Mateso na uovu

Mwandishi: 
Manu Ryösö
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Hili ni swali ambalo mwadamu amefikiriwa sana tangu zamani. Kama Mungu mwenye enzi na Mungu mwema yupo kwa nini anarushusu vita, njaa, mauaji na mambo mengine ambayo yanaharibu maisha? Si angekuwa na uwezo wa kuzia haya yote?

Biblia imeliacha swali hili wazi. Mambo mengine yamejibiwa ila maswali mengine mengi yako hewani tu. Mojawapo ya mitazamo ni kwamba duniani kuna shida ambazo zimesababishwa na mwanadamu mwenyewe. Vita, mateso, uasherati na hali zingine nyingi za kuumiza zimezababishwa na mwadamu. Mwadamu hawezi kumlaumu Mungu kwa haya yote ila lazima atajizame katika kioo.

Katika dunia hii, kuna mateso ya aina nyingi ambayo yamesababishwa na mwanadamu mwenyewe. Haya yote ni pamoja kwa mfano magonjwa na shida za hali ya hewa. Kwa nini Mungu asizuie haya yote yasitendeke? Haya yamebaki siri kwetu. Inaonekana hata hivyo kuwa mambo mengine ni hali ambayo Mungu anayatumia kuwaleta watu kwake. Pengine sababu moja wapo ya mateso hapa duniani ni ili mwadamu ajue jinsi alivyo mdogo ili aweze kumgeukia Mungu. Kwa upande mwingine shida huwaleta watu kukaribia mapenzi ya Mungu kwamba tuweze kuzaidia wale ambao wana mahitaji. Faraja yetu na tumaini ni neno la Kristo aliye fufuka- mshindaji wa mauvu na mateso.

Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini BWANA humponya nayo yote.
(Zaburi 34:19)

Mungu, uovu na mateso yanasumbua moyo wangu. Utuokoe na huovu!
Mwandishi: 
Manu Ryösö
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Biblia haitwambii kila kitu. Inatutangazia yale ambayo ni muhimu kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, Mwanzo wa maovu ni miongoni mwa yale mambo ambayo inazungumzia kidogo sana juu yake.

Mwanzo wa Biblia inatibithisha kimsingi kuwa mwanadamu ana uhuru wa kuchagua mema na mabaya. Dunia na mwadamu viliumbwa ili viwe vyema, lakini mwanadamu alichagua uovu alipodanganywa na shetani. Ibilisi ni kiumbe cha Mungu pia. Imesemekan kwamba kwanza ni mwanadamu ambaye alimpinga Mungu. Shetani alimvuta mwanadamu kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu na hivyo ndivyo maovu yalienea duniani.

Kwetu sisi imebaki muujiza kwa nini Mungu mwema aliruhusu maovu kuingia duniani. Hata hivyo, ni wazi kwamba Mungu mwenyewe alishinda nguvu za maovu alipozaliwa kama mwanadamu akafa msalabani kwa ajili ya dhamabi zetu. Kwa kuchagua maovu, mtu wa kwanza alijiuza na wakati huohuo wanadamu wote kuwa utumwa wa dhamabi. Hivi ndivyo tulivyopoteza uhuru. Yesu Kristo alikucha ili kutununua kutoka utumwa wa dhambi. Ni katika Yesu tu tunaweza kuwa huru na kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu.

Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.
(Yohana. 8:34–36)

Mungu, hutoi majibu yote kwa maswali yangu. Nizaidie nisikwasike kwa hilo. Badala yake nizaidie ili niweze kusisitiza kusikiliza yale ambayo umetangaza.
Mwandishi: 
Manu Ryösö
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Dhambi inaweza kuelezewa na manono mengi. Ni kupotoka, udanganyivu na upinzani wa mawazo, maneno na matendo. Kwa kifupi dhambi ni wakati moyo unamwacha Mungu.

Hali ya kuchagua maovu ambayo yanakaa katika wanadamu huitwa dhamabi ya asiri. Matunda yake ni tofauti na mawazo mabaya, matendo mabaya, maneno na kuacha kutenda mema.

Dhambi huumiza. huvunja and huraribu maisha. Unaweza kupata mifano kutoka kwako and maisha ya watu wengine. Hatimaye hali hasa ya Mwanadamu hujulikana mbele za sheria ya Mungu.

Kulingana na Biblia kila mwadamu ni mwenye dhambi. Hakuna hata mmoja wetu ambaye anaweza kuepukana na dhambi au madhara ya dhambi. Dhambi hututenganisha na Mungu na utakatifu wake. Mshahara mkubwa wa dhambi ni mauti na kutengana na Mungu milele. Hata hivyo, binadamu mwenyewe hawezi kujipatanisha na Mungu na madhara yake mbele za Mungu. Ni Mungu pekee anayeweza kutuzaidia.

Haki hii hutoka kwa Mungu kwa imani katika Yesu kristo kwa wate waaminio. Hakuna tofauti, ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti; kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu”
(Warumi 3:22–24).

Mungu, unihurumie mimi mwenye dhambi!
Mwandishi: 
Manu Ryösö
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Mungu alimtuma mwanawe afe mslabani miaka 2000 iliyopita. Yesu Kristo alipopigiliwa msumari msalabni alichukua ubinafsi wako, kutoamini, uchoyo,kutokuwa mwaminifu na dhambi zote zingine mapegani mwake. Mungu alitibithisha msamaha wa dhambi alipomfufua mwanae kutoka kwa wafu.

Dhambi husamahewa ikiwa mtu akiamini ubatanisho alioupata msalabani. Tunazungumza juu ya zawadi ambayo tunapewa bure. Mwanadamu haitaji kwanza kusafisha maisha yake na wala kukamua imani kutoka kwake mwenyewe. Tunaweza kupata kwa uraisi neema ambayo iko tayari kwa ajili yetu. Mungu alifahamu kuwa hatuwezi kupatanisha dhambi zetu na hivyo alifanya upatanisho mwenyewe.

Unaweza kuamini kuwa dhambi zako zote zimesamahewa kwa ajili ya Yesu kristo. Haijalishi jinsi hali yako ilivyo au amefanya nini, unaweza kuamini kwa uhakika kuwa umesamehewa. Mbele za Mungu matendo yetu mema au maendeleo yetu hayatoshi. Haifai chochote kumwonyesha, kwa sababu ya kifo cha Yesu msalabani ambacho ni tendo jema la Mungu linalotosharesha.

yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
(2 Wakorintho 5:19,21)

Mungu mwema, asante kwa neno la msalaba. Ahsante kwamba kwa ajili ya Yesu ninaweza kuamini kuwa dhambi zangu zimesamehewa.
Mwandishi: 
Manu Ryösö
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Mwanadamu ana shida ya kuelewa jinsi dhamani alivyo na nguvu kubwa. Tusingaliweza kufikiria swali kama hili kama tungeweza kuona kweli jinsi uaribifu huu mkuu wa nguvu hii.

Hali ya dhambi ndiyo inatutenganisha na Mungu mtoaji uzima na mwokozi. Kwa nini kumpinga, yeye ambaye pekee yake anaupendo kwetu usio na kipimo na amejitoa kwa ajili yetu?

Dhambi humuhumiza mkosanji na watu ambao wanao mzuka. Kutenda dhambi makusudi ni kudharau mateso ya Yesu. Kwa kweli ilibidi afe kwa ajili ya ubinafsi na kutotii kwa mwanadamu. Kwake yeye ambaye dhamani ya msamaha wake imekuwa wazi, ambao huwezi kupuuzwa na kuendelea kutenda dhambi tena.

Dhambi ni uovu dhidi ya maisha, hata kama hatuoni bayana uhusiano. Dhambi ina madhara yake, iwe kwa mkosaji au kwa watu wengine. Dhambi huchafua dhamiri na kwa haraka huelekea katika hali mbaya. Mkristo anaondolewa kutoka giza kuingia katika nuru katika ubatiso na anaitwa kupigana na dhambi kwa msaada wa Mungu.

…uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani.
(1. Timotheo 1:19)

Mungu uniehepushe kutoka dhambi na maovu yote. Niongoze kwamba matendo yangu na maisha yangu yakupendeze.
Mwandishi: 
Manu Ryösö
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Mlango wa neema ya Mungu uko wazi maadamu tu kuna swali hili katika moyo “ Ninaweza kusamahewa bado?” kadiri dhambi inavyoendelea kuleta majuto moyoni, ndivyo msamaha wa Yesu ni kimbilio.

Wakati mwingine tunaweza kupotea kwa kufikiri kuwa hakuna neema inatotutosha. Dhambi ambayo nimeifanya ni kubwa sana kiasi kwamba haiwezi kusamahewa tena. Haya ndio mawazo ambayo kwa furaha ananongoneza katika masikio yetu. Hivi ndivyo anataka kutupotosha kutoka kwa Mungu. Ni kweli kwamba yale ambayo yamefanyika hayawezi kurudishwa tena, lakini neema ya Mungu hufunika kabisa dhambi zote. Kwa hivyo tunaweza kuendelea kuamini vema msamaha wa Mungu.

Kwa sababu sisi ni wanadamu wenye dhambi, tunaendelea kuanguka katika dhambi tena na tena. Mungu hata hivyo husamahe tena na tena. Ni kupitia kwa msamaha wake tunaweza kupokea nguvu ya kupigana na dhambi. Dhambi ni adui hatari na tutapigana naye hadi kifo.

Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. 23 Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu. BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
(Maombolezo 3:22–23, 25).

Mungu imesemwa juu yako kuwa “Neema yake yadumu milele”. Ahsante kwamba ninaweza kuami maneno haya. Nisafishe na kunipa mwanzo mpya.
Mwandishi: 
Manu Ryösö
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Kusamehe kunaweza kuwa vigumu na pengine kutowezekana. Si hoja, katika Biblia tunatiwa moyo kuomba msamaha na kusamehe. Kwa kweli, inetamkwa kwa nguvu kwamba hatutasamehewa kama hatutasameheana.Tufanye nini basi, wakati hatuwezi kusamahe na uchungu unasumbua moyo?

Kwa kabisa, ni muhimu kwamba tuweze kukiri dhambi hii mbele za Mungu. Tulete ukweli huu mbele zake kwamba tunmeshindwa kusamehe. Kwa ajili ya Yesu tunaweza kuamini kuwa hata dhambi hii imesamahewa. Wakati huo huo tuombe kwamba Mungu kwa neema yake anaweza kufanya kazi yake ndani yatu na atuzaidie tuweze kusamahe. Ni kwa msaada wa neema yake tu vidonda katika mioyo yetu vinaweza kupona kabisa. Mazungmzo na mwanasaikogia au mchungaji au mtu aliyetukosea inaweza kuwa msaada mwema.

Kusamehe ni uamzi tunauchukua. Kama hali, msamaha unaeza kuwa hata hivyo hatua ndefu. Inaweza kuchukua hata miaka ili kuweza kuwa huru kutokana na uchungu. Hata hapo ni muhimu kuachilia hali ya kulipisa kisasi.

tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
(Waefeso 4:32)

Mungu mwenye neema, unajua mambo yangu yote yaliyo moyoni mwangu. Niepushe na kutokuwa na moyo mugumu na uchungu.
Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Biblia inazunguamzia juu ya shetani, ijapokuwa kwa nadra. Yeye si sawa wala kinyume na nguvu za Mungu. Yeye kiumbe cha Mungu. Sababu zilizopo shetani kuwa mwovu kwa asili zinaonekana kuwa sababu zilizosababisha mwanadamu kuanguka: Kiburi, tamaa ya kuwa sawa na Mungu. Kwa sababu Mungu alikuwa na mapenzi mema kuhusu uumbaji wake na kwenda kinyume na mapenzi yake ni uovu kabisa. Hivyo shetani kila hali ya kumpinge Mungu.

Shetani anashughulikaje? Biblia inafundisha kwamba anafanya kazi ndani ya watu wasiotii” kama hatufuati mapenzi ya Mungu, tunafuata mapenzi ya adui wa Mungu na hivyo kuwa katika himaya ya shetani. Hata hivyo tunaweza kubadilisha msimamo kwa kumkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozin wetu.

“Vaeni silaha za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shetani kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya ufalme na mamlaka, juu ya mkuu wa giza, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”
(Waefeso 6:11-12 SUV)