Kwa nini niamini yale Biblia hufundisha?

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Kuna vitabu vitakatifu kadhaa kuniani. Biblia ni mmoja wapo. Kwa nini ni Biblia na wala si vingine, kwa mfano mojawapo kitabu ambacho cha zamani kuliko Biblia?

Sasa, tunaelekea katika somo ambalo ninaponyoka fikra na mawazo ya binadamu. Wakristo hawawezi kutumia fikra za binadamu kuwahakikishia wale ambao wana mashaka kuwa Biblia tu ndio neno la Mungu na wala si kama vitabu vingine vinavyo dai kichwa hiki. Hatujalinganisha mkusanyiko wa vitabu vyote vya zamani na baada kufikiria, kuchagua mojawapo kama vile unaponunua simu mpya. Walimu wa zamani wa Kilutheri walisema katika maneno makali. Ni hali ya Biblia kuwa inamtibithishia musomaji kuwa kwa uhakiki ndiyo neno la Mungu. Kwa njia hii mamlaka ya neno la Mungu hayategemei na maamuzi yanayotolewa na Kanisa, kwa mazungumzo ya kueleweka au utafiki wa kisasa. Haitegemei chochote ila ukuu na nguvu za Mungu.

Hii ndio sababu msomaji wa Biblia anaweza kuhakikishiwa kwamba Mungu anamzungumzia.Msomaji mwingine anaweza asikubaliane na mawazo haya. Kulingana na imani yetu, hii inamaanisha kwamba nuru ya Mungu haifikii moyon wa kila mtu.

Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa.
(1 Wakorintho 1:20-21)

Mungu, umenipa fahamu zangu zote. Nizitumie vema kwa faida zangu na wengine.