Mbinguni ni wapi?

Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Biblia haijatupa kijiografia mahali mbinguni ilipo. Mbinguni ni pale ambapo Mungu anapokaa katika ukamilifu wake. Biblia inasema;
“Ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti amekaa katika Nuru isiyoweza kukaribiwa, wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona, Heshima na uwezo una yeye hata milele Amina” (1 Timotheo 6:16, SUV)
 Hivyo basi hatuwezi kumfikia Mungu au Mbingu kupitia nafsi yeyote katika mpango wa kuchunguza wala kupitia akili zetu.

Yeye mwenyewe ametoka katika sehemu aliyojificha na kujifunua kwetu, kila tunachohitaji kujua kuhusu mbinguni. Biblia kwa mfano katika kitabu cha Ufunuo kuna maelezo mbali mbali kuhusu picha za mbinguni. Hizi picha haziwezi kulinganishwa kutoka katika picha moja nzuri. Ni kwa jinsi gani chumba kama mji umejaa barabara za dhahabu unavyoonekana? Au ni vipi kuabudiwa pasipo mwisho kunavyoonekana? Vipi kuhusu bustani, ambazo uzuri wake ni mzuri haijawahi kuonekan. Hii ni nini kwamba Mungu mwenyewe atayafuta machozi yetu. Mwalimu moja wa zamani wa kanisa alisema hivi kuhusu mbinguni” furaha ya Mungu inaonekana; kwangu mimi hiyo ni tayari sababu tosha kutaka kuona yote hayo!”

“Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.”
(Ufunuo 21:3, SUV)

Ombi: Mungu anataka kwenda mbinguni nichukue mimi huko