Ubatizo ni Nini?

Mwandishi: 
Jari Rankinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Mchungaji anamwaga maji juu ya kichwa cha mtoto na kumbatiza yeye katika jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Na kama hili halikufanyika kwa mtoto, linaweza kufanyika hata kwa mtu mzima. Kwa nini?

Yesu aliamuru tupatize. Alisema kwamba kupitia ubatizo mtu hufanyika kuwa mwanafunzi wake. Kupitia ubatizo tunakuwa watoto wa Mungu, na kupata zawadi ya msamaha wa dhambi na uzima wa milele. Biblia inasema tulivikwa Kristo wakati wa ubatizo. Kutoka hapo kuendelea mbele kimbilio letu ni ndani ya kile Yesu anafanya kwa ajili yetu.

Ni asili yetu kushangaa ni kwa jinsi gani maji yanaweza kufanya mambo makubwa kama haya. Mungu ameahidi kutenda wakati mtu anabatizwa. Ameahidi kumchukua mtu kama mtoto wake,kumsamehe na kumwokoa. Mungu amechagua njia hii kutufanya sisi wake kwa kile Yesu alifanya. Hakika kuna hekima kubwa kwa kazi Mungu aliyofanya kwa njia ya Yesu Kristo.

"Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkawabatize kwa jina la Baba, na Mwana na Roho mtakatifu”.
(Mathayo 28:19-20, SUV)