Yesu ni nani?

Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Wakristo wa kwanza, walimtambua Yesu kama mwokozi wao. Waliamini kwamba Yesu ni mwana wa Mungu aliyekuja duniani kama mwanadamu, kuna kifungu kinachosema “Yesu ni Bwana” kinadhaihirisha hakika imani yao.

Injili ndani ya agano jipya inatuambia habari njema kuhusu Yesu, jinsi alivyochukuliwa mimba kwa Roho mtakatifu na kuzaliwa na bikira Maria, na jinsi alivyoishi, kufundisha na kutenda miujiza mingi. Je! Yesu ni nani basi? Mateso yake, kifo chake na kufufuka kwake siku ya tatu ndicho kiini cha ukristo.

Je! Yesu ni nani kwako?
Ufahamu wako juu ya Yesu, na yeye ni nani kwako Inakupa umilele. Kwa hiyo soma bibilia na tafuta zaidi kujua.

Kwa kufa kwake juu ya msalaba kwa ajili ya dhambi zetu, na kufufuka kwake kutoka kwa wafu, Yesu alifanya njia kwetu ya kumjua yeye katika viwango vyetu wenyewe. Ni kupitia Yesu tu tunaweza kuokolewa na kuwa na uhusiano na Mungu.

“Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.”
(Matendo ya mitume 4:12 SUV)