Jinsi ya kutafsiri Biblia?

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Biblia hutafsiriwa katika njia mbalimbali, lakini si tafsri zote huleta sifa kwa wandishi. Ni rahisi kupata matokeo sahihi ukitilia maanani sheria za msingi.

Biblia yetu ilizaliwa katika kipindi cha miaka mia kadhaa. Katika kuitafsiri, ni vema kuuliza jinsi wasikilizaji wanaelewaje kitabu hiki. Na mwasikilizaji walikuwa na magwazo gani juu ya maneno ya Yeremia, wakati moja wapo wa manabii waliona huaribisfu wa Yerusalemu ilipoacha mapenzi ya Mungu? Baada ya huaribifu huu, watu walifikiri nini waliposikia maneno ya Isaya, ahadi ya ajabu katika sura ya 40? Je wasikilizaji wa kwanza wa ufunuo walitafsirije unabii wa lazima? Kuuliza maswali ya namna hii huleta utayari wa kujifunza, kusoma sehemu kubwa ba kuuliza ushauri. Lakini je unafaa.

Kuelewa historia hujenga daraja nyingi katika maisha yetu ya siku kwa siku. Mkristo husoma Biblia nzima, akiweka Kristo kama kiini na kidogo kidogo uelewa unapanuka. Ni kwa hatua hii mkusanyo wa vitabu ulizaliwa katika kipindi cha karne nyingi imekuwa jinsi kilivyo-Mungu ametuma barua ya mepenzi kwako.

Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
(2 Wakorintho 5:18-21)

Mungu, ahsante kwa walimu wanaofundisha mapenzi yako. Naomba niwapata pia.