Injili ya Yohana sura ya 11 – Ni nani aliyekufa na nani aliye hai?

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Emmanuel Samwel Sitta

Katika sura ya sita, Yesu aliweza kuwalisha maelfu ya watu na kisha akaanza kuzungumza juu ya mkate wa uzima. Pia katika sura ya tisa, alimponya mtu kipofu na kisha akazungumza juu ya upofu wa kiroho. Katika sehemu ambayo sasa tunazungumzia, anamfufua Lazaro kutoka kwa wafu. Hata hivyo, sehemu hii inajadili mambo zaidi ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu. Tunakabiliwa na maswali kama haya: maisha ni nini? na kifo ni nini?, na ni nani aliyekufa na nani atakayeishi?

Kutoshuka kwa makusudi 11: 1-10

Wakati Yesu yupo ng'ambo ya Yordani, alipokea neno la kusikitisha kwamba Lazaro ni mgonjwa sana tena hawezi. Hata hivyo Mwokozi hakuweza kuacha kwenda lakini alichelewa kuondoka kwa kusudi. Hata hivyo hii sio hatua itakayofunua yote yaliyo kwenye moyo wa sura nzima: sio tu juu ya kuwafufua wafu ambao sasa tunazungumzia. Lengo la matukio haya ni kufunua utukufu wa Mwana wa Mungu, kwa maneno mengine, kuonyesha utambulisho halisi wa Yesu. Kwa sababu hiyo kwamba waombolezaji watalazimika kumsubiria Yesu afike tayari wakati huo Lazaro amekwisha kufa.

Wanafunzi wanashangaa kwamba Yesu ataondoka katika eneo la Yerusalemu. Baada ya yote kutendeka huko, alikuwa amekwishakuwa katika hatari ya kifo. Yesu anatoa sababu sawa za matendo yake kama alipomponya kipofu (9: 4-5): kuna wakati mdogo tu wa kufanya kazi. Usiku utakapokuja, haiwezekani kufanya vizuri. Hii inatumika hasa kwa Yesu - kwani alikuwa na kazi yake, na ilidumu kwa muda mdogo. Wakati huo, alipaswa kufanya kazi na siyo kuepuka hatari.

"Lazaro amekufa" 11: 11-16

Lazaro alikufa katika mji wa Bethania. Kwa Yesu, tukio hili lilikuwa ishara njema ya kuanzia. Mara mbili wanafunzi hawaelewi maneno yake, ambayo ni sifa ya injili ya Yohana; kwanza anataka kuwa Muuguzi mzuri, na kisha Thomaso anataka kuonyesha ujasiri wa shahidi. Katika matukio hayo yote, wanafunzi walimaanisha mema. Mipango ya Mungu mkuu ilionekana kuwa ya ajabu sana kwao.

Martha kukiri kwa imani 11: 17-27

Nyumba ya Lazaro aliyekufa ilikuwa imejaa waombolezaji waliofika kumfariji dada yake. Yohana wa kwanza anatuambia jinsi gani Yesu alivyozungumza na Martha.

Kwa sasa tumegundua kuwa neno 'kuamini' lina maana ya aina nyingi katika Injili ya nne. Wakati mwingine inasemekana kwamba watu fulani 'wanaamini' katika Yesu na, wakati huo huo, wanajiuliza na kushangaa kwamba wakati Kristo atakapokuja, atafanya miujiza mingi zaidi kuliko Yesu.

Katika hali nyingi, watu wengi wanaongea na Yesu bila kujua nini kinaendelea. Hii ilionekana mwisho pale wanafunzi walipokuwa wakiongea na kushindwa kuelewa mambo fulani. Lakini sasa hali ni tofauti; Kukiri kwa Martha kwa imani kulikuwa ni jambo kamilifu na zuri. Anaonyesha kwanza imani yake pale aliposema kwamba Yesu anaweza kufanya miujiza. Angeweza kumponya Lazaro mgonjwa na, hata sasa, anaweza kumfufua mtu aliyekufa. Taarifa yake baada ya hii inaonyesha imani yake inayoaminika katika ufufuo wa siku ya mwisho. Swali la muhimu hapa linalokuja mwishoni: je ni uzima na ufufuo unaohusishwa na utu wa Yesu, hivyo kwamba kile ambacho hakika sio mapigo ya moyo wetu au jinsi ya kupumua, lakini ni juu ya uhusiano wetu na Yesu?

Martha ni mmoja wa wale walio vipofu wa kiroho ambao Mungu amewaondolea na . Anaweza kuona wazi utukufu wa Kristo,

”Naam, Bwana; Ninaamini kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye anakuja ulimwenguni.”

Hivyo masuala ya kuishi na kifo yanafanywa wazi na mazungumzo kati ya Martha na Yesu. Hakukuwa na hasara kwamba Lazaro amekufa kaburini. Hakuna chochote kibaya kilichotokea kwake. Ni wakati Kristo alipokataliwa na kufanyika huzuni.

Nguvu ya kifo imeangushwa chini 11: 28-44

Yohana anasimulia hadithi ya ufufuo kwa njia yake mwenyewe, ya ajabu. Tunakabiliwa na nguvu za kifo katika hofu zake zote kwenye kaburi la Lazaro. Wakati huo huo, tofauti kubwa kati ya wanadamu na Mungu inakuwa dhahiri. Watu wanaweza tu kuona kifo cha duniani na huzuni husababishwa na kuomboleza. Wakati Yesu anatokwa na machozi kaburini, watu walifikiri kwamba alilia kilio cha kuomboleza kifo cha Lazaro. Katika ukweli, Yesu alilia kwa nguvu ya kifo na giza katika mioyo ya watu na kwa kutokuamini kwa watu waliokuwa wamekusanyika kuomboleza kifo cha Lazaro. Yeye mwenyewe hakuwa na haja ya kushuhudia muujiza wa ufufuo. Muujiza ule ulikuwa muhimu kwa watu waliozunguka ambao, kinyume na kile wanachoweza kufikiria, hawajui chochote kuhusu maisha na kifo.

Wakati mtu aliyekufa atatoka katika kaburi lake, kila mtu alikuwa na nafasi ya kuelewa kweli iliyofunuliwa na Mungu: Nguvu ya kifo imevunjika mbele ya Kristo, kwa sababu alikuwa ametumwa na Mungu kuleta uzima kwa ulimwengu.

Kwamba Yesu alilia kwa kuhamasisha sana ni maelezo yaliyo muhimu. Hata wakati wa injili ya Yohana ilikuwa imeandikwa, watu wengi waliona kuwa hasira kwamba Yesu alisulubiwa - kwamba atapaswa kuteseka na kufa kama mwanadamu. Walijaribu kuelezea mbali mambo haya yenye kukera kwa kumfanya Yesu awe mtu wa kiroho ambaye hakuweza kuumia maumivu, asiache tu kufa.

Hakuna ishara ya tabia ya namna hii katika injili ya Yohana au katika Injili pacha (Synoptics). Katika maandiko haya, Yesu ni wazimu na mwenye shida, mtu wa huzuni na mwenye ujuzi. Kipengele kizuri katika picha hii ni maelezo ya Yohana ya Yesu akiomboleza, kama alivyoona nguvu ya kifo juu ya watu wasioelewa.

Mpango wa kumwua Yesu 11: 45-57

Muujiza mkubwa wa Yesu wa kumfufua mtu aliyekufa, haukusababisha mshangao wala haukusababisha mageuzi ya imani. bali muujiza huu ulihamasisha kundi la wanaume wenye nguvu. Baraza, na mamlaka iliyokuu zaidi ya maamuzi ya Wayahudi, iliandaliwa. Yesu lazima asimamishwe, kwa gharama yeyote.

Katika giza hili lote, Roho wa Mungu alikuwa akifanya kazi. alifichwa katika giza na maneno yasiyo ya Kimungu na yasiyo ya mpango wa Mungu, na uasi wa Kayafa sio kikwazo kwa Mungu kumtumia kama sauti yake; ni bora kwamba mtu mmoja apate kufa ili mwingine asiangamie. Na kifo hiki hakitagusa Waisraeli tu bali kitagusa watu wa ulimwengu wote.

Uamuzi huo umefanywa sasa, na kila kitu kitakuwa tayari kwa hitimisho kubwa. Mpango huo umekwisha kamilika. Sura inayofuata ni kuhusu Pasaka ya Kristo.