Je Biblia ni ukweli?

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Ndio. Ila ni kosa kubwa kupima hili kutumia vipimo vya wanadamu.

Kwa karne nyingi, Wakristo ambao walikosa kukubaliana mambo mengine angalau walikubaliana kuwa Biblia ni kweli na ni neno la Mungu. Hawakukubalina tu juu ya tafsiri ambazo zinatolewa kwake. Kama Karne moja na nusu iliyopita, uchunguzi wa historia na sayansi ulianza kuuliza juu ya ukweli wa Biblia na Wakristo walijibu kwa njia tofauti. Wengine walianza kutibithisha kuwa Biblia ni neno la Mungu kwa kukataa habari mpya kinyume na Biblia. Wakristo wengi bado hufanya hivi.

Walipokea tu, mawazo ya namna hii hutuongoza katika kufikiria katika njia ifwatayo: Ili iwe neno la Mungu Biblia inahitaji kuendana na akili na sayansi ya elimu. Kujaribu kuchukua msimamo huu huchukua nguvu zetu zote, na tuna uzoefu mkubwa juu ya jambo hili.

Uweli wa neno la Mungu hautegemei mawazo ya kibinadamu wala elimu. Uweli wa Biblia umejengwa juu ya ukweli kwamba Mungu anajitambulisha na mapenzi yake kwetu katika mfumo wa maandishi. Ni jambo la imani, ambalo ni zawadi kutoka kwa Mungu. Kwa sababu fulani wapitaji katikati ya soko la Thessalonika walitambua wito wa Mungu katika mazungumzo ya watu . Paulo anaelewa kuwa hii ni kazi ya Mungu.

Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.
(1 Wathesalonike 2:13)

Mungu wewe si kisiwi na neno lako si bure. Usinyamaze kwangu pia lakini naomba nisikie sauti yako.