Dhambi zinewezaje kusamehewa?

Mwandishi: 
Manu Ryösö
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Mungu alimtuma mwanawe afe mslabani miaka 2000 iliyopita. Yesu Kristo alipopigiliwa msumari msalabni alichukua ubinafsi wako, kutoamini, uchoyo,kutokuwa mwaminifu na dhambi zote zingine mapegani mwake. Mungu alitibithisha msamaha wa dhambi alipomfufua mwanae kutoka kwa wafu.

Dhambi husamahewa ikiwa mtu akiamini ubatanisho alioupata msalabani. Tunazungumza juu ya zawadi ambayo tunapewa bure. Mwanadamu haitaji kwanza kusafisha maisha yake na wala kukamua imani kutoka kwake mwenyewe. Tunaweza kupata kwa uraisi neema ambayo iko tayari kwa ajili yetu. Mungu alifahamu kuwa hatuwezi kupatanisha dhambi zetu na hivyo alifanya upatanisho mwenyewe.

Unaweza kuamini kuwa dhambi zako zote zimesamahewa kwa ajili ya Yesu kristo. Haijalishi jinsi hali yako ilivyo au amefanya nini, unaweza kuamini kwa uhakika kuwa umesamehewa. Mbele za Mungu matendo yetu mema au maendeleo yetu hayatoshi. Haifai chochote kumwonyesha, kwa sababu ya kifo cha Yesu msalabani ambacho ni tendo jema la Mungu linalotosharesha.

yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
(2 Wakorintho 5:19,21)

Mungu mwema, asante kwa neno la msalaba. Ahsante kwamba kwa ajili ya Yesu ninaweza kuamini kuwa dhambi zangu zimesamehewa.