Dhambi ni nini?

Mwandishi: 
Manu Ryösö
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Dhambi inaweza kuelezewa na manono mengi. Ni kupotoka, udanganyivu na upinzani wa mawazo, maneno na matendo. Kwa kifupi dhambi ni wakati moyo unamwacha Mungu.

Hali ya kuchagua maovu ambayo yanakaa katika wanadamu huitwa dhamabi ya asiri. Matunda yake ni tofauti na mawazo mabaya, matendo mabaya, maneno na kuacha kutenda mema.

Dhambi huumiza. huvunja and huraribu maisha. Unaweza kupata mifano kutoka kwako and maisha ya watu wengine. Hatimaye hali hasa ya Mwanadamu hujulikana mbele za sheria ya Mungu.

Kulingana na Biblia kila mwadamu ni mwenye dhambi. Hakuna hata mmoja wetu ambaye anaweza kuepukana na dhambi au madhara ya dhambi. Dhambi hututenganisha na Mungu na utakatifu wake. Mshahara mkubwa wa dhambi ni mauti na kutengana na Mungu milele. Hata hivyo, binadamu mwenyewe hawezi kujipatanisha na Mungu na madhara yake mbele za Mungu. Ni Mungu pekee anayeweza kutuzaidia.

Haki hii hutoka kwa Mungu kwa imani katika Yesu kristo kwa wate waaminio. Hakuna tofauti, ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti; kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu”
(Warumi 3:22–24).

Mungu, unihurumie mimi mwenye dhambi!