Ubatizo wangu una maana?

Mwandishi: 
Jari Rankinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Nilibatizwa zamani. Hii ina maana gani sasa? Je ina maana yeyote? Kwa mimi ubatizo una maana kubwa wakati nikiwa mtoto nilibatizwa sikuwa na la kufanya sikujua, wala kufanikiwa au kubadilisha. Si hata kitu kidogo. Nikiwa ndani ya kutokamilika, kutokujua au kuwa mzuri- nilifaa kwa Mungu. Nilikuwa mkamilifu kwa sababu Yesu alikufa kwa ajili yangu na aliyepatanisha dhambi zangu. Ilikuwa hivyo na iko hivyo sasa. Hivi ndiyo ubatizo unavyonikumbusha mimi.

Tunaweza kujikumbusha kila asubuhi maana ya ubatizo wetu una maana gani: kama nilivyo mimi ni mali ya Mungu na ninaenda mbinguni. kama nilivyo, ninawezakupata suluhisho kwa Yesu. Sasa hii inaleta furaha na heshima. Hili ni jambo ambalo linaleta nguvu na kuishi kama mkristo na kuishi kwa mapenzi ya Mungu hata kama kwa kiasi kidogo.

Biblia hufundisha kwamba tumeokolewa kwa neema. Kwa kuokolewa kwa neema ina maana kwamba tunaweza kuwa mali ya Mungu pasipo kuwa na kuchangia na kuipata mbingu kama jinsi tulivyo na yote hii ni kwa sababu ya kazi ya Yesu msalabani. Kila mtu aliyebatizwa na kuamini katika Yesu ataokolewa kwa neema.

“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu."
(Efeso 2:8 SAV)