Je nitawaona jamaa yangu?

Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Kifo si mwisho wa yote.
“Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa ,cheupe na yeye aketiye juu yake , ambaye Nchi na Mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana, Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi. Na vitabu vikafunguliwa , na kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha Uzima, na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu sawasawa na matendo yao" (Rev. 20:11-12, SUV)

Itakuwa furaha kuu kuwaona huko Mbinguni. Nadhani ni ushauri mzuri kuamini wengine na kuwa na shaka kujihusu mwenyewe. Waache jamaa zako waliokufa katika wangalizi wa Mungu na uombe kwa ajili yao mara moja au mbili. Wewe mwenyewe uamini katika mshindi wa kifo. Unaweza kujifariji mwenyewe kwamba kwa Mungu hakuna yeyote amekufa. Kwake kila mtu ni hai (mzima) kwa sababu yeye hafungwi katika sheria za ulimwengu huu.

“Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai, nilikuwa nimekufa tazama ni hai hata milele na ni nazo hizofunguo za kifo na kuzima”
(Ufunuo 1:17-18,SUV)

Mungu ninaweka wapendwa wangu waliokufa katika mikono yako salama.