Ni kweli Yesu alifufuka kutoka kwa wafu?

Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Ni sehemu mbili zinatueleza tangu mwanzo – ni ipi unayoiamini?

Injili ya mathayo inatuambia kwamba walinzi katika kaburi la Yesu walipewa rushwa na kutoa maelezo na kusema kwamba wanafunzi wake walikuja usiku na kuiba mwili wa Yesu. Uongo huu unaendelea hata leo na unaendelea kuboreshwa, maelezo ya leo ni kwamba kifo cha Yesu kilisababisha mkanganyiko wa kiakili kwa wanafunzi. Hivyo njia moja tu kwako kuendelea kuishi ni kutengeneza imani, kuamini kwamba Yesu alifufuka katika wafu na kupitia imani anaishi katika roho.

Agano jipya hata hivyo linatuambia kwamba kuna watu wengi walikutana na Yesu katika hali ya kimwili. Wanawake katika kaburi, wanafunzi waliokuwa wamefunga milango kwa uwoga watu wawili katika safari ya Emau Tomaso mwenye mashaka alipata nafasi ya kugusa majeraha ya Yesu. Watu hao walikuwa na vitu vinavyofanana wote, walikuwa na muda mgumu wa kuelewa na kukubali kwamba Yesu alifufuka hakika kutoka kwa wafu.

Baada ya fufuko wake Yesu hakujionyesha kwa washtaki wake au ulimwengu mzima ni kaburi tupu tu ndilo lilidhihirisha hivyo. Mwili wake haukuwepo kaburini.

Ni kiasi gani tunaweza kuhakiki hiyo kazi au kutoa sababu ambayo inaweza kumshawishi mtu kuhusu ufufuko wa Yesu- imani inakuja unapokutana na Yesu. Yesu yuko mbinguni na baba yake, lakini neno lake Biblia linazidi kumzungumza na watu wote ulimwenguni. Na kanisa linahakikisha kwamba Yesu yu hai.

”Yesu akamwambia kwa kuwa wewe umeniona, umesadiki; waheri wale waio ona wakasadiki.”
(Yohana 20:2a SUV)

- Yesu wasema kwamba unaishi. Unaweza kusikia wakati naomba?