Nitajuaje kama nimeokolewa?

Mwandishi: 
Ville Auvinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Uhakika wa wokovu hauwezi kutegemea kazi yeyote ya mwanadamu, hisia na, matendo yake kwa sababu siku zote siyo kamili ni mtu anayebadilika kila wakati. Usalama wetu unaweza kutegemea juu ya kazi ya Mungu na Ahadi zake.

Kwanza, Biblia inasema Mungu aliupenda ulimwengu na alifanya upatanisho na huo ulimwengu kwa kusulubishwa kwa Kristo. Kwa hiyo Yesu alikuja kwa ajili yako pia.

Pili, kama umebatizwa umeunganishwa na kazi ya kuokoa ya Kristo.Wewe wenyewe ni sehemu ya wokovu ambao ni mali ya ulimwengu wote.

Tatu, Biblia inafundisha kwamba atakaye amini na kubatizwa ataokoka.Sehemu kubwa ya imani si katika nguvu zake ila ni malengo yake, Kristo na Ahadi za Mungu kwa hakika, imani ni kugeuka kwa mtu dhaifu na kuomba msaada kutoka kwaYesu ambaye anasamehe dhambi.

Biblia inaahidi “Yeyote atakayeliitia jina la Bwana ataokoka”. Imani kama hii ni zawadi kutoka kwa Mungu pia; Si kazi ya mwanadamu mwenyewe. Hivyo basi kama umebatizwa na kurudi kwa Yesu na kuomba msamaha kwa dhambi zako na kuomba wokovu, upo katika njia ya mbinguni.

Ndani ya chakula cha Bwana na Ahadi za Mungu umeunganishwa kukupa nguvu na kuimarisha imani yako.

“Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu,nami hukaa ndani yake”.
(Yoh 6:54-56, SUV)