Agano la Kale

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Soma Agano la Kale kwenye mtandao:
Agano la Kale (bibles.org)


Njia mbili za kusoma Agano la Kale

Kusudi la kuandika kifungu hiki kifupi nikusaidia msomaji kuelewa kwamba kuna njia mbili za kusoma Bibilia, na ni vipi njia hizi mbili zinaweza kudhihirishwa na kutusaidia kufahamu kitabu kitakatifu vizuri zaidi.

NJIA YA KWANZA: ni vipi wasikizaji wa kwanza walifahamu maandiko?

Kitu kizuri wanachuo kikuu wanaweza kufafanua, kutoa mfafanuzi ni maswali marahisi. Ni kwa namna gani watu wa kwanza walisikia na kusoma na kuelewa? Swali litatuongoza kwa usahihi kujifunza lugha, historia na tamaduni, hivyo msomaji wa Bibilia jaribu kusafiri ndani ya muda wa miaka ya Isaya, Ezekieli na Zakaria na simama upande kwa upande pamoja na wasikilizaji wa kwanza na maneno yao na usikilize kwa makini hii ndio kazi ya kihistoria mafafanuzi kazi hii inachangamoto tunafikira kuhusu mtu anayekuja kutoka moja kwa moja na kutoka aina tofauti ya tamaduni aliye katikati yetu na anayejua lugha yetu. Anafahamu kidogo matamshi yetu na desturi zetu zinaonekana ngeni na zisizoeleweka kuja kwa urahisi sana na wasomaji wa Agano la kale walikutana nazo na kutokueleweka kwa kiasi kikubwa sana pamoja na maana hii ingawaje mtazamo huu una mengi ya kutoa.

Njia hii ya kusoma inatusaidia sisi kufahamu vipi Isaya alitendakazi yake katikati ya vikwazo vingi, Ezekieli alikaa mbali huko Mesopotania akiona hatua za mwisho za mji wake mpendwa ukiangamizwa, na vipi Zakaria alivyotembea pamoja na Hagai ndani ya Yerusalemu ilivyoharibiwa wakati wakazi wa Judea walipokuwa wamerudi wakati huohuo, kumtafuta mmoja baada ya mwingine twavutiwa zaidi na zaidi na ndani tunapata historia ya neno la Mungu.

NJIA YA PILI: wakristo wa kwanza walisomaje bibilia?

Nija ya pili ya kusoma imekuwa ikihusishwa na ushahidi wa kipekee ndani ya kanisa la kristo tokea mwanzo.

Agano la kale lilisomwa kupitia Kristo. Kutokana na kuamini kwetu amemkaribia mwanadamu mwenye dhambi. Kwa mfano katika waraka wa Efeso unaelezea kwa nguvu ni vipi Mungu alivyokuwa ameandaa kazi yake ya wokovu kabla ya misingi ya ulimwengu, aliandaa kipindi cha Agano la kale na anatimiliza katika upatanisho wa Yesu na, kwa mtazamo huu aagano la kale na jipya liko pamoja na linatengeneza barua ya upendo kwa mwanadamu.

Tunapata msingi wa njia hii pekee wa kusoma katika ukurasa wa mwisho wa injili ya Luka mtakatifu ambayo Kristo amefufuka, anayadhihirisha maandiko kwa wanafunzi wake wawili fundisho linaanzia kutoka Musa- na kama Paulo alivyoliweka- Ondoa magamba aliyafungua macho ya wanafunzi. Mfano ifuatayo itaelekeza njia mbili za kusoma Bibilia zinaweza kusaidia kila mtu.

YEREMIA NA AGANO JIPYA

Nabii Yeremia hakupokea kazi rahisi, alikuwa kijana wakati Bwana alipomtuma kutabiri kwa watu wake. Wakati mwingine ilikuwa sahihi kwake kwamba watu walikuwa hawako makini kwa maneno yake. Alikwenda kwa matajiri na maskini, lakini neno lilikataliwa. Sura ya tano: aliketi juu ya bidhaa zake, alitukanwa na kila mmoja na kulaani wito wake, Sura 20” Aliandika utabiri wake na kuutuma kwa mfalme- waliusoma kwa mfalme, badaye aliuchoma mbele za watu. Sura 36” Haikuwa hivyo mpaka Yerusalemu ilipozingirwa kwa vita na kulazwa chini, baada ya taabu na shida na uvamizi na kushindwa ndipo maneno ya Yeremia yalichukuliwa kuwa uzito mkubwa. Hata hivyo baada ya hayo watu maskini walitendwa vibaya ndani ya kitambo kidogo baada ya matatizo.

Kusoma kwa njia ya kihistoria inatoa mengi kwa msomaji wa kitabu cha Yeremia. Wasikilizaji wa kwanza wa Yeremia waliona na kusikia kila kitu,lakini hawakupokea neno. Yeremia ni mmoja wa wengi katika mifano ya imani. Kazi ya ufalme wa Mungu inafanywa kwa uaminifu ijapokuwa tunalipa gharama kwa huo. Yeremia ni mmoja wa mgeni aliyechaguliwa, kama waraka wa kwanza kwa Petro unavyoelekeza wakristo kuwa:- tunapendwa na Kristo lakini ulimwengu unatuchukia.

Soma kupitia Kristo, kitabu cha Yeremia kitakupa utajiri wa ulimwengu kwa wingi. Yeremia ni kwa hakika ni mmoja wa watumwa, ambaye mmiliki wa mizabibu (Mungu) alimtuma kabla ya mwanae Yesu (Marko 12) hata hivyo kwa nyongeza alitabiri kitu kipya kabisa katikati ya uangamizi.

”Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema BWANA.
 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.
 BWANA asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku, aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; BWANA wa majeshi, ndilo jina lake; Amri hizi zikiondoka, zisiwe mbele zangu, asema BWANA, ndipo wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele zangu milele. BWANA asema hivi, Kama mbingu zikiweza kupimwa, na misingi ya dunia ikiweza kugunduliwa huko chini, ndipo wazao wa Israeli pia nitawatupilia mbali, kwa ajili ya hayo yote waliyoyatenda, asema BWANA.."
(Yeremia 31:31-37 SUV)

Maneno katika kitabu cha Yeremia yanaelekeza kwa agano jipya, kwa damu ya Yesu Kristo ushirika mtakatifu. Agano jipya ni agano la neema na msamaha.

EZEKIELI NA YERUSALEMU MPYA

Wakati ambao Yeremia anapita katika vita vyake juu ya Yerusalemu nabii mwingine alikuwa anafuata kwa hali kama hiyo kutoka mbali. Mfalme wa Babloni alileta nguvu yake kwa Yerusalemu mwaka 597 na alimwakilisha mfalme kuwa katika pande salama alikuwa mashuhuri, wenye nguvu na makuhani walichukuliwa mateka ndani ya nchi yao wenyewe. Kati yao walilazimishwa kuwa utumwani, alikuwa ni kuhani aliyeitwa Ezekieli. Tangu mwaka 593 alianza kuwa na maono. Mara ya kwanza alionya na kuonyesha ni vipi Yerusalemu itakavyoharibiwa. Matumaini ya maono yao yote yameelezwa sura ya 8-11: Utukufu wa Bwana umeondoka Yerusalemu na mji hivyo umebaki pasipo ulinzi, tayari kwa uharibifu na Yerusalemu hakika uliharibiwa mwaka 587/586 BC.

Baada ya uharibifu wa mji, kitabu cha Ezekieli kinatoa kabisa aina tofauti ya vifungu. Hapa ni upande wa kitabiri kuhusu ni vipi Bwana atakuja kuwa mchungaji wa watu wake (sura 34) na vipi atawaleta watu wake katika uzima ingawaje wako kama mifupa ya wafu iliyokauka (sura37).

Kutoka katika mtazamo wa kihistoria, kitabu cha Ezekieli ni kitabu kinachotisha kukisoma, kinatueleza hadithi kuhusu chukizo la Mungu na Upendo wake. Soma kupitia Kristo, kitabu cha Ezekeil kitafungua moja kwa moja kwa wingi njia mpya. Tumechukua tu kifungu cha sura ya 40-48, ambacho ni kinyume cha maono kwa maono yasiyo na faida. Ndani ya sura ya 8-11. Utukufu wa Bwana ulirudi Yerusalemu na nabii alipata kutembea juu ya mitaa ya mji. Hivyo mji ni tayari na unatusubiri, Bwana mara moja anazungumza na watu wake pale, sawasawa na kitabu cha ufunuo, bibi arusi wa kondoo amechukuliwa. Hazina ya kitabu cha ufunuo kimechanua kipitia kitabu cha Ezekieli.

MITAZAMO MIWILI

Mifano iliyotajwa juu ina kusudi la kutuonyesha ni vipi inavyowezekana kwa msomaji wa kawaida wa Bibilia kuchukua katika maanani mitazamo yote miwili. Mafafanuzi katika mtazamo wa kchuo kikuu katika agano la kale kutoka mtazamo wa kihistoria, kama vile kanisa lilivyoona kama sehemu ya mafungu ya Mungu. Mitazamo yote miwili ina zawadi nyingi, kwa usahihii wakati zinatumika pamoja. Bibilia inajumuhisha mengi zaidi ya tunavyoelewa, na inatukaribisha kujifunza barua za upendo mkubwa wa Mungu.