanani sheria za msingi.

Biblia yetu ilizaliwa katika kipindi cha miaka mia kadhaa. Katika kuitafsiri, ni vema kuuliza jinsi wasikilizaji wanaelewaje kitabu hiki. Na mwasikilizaji walikuwa na magwazo gani juu ya maneno ya Yeremia, wakati moja wapo wa manabii waliona huaribisfu wa Yerusalemu ilipoacha mapenzi ya Mungu? Baada ya huaribifu huu, watu walifikiri nini waliposikia maneno ya Isaya, ahadi ya ajabu katika sura ya 40? Je wasikilizaji wa kwanza wa ufunuo walitafsirije unabii wa lazima? Kuuliza maswali ya namna hii huleta utayari wa kujifunza, kusoma sehemu kubwa ba kuuliza ushauri. Lakini je unafaa.

Kuelewa historia hujenga daraja nyingi katika maisha yetu ya siku kwa siku. Mkristo husoma Biblia nzima, akiweka Kristo kama kiini na kidogo kidogo uelewa unapanuka. Ni kwa hatua hii mkusanyo wa vitabu ulizaliwa katika kipindi cha karne nyingi imekuwa jinsi kilivyo-Mungu ametuma barua ya mepenzi kwako.

Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
(2 Wakorintho 5:18-21)

Mungu, ahsante kwa walimu wanaofundisha mapenzi yako. Naomba niwapata pia.