Ninawezaje kwenda Mbingu? Je nawezaje kuokoka?

Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Siku moja tajiri mmoja alimuuliza Yesu nitawezaje kuurithi uzima wa milele. Huyo mtu aliishi maisha mazuri. Yesu alimwambia auze mali yake yote na kuwapa maskini hizo fedha kisha amfuate Yesu. Tajiri alihuzunika sanakwa sababu aliulizwa zaidi. Wanafunzi walichanganyikiwa na kuanza kumuuliza Yesu ”Mtu anawezaje kuokolewa?” Yesu aliwajibu, kwa wanadamu hilo haliwezekani bali kwa Mungu yote yanawezekana.

Ili ni jibu la Kikristo.

Tumefungwa na ubinafsi wetu wenyewe, tunajipenda wenyewe kuliko kuwapenda wenzetu. Nguvu zetu za kupata wokovu ni za kibinafsi pia. Je unalo tumaini lolote?

Jibu ambalo Ukristo unatupa ni to tofauti na dini zingine. Mtazamo wetu si juu ya yale mwanadamu atafanya. Yesu Kristo ndiye kiini cha kila kitu. Yesu alifanya kile ambacho sisi tusingeweza kufanya. Alichukua mashtaka yetu mbele za Mungu na kupatanisha dhambi zetu na maovu yetu msalabani.

Hii ndio maana kunayo msamaha kalimifu katika moyo wa Mungu. Umetangazwa kwetu katika Biblia. Inaitwa injili ”Habri njema”. Na tunaridhi hiyo kwa imani. Kwa imani katika Yesu Kristo tunaokolewa na kuweza kuingia mbinguni. Nilipobatizwa katika jina la Mungu Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu na ninatambua kwamba mimi ni mali ya Mungu. Siku ya hukumu sitajaribu kujibu juu ya mashtaka ya dhambi zangu kwa Yesu amelipa deni langu la dhambi zangu zote.

Tunaweza kuwa na hakika kuhusu kuingia mbinguni maana unaweza kuwa na uhakika juu kazi ya Yesu.

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani;ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu."
(Efeso 2:8-9, SUV)

Ombi: Yesu nizaidie nipate kukuamini.