Nitapata wapi msaada wakati naogopa kifo?

Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Kutoka kwa Yesu. Ni asili kwamba tunaogopa kifo. Kifo na washirika wake- magonjwa, ajali majanga yote ni ya muovu, si sehemu ya uumbaji wa Mungu. Kifo kwa hakika si cha asili na hutakiwi kuwa rafiki nacho. Paulo alisema “kifo ni adui wa mwisho. lakini kazi ya Yesu ni ushaidi imara kwamba kifo na washirika wake hawatashinda.”

Yesu ameshinda kifo, na wewe kama mtoto wake utatokea kupitia kifo kama mshindi. Sikia kwa makini wewe mwenyewe. Hakikisha unajikabidhi kwa Yesu. Atakikabili kifo chako moja kwa moja. Hata kama unaogopa bado. Fanya kama vile mtoto mdogo wanavyofanya anpokuwa na hofu: Mkikimbilie baba yako. Anatuliza hali. hata kama usiku ni mrefu na wa giza. Hisia hushindwa mara nyingi, lakini Imani ambayo inaamini katika Neno la Mungu, haitashindwa.

“Yesu akamwambia, mimi ndimi huo ufufuo, na uzima aniaminiye mimi,ajapokufa atakuwa anaishi, naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa milele, je! Unayesaidika hayo?"
(John 11:25-26, SUV)

Ombi: Mungu bado kifo kinaniogofya. Utakuwa pamoja nami?