Je ninaweza kuendelea kupokea msamaha kutoka Mungu?

Mwandishi: 
Manu Ryösö
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Mlango wa neema ya Mungu uko wazi maadamu tu kuna swali hili katika moyo “ Ninaweza kusamahewa bado?” kadiri dhambi inavyoendelea kuleta majuto moyoni, ndivyo msamaha wa Yesu ni kimbilio.

Wakati mwingine tunaweza kupotea kwa kufikiri kuwa hakuna neema inatotutosha. Dhambi ambayo nimeifanya ni kubwa sana kiasi kwamba haiwezi kusamahewa tena. Haya ndio mawazo ambayo kwa furaha ananongoneza katika masikio yetu. Hivi ndivyo anataka kutupotosha kutoka kwa Mungu. Ni kweli kwamba yale ambayo yamefanyika hayawezi kurudishwa tena, lakini neema ya Mungu hufunika kabisa dhambi zote. Kwa hivyo tunaweza kuendelea kuamini vema msamaha wa Mungu.

Kwa sababu sisi ni wanadamu wenye dhambi, tunaendelea kuanguka katika dhambi tena na tena. Mungu hata hivyo husamahe tena na tena. Ni kupitia kwa msamaha wake tunaweza kupokea nguvu ya kupigana na dhambi. Dhambi ni adui hatari na tutapigana naye hadi kifo.

Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. 23 Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu. BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
(Maombolezo 3:22–23, 25).

Mungu imesemwa juu yako kuwa “Neema yake yadumu milele”. Ahsante kwamba ninaweza kuami maneno haya. Nisafishe na kunipa mwanzo mpya.