Je kutenda dhambi kuna maana yeyote kama mtu amesamahewa?

Mwandishi: 
Manu Ryösö
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Mwanadamu ana shida ya kuelewa jinsi dhamani alivyo na nguvu kubwa. Tusingaliweza kufikiria swali kama hili kama tungeweza kuona kweli jinsi uaribifu huu mkuu wa nguvu hii.

Hali ya dhambi ndiyo inatutenganisha na Mungu mtoaji uzima na mwokozi. Kwa nini kumpinga, yeye ambaye pekee yake anaupendo kwetu usio na kipimo na amejitoa kwa ajili yetu?

Dhambi humuhumiza mkosanji na watu ambao wanao mzuka. Kutenda dhambi makusudi ni kudharau mateso ya Yesu. Kwa kweli ilibidi afe kwa ajili ya ubinafsi na kutotii kwa mwanadamu. Kwake yeye ambaye dhamani ya msamaha wake imekuwa wazi, ambao huwezi kupuuzwa na kuendelea kutenda dhambi tena.

Dhambi ni uovu dhidi ya maisha, hata kama hatuoni bayana uhusiano. Dhambi ina madhara yake, iwe kwa mkosaji au kwa watu wengine. Dhambi huchafua dhamiri na kwa haraka huelekea katika hali mbaya. Mkristo anaondolewa kutoka giza kuingia katika nuru katika ubatiso na anaitwa kupigana na dhambi kwa msaada wa Mungu.

…uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani.
(1. Timotheo 1:19)

Mungu uniehepushe kutoka dhambi na maovu yote. Niongoze kwamba matendo yangu na maisha yangu yakupendeze.