Kwa nini nisome Biblia?

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Maneno ya ajabu ya kwanza ya Injili ya Yohana hutuambia maneno ya Biblia: Mungu aliuumba dunia kupitia Kristo. Yalitekwa na giza ambayo hakuna mwanadamu hata mmoja anayeweza kumtafuta Mungu kamwe kwa nguvu zake. Huwezi kukaribia, huwezi kusikia sauti yake, huwezi kumwomba ushauri wake. Hali hii ilibadilishwa Kristo alipozaliwa katika dunia hii: “Nuru imengaa gizani.”

Kulinga na imani ya Kanisa letu, Kristo ndiye nuru ya ulimwengu na njia pekee ya kwenda kwa Mungu. Mwanga huja kwetu katika Biblia, neno la Mungu. Mungu hazungumzi nasi moja kwa moja lakini Roho wake Mtakatifu huzungumza kwa neno lake ambalo ni hai na lenye nguvu.

Bado hatuwezi kumkaribia, hatuwezi kusikia sauti yake bado wala kuuliza ushauri wake. Lakini tunao nuru ya neno lake, na mwanga huu hutuongoza nyumbani kwa mwanga.

Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. (Yohana 1:14)

Ee Mungu, niangazie nuru yako na katika mapito yangu. Nizaidie nimfahamu mwanao Yesu.