Kwanini Yesu alikufa msalabani

Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Yesu alipawa adhabu ya kifo kwa sababu wazee wa Kiyahudi walidai alimdhihaki Mungu. Kwa mafundisho na miujiza yake, Yesu adhibithisha kuwa yeye ni mwana wa Mungu aliyeshuka kutoka mbinguni. Kulingana na na sheria ya Musa mtu anayedai kuwa yeye ni Mungu alihesabika kama anakufuru, na nilazima apate adhabu ya kifo.

Hata hivyo ni Warumi waliooweza kutoa hukumu ya kifo. Mtawala Pontio Pilato hakuwa haja malumbano ya kidni kati ya viongozi wa kiyahudi. Hivyo Pilato hakushawishiwa, hata hivyo alitoa hukumu ya kifo kwa kulazimishwa ili Yesu asulubishwe.

Yeyote anayesoma habari ya kifo cha Yesu na kusulubishwa kwake katika injili anaweza kushangaa kwa nini mtu mwema hivi na asiye na makosa afe kifo cha kusikitisha hivyo. Kwa nini Yesu hajitetea kwa uongo?

Tunapata majibu kutoka kitabu cha “Isaya 53" – cha ajabu haya yaliandikwa miaka mia tano kabla ya kifo cha Yesu. Kama wakristo tunaamini hili na mistari mingine katika Biblia inavyosema, kwamba haya yote yalikuwa ni mpango wa Mungu kwa wokovu wetu. Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, Mungu alimtuma mwane Yesu mwanaye wa pekee ili afe na kuteseka ili sis tusiteseke hivyo Alikuwa upatanisho wa dhambi zetu.

"bali alijeruhiwa kwa makosa yetu alichubuliwa kwa maovu yetu adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kupigwa kwake sisi tumepona sisi sote kama kondoo tumepotea kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote”.
(Isaya 53:5-6 SUV)

Ombi: Bwana Yesu siwezi kuelewa mateso uliyopitia lakini nina amini kwamba dhambi zangu zimesamehewa.