Injili ya Yohana sura ya 2 – Moto wa Mungu unaenezwa

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Arusi ya Kana 2:1-12

Hadithi ya muujiza wa kwanza ambao Yohana anazungumzia haupatikani katika injili nyingine tatu. Tukio hili lilipatikana katika mji wa Galilaya,sehemu ambayo haijulikani kwetu sisi.

Matukio haya yalitokea huko mashariki ya kati iliyojumuhisha pia chakula kigumu. Mvinyo uliwaishia, lakini Yesu aliwaambia wale vijana waliokuwa arusini wajaze mabalasi yenye ujazo wa lita mia sita maji mabalasi hayo hayakuwa na mvinyo. Yohana anasema kwamba wanafunzi waliona utukufu wa Yesu na walimwaamini Yeye.

Hadithi hii inatufundisha nini?

Katika agano la kale mvinyo ulikuwa na ishara yenye maana. Sehemu ya maajabu ya wokovu uliotolewa kwetu na Mungu unajumuhisha wingi wa sherehe (Mwanzo 49:8-12). Wakati Yesu anaokoa sherehe ya arusi Kana, Yohana aneleza kwa hakika hivi: Kuna mwokozi mkuu mwenye uwezo katikati ya watu wa Mungu.

Maana nyingine: hii mara kwa mara haijadiliwi: Ni mwonekano wa Yesu juu ya vijana maarusi na kusherehekea kwao juu ya arusi. Hata hivyo aliwaita watu wengine kuacha kila kitu nyuma na kumfuata yeye, hakuwa na maana kudharau familia, ilikuwa ni kinyume chake kabisa, kwa kawaida familia upokea Baraka yake.

Tunapaswa pia kujadili mafundisho ya Biblia kuhusu kunywa mvinyo. Ni wazi kabisa ulevi ni dhambi, lakini Biblia haijadili kabisa. Kabisa huu ni mtindo wa nidhamu na mzuri tena unaokubalika, lakini haupaswi kudaiwa kwa kila mmoja. Ni kama kingo mbili za geti “njia nyembamba sana” ambayo imewekwa katika huu mtindo” kila mmoja katika ndhamira yake apime kwa uzito ni nupande gani wa njia anatembea. Ni makosa na madhara makubwa kutend a juu ya dhamira ya mtu mwingine.

Jambo la kuongezea: Yohana na mafanano

Katika kipindi cha Injili ya Yohana ilikuwa ni vigumu kuweka pamoja imjii zingine tatu. Hii inatoka katika mfano wa hadithi ambayo Yesu anasafisha hekalu: Wainjilisti wote watatu wa kwanza wanasema kuhusu Yesu akitembea Glilaya, safari yake kuelekea Jerusalemu, na kifo chake na ufufuo wake. Katika maelezo yao, na hadithi ya Yesu kusafisha hekalu imewekwa katika siku ya mwisho ya maisha ya Yesu. Lakini yeye Yohana anatoa muda tofauti. Yesu alifika Yerusalemu mara nyingi, na pia kipindi cha pasaka, hivyo alifanya huduma yake wazi miaka mingi. Usafishaji wa hekalu uliwekwa Yohana mapema kipindi cha huduma ya maisha ya Yesu.

Inawezekana kwamba Yesu alifundisha kikundi kidogo cha wanafunzi wake kwa muda mrefu kuliko watu wengine wote baada ya wao kuondoka. Yeye Yohana alikuwa na kusudi kuweka tukio hilo katika hatua za mwanzo kabisa katika huduma za Bwana Yesu. Kwa sababuhiyo hakuna hata mmoja anweza kukosa kusema kuwa Yesu alikuwa kiongozi wa kisiasa.

Hata hivyo, wainjilisti wote wane wameelezea juu ya kusafishwa kwa hekalu, vizuri kama walivyoelezea juu ya mateso yake na kufufuka kwake. Injili si historia ya maisha iliyoandikwa kwa mpangilio na utaratibu wa maisha ijapokuwa zimehifadhi taarifa kamili na sahihi ya historia. Kusudi la Injili ni kutufanya sisis kuamini katka Kristo. Ushuhuda wa Wainjilisti wane, achilia mbali mawazo yao, ni ya utajiri na mengi ya maelezo mazuri kuliko yangeandikwa na mwaandishi mmoja.

Yesu anasafisha hekalu 2:13-25

Nyakati zile za mwanzo sawa na sasa hivi, kusanyiko la watu walikusanyika ndani ya hekalu kwa shughuli za kibiashara. Ombaomba walikuwa na sehemu yao, na Wayahudi walikuwa na sehemu ndogo sana hekaluni ambayo waliweza kutoa adhabihu yao kwa Mungu. Wale waliokuja na shida ya kutoa dhabihu walitakiwa kujigharamia gharama za malazi na chakula na wanyama kwa ajili ya dhabihu . Wakusanya mapato wa hekalu waliweza kukusanya mapato kwa thamani ya pesa ya kiyahudi, hata hivyo mabadiliko ya lazima yalihiitajika. Makaburi ya makuhani wakuu yalionyesha maisha ya kitajiri ya makuhani waliotumika kutoa huduma. Si jambo la kushangaza kabisa kuona kwamba umuhimu wa hekalu umesaulika.

Utakatifu wa hekalu ulikuwa ni maigizo tu, na matukio yamefafanuliwa na Yohana kwa mfanano kiasi ulivyojipanga. Yesu aliwafukuza wafanya biashara wote ndani ya hekalu. Walifanya sehemu takatifu kuwa sehemu ya wanyanganyi. Wayahudi walilijua vizuri Agano la kale na waliyajua vema maneno ya nabii Malaki:

“Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema BWANA wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea BWANA dhabihu katika haki. Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za BWANA, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani."
(Malaki 3:1-4, SUV)

Kitu kingine cha muhimu maandiko ya kale yanatupatia kinapatikana katika Zaburi ya 69:9 (“Maana wivu wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.”).

Majibu ya Yesu kwa Wayahudi yalikuwa kama upuuzi tu, kila aliyesikiliza alifikiri kuwa Yesu anazungumzia juu ya hekalu la kawaida, lakini yeye Yesu alikuwa akizungumzia juu ya mwili wake mwenyewe. Kwa ajili hiyo kifo cha Yesu na ufufuo wake utaleta mtazamo uliopo katika Injili. Tunachukulia ulinganifu na Marko Masihi kama ni fumbo. Kristo alielezea ukuu wake waziwazi lakini watu hawakuelewa maneno yake.

Katika mistari ya mwisho ya kitabu cha yohana, tunahesabu tena maswali ya umuhimu wa miujiza, Yesu alifanya miujiza iliyopelekea watu wamwamini. Kwa jinsi hii miujiza ndani ya injili ya Yohana ina umuhimu wa kutunzwa. Kwa wakati mmoja, mwinjilisti anaongoza utafiti wa Yesu ambao unaiweka imani ya mwanadamu katika nafasi maalumu, Yesu akuwekeza kwa mwanadamu kwa sababu alifahamu imani ya binadamu kuwa legevu.