Imani inafananaje katika maisha ya kila siku? Na vipi nitamfuata Yesu?

Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Mwamini ni mshirika wa kanisa, maisha ya wakristo yameunganishwa na wakristo wengine; kusikiliza neno la Mungu, kuomba, na kushiriki meza ya Bwana tena uunganishwa kwa kusudi maalumu. Yote hii inaimarisha, na kulinda imani. Roho Mtakatifu yupo kutuimarisha sisi. Amri za Mungu zinatuhusu sisi sote. Kama mkristo kamwe hatuwezi kuzidharau Amri za Mungu na mapenzi ya Mungu baba yetu wa mbinguni.

Kila mmoja wetu hapa ana wito wake, na Mungu anataka tuwe waaminifu katika kuhudumia watu wanao tuzunguka. Hata hivyo wakati tunapokumbana na mahitaji ya maisha haya, mara moja tunatambua kuwa mwisho wetu kama binadamu na kwamba nguvu zetu hazitoshi. Tunafikiri isivyotosha. Na hivyo tunajaribu kufanya kile kilicho kinyume na Amri za Mungu na dhambi.

Asili yetu ya ubinadamu, mwili wakati wote unatuingiza katika dhambi na kufanya yale yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu haijalishi wewe ni mkristo au lah! Hivyo tunahitaji mwendelezo wa msamaha wa Mungu, kuomba na Nguvu zitokazo kwa neno la Mungu.

Maisha katika imani hata hivyo si kukataa vitu na kujitahidi kuwa mzuri. Kama Mkristo tunaishi kama watoto wa Mungu ndani ya Uhuru na Usalama ndani ya Neema yake, ndani ya Kristo Yesu tunapewa imani, tumaini na upendo kama zawadi. Hii ndiyo maana mkristo anapenda kusogea karibu na Yesu.

"Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu."
(Yoh 15:9, SUV)

Bwana Mungu nisogeze karibu na Yesu katika njia zako, usinifanye nipoteze njia yangu.