Imani huanzaje?

Mwandishi: 
Ville Auvinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Imani iokoayo siyo kazi ya mwanadamu bali ni zawadi itokayo kwa Mungu. Mwanadamu hawezi kwa asili kuzalisha imani yeye mwenyewe au kuamua kuja katika imani. Kwa jumla inategmea Mungu. Msingi wa kwanza wa vyombo vya neema ni neno la Mungu. Katika ubatizo imani inazalishwa kupitia neno pamoja na maji. Katika chakula cha meza ya Bwana imani iliyounganika na mkate na mvinyo. Na katika ungamo la dhambi inaunganishwa na msamaha wa dhambi.

Roho mtakatifu anazungumza na mwanadamu kupitia neno la Mungu. Na kupitia neno hilo Roho mtakatifu anakuja ndani ya roho ya mwanadamu na kuzalisha imani. kuamsha na kuimarisha imani ni kazi muhimu za Roho Mtakatifu.

Kama unashangaa labda una imani au hauna ya kutosha unaweza kumuomba Mungu akuimarishie imani. Hili ni ombi ambalo Mungu analojibu kulingana na hitaji. Unaweza kuamini kwamba Mungu anakupa imani lija ya au unavyojihishi au unavyojizoesha.

Katika kanisa Roho anamtukuza Yesu Kristo kama Mwokozi na kuhakikisha kwamba neema inakutosheleza pia. Imani siyo kitu chetu tunachokisukuma au kujaribu ila ni kazi ya Mungu ndani ya mtu.

"Basi imani, Chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo."
(Rum 10:17, SUV)