Roho Mtakatifu ni nani?

Mwandishi: 
Ville Auvinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Biblia inatwambia kwamba kuna Mungu mmoja mwenye nafsi tatu; Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Na kila moja ya nafsi ina huduma yake. Mungu Baba aliumba ulimwengu na anaendelea kuutunza. Na Mungu Mwana alizaliwa katika mwili wa binadamu na kuaokoa ulimwengu kutoka katika dhambi. Roho Mtakatifu anaamsha na kujenga imani ndani ya mwanadamu. Kwa hiyo lazima tuulize “Roho Mtakatifu ni nani?" Kwa sababu Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Mungu na wala sio nguvu inayojitegemea.

Roho Mtakatifu anafanya kazi kati ya mtu akiamsha na kuimarisha imani katika Yesu. Anafanya kazi kupitia vyombo vya Neema: neno la Mungu, Ubatizo na Meza ya Chakula cha Bwana (sacramenti) na ungamo la dhambi; hivi ni vyombo vya Neema.

Yesu alimwita Roho Mtakatifu “Roho wa Ukweli” na Mlinzi, kama Roho wa ukweli, Roho Mtakatifu aliwaongoza waandishi wa Biblia kuandika katika mapenzi ya Mungu, na yeye anatupa kuelewa pale tunaposoma Biblia . Kama Mlinzi anatuhakikishia katika roho zetu kwamba Mungu ni wa rehema kwetu kupitia Yesu Kristo ijapokuwa tumeanguka na kustahili adhabu.

Ndani ya waamini Roho Mtakatifu anatoa uzima ambao unatokana na mapenzi ya Mungu na pia anatoa zawadi za Roho kulijenga Kanisa.

“Lakini ajapo huyo msaidizi nitakayewapelekea, kutoka kwa Baba, yaani Roho wa kweli, atokaye kwa baba yeye atanishuhudia"
(John 15:26, SUV)

Ombi: Mungu, niongoze kwako wewe.