Je Mungu ananipenda?

Mwandishi: 
Liisa Rossi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Mungu anakupenda – wewe hasa. Unaweza kujiuliza jinsi utakavyokuwa na uhakika juu ya hilo. Jibu ni raisi: Mungu mwenyewe anatuambia katika Bilia. Hasemi kwamba anawapenda watu wazuri na wema ila anapenda kila mmoja na wewe ni miongoni mwao.

Lakini unawezaje kuona upendo wa Mungu? Haonyeshi upendo kwa maneno tu ila pia kwa matendo. Tunapotazama aliyotutendea Mungu, tunaona jinsi upendo wake ulivyo mkuu. Mwanzoni kabisa uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu ulikuwa mkamilifu. Hawakuwa na mashaka juu ya upendo wa Mungu. Ila anguko na mwadamu liliharibu kila kitu na kuharibu uhusiano wetu na Mungu. Hata hivyo haikubadilisha upendo wa Mungu.

Upendo wa Baba yetu wa mbinguni ni mkuu kwamba alirekebisha hali hiyo. Upendo wake ulionekana miaka 2000 iliyopita wakati mwanae alikufa msalabani. Yesu alikufa ili usitenganishwe na Mungu kwa sababu ya dhambi zako. Yesu alikufa ili upate kufika mbinguni kuishi milele ukizungukwa na upendo wa Mungu.

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele
(Yohana 3:16)

Mungu naomba nisikie upendo wako na kuuamini.