Unweza kuwa na Roho Mtakatifu?

Mwandishi: 
Ville Auvinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Roho Mtakatifu anaweza kuishi ndani ya mwanadamu, hakika, kila muumini katika Yesu Kristo ana Roho Mtakatifu. Pasipo Roho Mtakatifu hakuna anayeweza kuamini. Mojawapo ya mambo yasiyoeleweka ya ukristo ni kwamba Mungu mwenye nguvu anatamani kuishi ndani ya moyo wa mwanadamu mdogo na mwenye dhambi.

Roho Mtakatifu anakuja kwenye moyo wa mwanadamu kupitia Neno la Mungu na kupitia sakramenti ya ubatizo na sacramenti ya Meza ya Bwana. Kwa Kutumia hivi vyombo vya Neema anaamsha imani ya kweli (uokoayo) ndani ya Yesu Kristo katika Moyo wa mwanadamu na kumfanya mtoto wa Mungu. Mtoto wa Mungu hata hivyo anaweza kukosa utii na kumhuzunisha Roho Mtakatifu na kuanguka katika kutoamini. Hii ndio maana Biblia inaonya kuhusu watu wenye mioyo migumu, na waasi na wanaojiinua, wapate kurudi tu kwa Mwokozi.

“Lakini Roho wa Mungu anakaa ndani yenu ninyi hamwufuati mwili, bali mwaifuata Roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyo si wake”
(Warumi 8:9,SUV)