Yesu

Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Wakristo wa kwanza, walimtambua Yesu kama mwokozi wao. Waliamini kwamba Yesu ni mwana wa Mungu aliyekuja duniani kama mwanadamu, kuna kifungu kinachosema “Yesu ni Bwana” kinadhaihirisha hakika imani yao.

Injili ndani ya agano jipya inatuambia habari njema kuhusu Yesu, jinsi alivyochukuliwa mimba kwa Roho mtakatifu na kuzaliwa na bikira Maria, na jinsi alivyoishi, kufundisha na kutenda miujiza mingi. Je! Yesu ni nani basi? Mateso yake, kifo chake na kufufuka kwake siku ya tatu ndicho kiini cha ukristo.

Je! Yesu ni nani kwako?
Ufahamu wako juu ya Yesu, na yeye ni nani kwako Inakupa umilele. Kwa hiyo soma bibilia na tafuta zaidi kujua.

Kwa kufa kwake juu ya msalaba kwa ajili ya dhambi zetu, na kufufuka kwake kutoka kwa wafu, Yesu alifanya njia kwetu ya kumjua yeye katika viwango vyetu wenyewe. Ni kupitia Yesu tu tunaweza kuokolewa na kuwa na uhusiano na Mungu.

“Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.”
(Matendo ya mitume 4:12 SUV)

Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Wasomi na wanahistoria hawawezi kukataa historia ya Yesu.

Maana mtu aitwaye Yesu alikulia Galilaya katika mji utwao Nazareti na mara zote ililetwa kwetu kama Yesu wa Nazareti. Yesu alifundisha katika sehemu nyingi, alikusanya waliomfuata, Wanafunzi wake ambao walikusanya mafundisho yake na kuyasambaza. Takribani mwaka wa 30 huko Yerusalemu Pontio Pilato alitoa amri Yesu auwawe. Wanahistoria wanakubaliana na kweli hizi.

Lakini Yesu alikuwa ni nani? Naweza kupata kumjua vizuri? Majibu ya maswali haya yanaweza kupatikana ndani ya Biblia, zaidi ndani ya agano jipya.

“Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo Mwana wa Mungu.”
(Marko 1:1 SUV)

Yesu! Wewe Ni Nani?
Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Yesu alipata adhabu ya kifo kwa sababu wazee wa kiyahudi walidai alimdhihaki Mungu. Kwa mafundisho yake na miujiza, Yesu alijiita kwamba yeye ni mwana wa Mungu alikuja chini kutoka mbinguni. Kutokana na sheria ya Musa mtu anayedai kuwa yeye ni Mungu alihesabika kama anakufuru, ni kafiri na nilazima apate adhabu ya kifo.

Hata hivyo ni warumi waliooweza kutoa hukumu ya kifo. Mtawala pontio pilato hakuwa anavutiwa sana katika magomvi ya dini kati ya viongozi wa kiyahudi. Hata hivyo pilato hakushawishiwa, hata hivyo alitoa hukumu ya kifo kwa kulazimishwa ili Yesu asulubishwe. Yeyote atakaye soma habari ya kifo cha Yesu na kusulubishwa kwake, ndani ya injili anaweza kushangaa kwanini mtu mzuri na asiye na makosa afe kifo cha kusikitisha hivyo. Kwanini Yesu hakujilinda mwenyewe kwa mabaya aliyoshtakiwa nayo?

Tunapata majibu kutoka kitabu cha “Isaya 53" - cha kushangaza yaliandikwa miaka miatano kabla ya kifo cha Yesu. Kama wakristo tunaamini hivyo na mistari mingine katika Biblia inavyosema, yote hii ilikuwa ni mpango wa Mungu kwa wokovu wetu. Yesu alikufa juu ya msalaba kwa dhambi zetu, Mungu alimtuma Yesu mwanaye wa pekee ili afe na kuteseka ili sisI tusiteseke hivyo Alizipatanisha dhambi zetu.

"bali alijeruhiwa kwa makosa yetu alichubuliwa kwa maovu yetu adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kupigwa kwake sisi tumepona sisi sote kama kondoo tumepotea kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote”.
(Isaya 53:5-6 SUV)

Bwana Yesu siwezi kutambua mateso uliyopitia lakini na amini dhambi zangu zimesamehewa.
Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Ni sehemu mbili zinatueleza tangu mwanzo – ni ipi unayoiamini?

Injili ya mathayo inatuambia kwamba walinzi katika kaburi la Yesu walipewa rushwa na kutoa maelezo na kusema kwamba wanafunzi wake walikuja usiku na kuiba mwili wa Yesu. Uongo huu unaendelea hata leo na unaendelea kuboreshwa, maelezo ya leo ni kwamba kifo cha Yesu kilisababisha mkanganyiko wa kiakili kwa wanafunzi. Hivyo njia moja tu kwako kuendelea kuishi ni kutengeneza imani, kuamini kwamba Yesu alifufuka katika wafu na kupitia imani anaishi katika roho.

Agano jipya hata hivyo linatuambia kwamba kuna watu wengi walikutana na Yesu katika hali ya kimwili. Wanawake katika kaburi, wanafunzi waliokuwa wamefunga milango kwa uwoga watu wawili katika safari ya Emau Tomaso mwenye mashaka alipata nafasi ya kugusa majeraha ya Yesu. Watu hao walikuwa na vitu vinavyofanana wote, walikuwa na muda mgumu wa kuelewa na kukubali kwamba Yesu alifufuka hakika kutoka kwa wafu.

Baada ya fufuko wake Yesu hakujionyesha kwa washtaki wake au ulimwengu mzima ni kaburi tupu tu ndilo lilidhihirisha hivyo. Mwili wake haukuwepo kaburini.

Ni kiasi gani tunaweza kuhakiki hiyo kazi au kutoa sababu ambayo inaweza kumshawishi mtu kuhusu ufufuko wa Yesu- imani inakuja unapokutana na Yesu. Yesu yuko mbinguni na baba yake, lakini neno lake Biblia linazidi kumzungumza na watu wote ulimwenguni. Na kanisa linahakikisha kwamba Yesu yu hai.

”Yesu akamwambia kwa kuwa wewe umeniona, umesadiki; waheri wale waio ona wakasadiki.”
(Yohana 20:2a SUV)

- Yesu wasema kwamba unaishi. Unaweza kusikia wakati naomba?
Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Njia nzuri ya kupata kumjua Yesu ni kusoma kuhusu yeye ndani ya Agano jipya ambacho ni kitabu kilichoenea ulikwengu mzima yaani Bibilia. Tunaweza kusoma kile ambacho alifundisha, nini alifanya akiwa duniani na kusoma hadhithi ya watu waliomjua Yesu na kutembea naye.

Biblia inatuambia maisha ya Yesu kifo chake na kufufuka kwake. Kuna baadhi ya barua zimeandikwa na mitume katika Agano jipya vile wakristo wa kwanza na kanisa la kwanza lilivyokuwa. Watu hawakukutana na Yesu moja kwa moja lakini walimjua yeye walimsoma na kusikia habari zake.

Hata leo kuna watu wanomjua Yesu. Unaweza kuwapata kanisani, mahali watu wanapokusanyika pamoja kujifunza kuhusu Biblia kuomba na kushiriki meza ya Bwana, tafuta kanisa na nenda moja kati ya hilo - huwezi kukuta tu watu wanaomjua Yesu lakini unaweza kupata kumjua Yesu wewe mwenyewe.

“basi Yesu akawajibu akasema mafunzo yangu siyo yangu mimi ila ni yake aliyenipeleka mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake atajua habari ya yale mafunzo kwamba yatoka kwa Mungu au kwamba mimi na nena kwa nafsi yangu tu.”
(Yohana 7:16-17 SUV)

- Yesu nataka kuwa na uhusiano na wewe. Jidhihirishe kwangu wewe mwenyewe.
Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Kila mkristo anaushuhuda wake ni vipi alipata kumjua Yesu. Mmoja aweza kuwa alipata mafunuo usiku, mwingine ilimchukuwa miaka mingi mpaka kuamini na mwingine alimjua Yesu tangia utoto wake, hakuna ushuhuda uliyomzuri zaidi ya mwingine. Hata hivyo nini kiliwafanya wawe wakristo kwa pamoja ni kwamba Bwana Yesu alifungua mioyo yao kupokea.

Hapa kuna kipande kifupi cha ushauri kuhusu wote wanaouliza kuhusu kuja kuwa wakristo: Acha kusita na kukimbia mbali na Mungu. Fungua masikio na sikiliza nin Bibilia inafundisha. Angalia nini Bwana amefanya kwa ajili yako. Mungu anakupenda na anataka mazuri kwako fanya maamuzi ya i imani hiyo inatosha.

Yote ya kufanya ni kutambua kwamba Yesu ni Mungu na omba kwa Mungu atakusamehe makosa yako. Na Biblia inatuambia kwamba Mungu anasikia maombi yetu yote na ameahidi msamaha wa dhambI kupitia Yesu Kristo. Imani si kuhusu hisia ni kuhusu kuamini katika moyo kwamba Yesu ameniokoa.

Wokovu ni zawadi kutoka kwa Mungu na ni kwa imani tunapokea zawadi hiyo. Kama umebatizwa umekuwa muumini maana umerudi nyumbani tena na kuwa na uhusiano na mwokozi wako. Tafuta kanisa pale utasikia msamaha wa Mungu na kushiriki Meza ya Bwana na wakristo wengine.

Yesu anawaita kila mmoja kwake ukiwa umebatizwa au hapana katika ubatizo tulisafishwa na kuunganishwa na wakristo wengine.

(Nini kitatokea kama sikubatizwa?)

“Kwa kuwa kila atakaye liitia jina la Bwana ataokoka.”
(Warumi 10:13 SUV)

- Bwana Yesu kristo mwana wa Mungu unirehemu mimi mwenye dhambi.