Kuna Jehanamu?

Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Jibu ni ndio. Agano la kale linasema waziwazi kuhusu mahali baada ya kufa, lakini kati ya kipindi cha Agano jipya na Yesu,Ufunuo umetoa mwanga hata katika zama hizi za giza . Yesu alisema jehanamu haikuumbwa kwa ajili ya mwanadamu ila ni kwa ajili ya shetani na malaika zake. Unaelezewa kama Jehanamu ya moto wa milele, ziwa la moto Giza, utengano, kilio na kusaga meno. Wakati hatuwezi kusema ni vipi tunafikiri kuhusu mtazamo wa kuzimu, tunaweza kutazama katika tafsiri hii, Kuzimu na utengano wa milele na Mungu na uzuri wote wa Mungu. Mkristo hatakiwi kuwa na mvuto wa kuzima, zaidi sana uepuke kuwa huko. Tunatakiwa kukumbuka kuwa Yesu hakuja katika ulimwengu huu kutuogopesh a kuhusu kuzimu bali kutukomboa kwa ajili ya kwenda Mbinguni. Pia wewe!

“Kisha atawaambia na wale waliopo mkono wake wa kushoto, ondokeni kwangu, mliolaaniwa mwende katika moto wa milele aliowekewa tayari Ibilishi na malaika zake.”
(Mathayo 25:41, SUV)