Ninawezaje kumfahamu Yesu?

Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Njia sahihi ya kupata kumjua Yesu ni kusoma kuhusu yeye ndani ya Agano jipya ambacho ni kitabu cha chapekee ambacho kilichoenea ulikwengu mzima yaani Bibilia. Tunaweza kusoma kile ambacho alifundisha, nini alifanya akiwa duniani na kusoma hadhithi ya watu waliomjua Yesu na kutembea naye. Biblia inatuambia maisha ya Yesu kifo chake na kufufuka kwake.

Kuna baadhi ya barua zimeandikwa na mitume katika Agano jipya vile wakristo wa kwanza na kanisa la kwanza lilivyokuwa. Watu hawakukutana na Yesu moja kwa moja lakini walimjua yeye walimsoma na kusikia habari zake.

Hata leo kuna watu wanomjua Yesu. Unaweza kuwapata kanisani, mahali watu wanapokusanyika pamoja kujifunza kuhusu Biblia kuomba na kushiriki katika meza ya Bwana, tafuta kanisa na nenda moja kati ya hilo - huwezi kukuta tu watu wanaomjua Yesu lakini unaweza kupata kumjua Yesu wewe mwenyewe.

“basi Yesu akawajibu akasema mafunzo yangu siyo yangu mimi ila ni yake aliyenipeleka mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake atajua habari ya yale mafunzo kwamba yatoka kwa Mungu au kwamba mimi na nena kwa nafsi yangu tu.”
(Yohana 7:16-17 SUV)

Ombi: - Yesu nataka kuwa na uhusiano na wewe. Jidhihirishe kwangu.