Kwa nini kuna shida duniani?

Mwandishi: 
Manu Ryösö
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Hili ni swali ambalo mwadamu amefikiriwa sana tangu zamani. Kama Mungu mwenye enzi na Mungu mwema yupo kwa nini anarushusu vita, njaa, mauaji na mambo mengine ambayo yanaharibu maisha? Si angekuwa na uwezo wa kuzia haya yote?

Biblia imeliacha swali hili wazi. Mambo mengine yamejibiwa ila maswali mengine mengi yako hewani tu. Mojawapo ya mitazamo ni kwamba duniani kuna shida ambazo zimesababishwa na mwanadamu mwenyewe. Vita, mateso, uasherati na hali zingine nyingi za kuumiza zimezababishwa na mwadamu. Mwadamu hawezi kumlaumu Mungu kwa haya yote ila lazima atajizame katika kioo.

Katika dunia hii, kuna mateso ya aina nyingi ambayo yamesababishwa na mwanadamu mwenyewe. Haya yote ni pamoja kwa mfano magonjwa na shida za hali ya hewa. Kwa nini Mungu asizuie haya yote yasitendeke? Haya yamebaki siri kwetu. Inaonekana hata hivyo kuwa mambo mengine ni hali ambayo Mungu anayatumia kuwaleta watu kwake. Pengine sababu moja wapo ya mateso hapa duniani ni ili mwadamu ajue jinsi alivyo mdogo ili aweze kumgeukia Mungu. Kwa upande mwingine shida huwaleta watu kukaribia mapenzi ya Mungu kwamba tuweze kuzaidia wale ambao wana mahitaji. Faraja yetu na tumaini ni neno la Kristo aliye fufuka- mshindaji wa mauvu na mateso.

Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini BWANA humponya nayo yote.
(Zaburi 34:19)

Mungu, uovu na mateso yanasumbua moyo wangu. Utuokoe na huovu!