Nini kinatokea kwetu wakati tutakufa?

Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Mwanadamu aliumbwa kwa kuishi milele, kuvunja mapenzi ya Mungu kifo kikaja, na hakika kinatuhumiza sisi sote. Hata hivyo kifo hikitashinda mapenzi ya Mungu mpaka mwisho.

Katika kifo, Muda wetu wa rehema unafika mwisho. Katika ulimwengu huu ulioumbwa tunaweza kuishi kwa zawadi ya Mungu. Ijapokuwa hatumjali Mungu kabisa. Nini kinatokea, hata hivyo, wakati tunapoteza pesa zetu, uzuri, nafasi zetu katika kazi, afya na maisha? Nini kinatokea tunapokutana na Mungu aliye uchi katika dhambi zetu? Yeye aliyetupa uzima na ambaye anatuuliza tumeutumiaje huo uzima? Hatutakuwa uchi katika kipindi hicho. Biblia inatufundisha kwamba katika imani tutavikwa mavazi meupe, nayo ni haki ya Kristo tuliopewa katika ubatizo nayo ni imani, ni yako.

Nini kuhusu baada ya kufa?
Waliokufa katika Roho watalala kabla ya ufufuo wa siku ya mwisho? Biblia inatupa wazo hili kwamba katika kifo mtu anakwenda katika ukweli mwingine, si muhimu kujua urefu wa kipindi hicho/ hiki, lakini haijulikani kipindi hiki cha kusubiri ni cha furaha au cha huzuni,wakati dhamira inapokuwa nzuri kila mmoja anajua nani anasubiri, ni vizuri kusubiri.

“Lakini ndugu , hatutaki msifue habari zao waliolala mauti , msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini maana ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye."
(1 Thesalonika 4:13-14, SUV)