Yesu kweli alikuepo?

Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Wasomi na wanahistoria hawawezi kukataa historia ya Yesu.
Mtu aitwaye Yesu alikulia Galilaya katika mji utwao Nazareti. Hivyo mara kwa mara alijulikana kama Yesu wa Nazareti. Yesu alifundisha katika sehemu nyingi, alikusanya wafuasi, ambao walikusanya mafundisho yake na kuyasambaza. Takribani mwaka wa 30 huko Yerusalemu Pontio Pilato alitoa amri Yesu auwawe. Wanahistoria wanakubaliana na kweli hizi.

Lakini Yesu alikuwa ni nani? Nawezaje kumfahamu vema? Majibu ya maswali haya yanaweza kupatikana ndani ya Biblia, zaidi ndani ya agano jipya.

“Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo Mwana wa Mungu.”
(Marko 1:1 SUV)

Ombi: Yesu! Wewe Ni Nani?