Je nina thamani yoyote?

Mwandishi: 
Liisa Rossi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Machoni pa watu, uwezo wetu unaonakana katika uwezo tulio nao, hali zetu, pesa, mwonekano na kadhalika. Unaweza kujisikia kuwa wewe si mwema sana– hasa wakati maisha yako hayatimizi matarajio yanayotoka nje.

Dhamani yako ya msingi haitegemei hata hivyo mambo yaliyotajwa hapo juu. Hakuna mtu awaye yote anayeweza kutoa dhamani yako. Ni Mungu pekee aliyekuumba anayeweza. Hakukumba bure tu au kwa bahati mbaya ila kwa kusidi na upendo. Biblia inasema kuwa Mungu alimuumba mwadamu kwa mfano wake, mwenye dhamani kubwa kuliko vyiumbe vyote duniani.

Ulichorwa na kuumbwa na Mungu kuwa mototo wake mpendwa. Wewe ni mtu wa ina yake na hakuna mtu yeyote atakayechukua nafasi yako hapa duniani. Wewe una maana kubwa kwake – sana hadi akamtoa mwana wake afe msalabani ili kwamba uondolewe kutoka dhambi zako. Huitaji kulipia dhamani yako. Wewe unadhamani isiyo na kipimo kwa sababu umeumbwa, kupendwa na kuokolewa na Mungu.

Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.Matendo yako ni ya ajabu,Na nafsi yangu yajua sana
(Zaburi 139:14)

Ee Mungu, nibariki ili niweze kujiona jinsi unavyo niona.