Kama Mungu ameumba kila kitu, maovu yanatoka wapi?

Mwandishi: 
Manu Ryösö
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Biblia haitwambii kila kitu. Inatutangazia yale ambayo ni muhimu kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, Mwanzo wa maovu ni miongoni mwa yale mambo ambayo inazungumzia kidogo sana juu yake.

Mwanzo wa Biblia inatibithisha kimsingi kuwa mwanadamu ana uhuru wa kuchagua mema na mabaya. Dunia na mwadamu viliumbwa ili viwe vyema, lakini mwanadamu alichagua uovu alipodanganywa na shetani. Ibilisi ni kiumbe cha Mungu pia. Imesemekan kwamba kwanza ni mwanadamu ambaye alimpinga Mungu. Shetani alimvuta mwanadamu kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu na hivyo ndivyo maovu yalienea duniani.

Kwetu sisi imebaki muujiza kwa nini Mungu mwema aliruhusu maovu kuingia duniani. Hata hivyo, ni wazi kwamba Mungu mwenyewe alishinda nguvu za maovu alipozaliwa kama mwanadamu akafa msalabani kwa ajili ya dhamabi zetu. Kwa kuchagua maovu, mtu wa kwanza alijiuza na wakati huohuo wanadamu wote kuwa utumwa wa dhamabi. Hivi ndivyo tulivyopoteza uhuru. Yesu Kristo alikucha ili kutununua kutoka utumwa wa dhambi. Ni katika Yesu tu tunaweza kuwa huru na kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu.

Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.
(Yohana. 8:34–36)

Mungu, hutoi majibu yote kwa maswali yangu. Nizaidie nisikwasike kwa hilo. Badala yake nizaidie ili niweze kusisitiza kusikiliza yale ambayo umetangaza.