Agano Jipya

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Soma Agano Jipya kwenye mtandao:
Neno: Bibilia Takatifu (SNT), Agano Jipya (biblegateway.com)
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote, Agano Jipya (bibles.org)
Biblia Swahili Union Version, Agano Jipya (bibles.org)


Maoni juu ya Injili ya Yohana
Maoni juu ya Barua ya kwanza kwa Wakorintho


Ni kwa jinsi gani Agano Jipya lilitokea

Kitabu cha Agano Jipya ni cha muhimu kwa wakristo. Hakika si tu kitabu kimoja ila ni mkusanyiko wa vitabu vingi vilivyoandikwa na waandishi tofauti.

Utajiri huu wa mkusanyiko wa maandiko unatuambia juu ya matendo na mafundish ya Yesu na mitume wake. Kuna pia maandiko kuhusu Yesu, kwamba yameandika na wapinzani na wasio wanahistoria wa ukristo. Hii ndiyo maana hakuna mtaalamu anaweza kukataa historia muhimu ya matukio ya maisha ya Yesu.

Agano Jipya ni kwa ajili yetu na chanzo cha utoshelevu wa kumjua mwokozi wetu.

Chukua ukaribu wa kuangalia Agano Jipya, mara moja unaweza kuona kuwa limejumuhishwa aina tofauti ya vitabu. Kwanza kuna injili nne (Mathayo, Marko, Luka, na Yohana.), halafu Matendo ya Mitume, na mkusanyiko mkubwa wa nyaraka, na mwisho kitabu cha Ufunuo wa Yohana. Lakini ni jinsi gani hivi vitabu vilitokea na jinsi gani vilikusanywa na kujulikana kama Agano Jipya na kumaliziwa katika jalada moja?

Injili

Yesu mwenyewe hakuandika kitabu chochote, lakini kuhusu yeye vimeandikwa vitabu vingi visivyohesabika, vilivyo muhimu kati yake ni Injili. Injili hazina ujazo wa wasifu wa Yesu. Tunatakiwa kusoma ikiwa tunataka kujua kwa mfano , maisha ya ujana wa Yesu, Lakini Injili haituambii chochote kuhusu hilo. Katika ukweli inaelezea tu kwa uchache matukio ya utoto wake ikifuatiwa kuzaliwa kwake. Injili ina kusudi rahisi lililotajwa na Yohana kama mfuasi wake:

“Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu: na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.”
(Yohana 20:30-31, SUV)

Injili zote zinaeleza tu sehemu ndogo ya matendo na mafundisho ya Yesu. Kiukweli, kuelezea wiki moja inahitaji nafasi zaidi ya ilivyotumika. Yohana alijua vizuri kwamba mengi yameachwa ambayo hayajasemwa.

“Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu: ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa."
(Yohana 21:25, SUV)

Kutokea kwa Injili tunaweza kutofautisha kutokana na vifungu vifuatavyo:

  1. HISTORIA YA MATENDO YA YESU.
    Yesu alifundisha watu kwa miaka mitatu. Alifanya mvuto kwa watu wasiohesabika, kwa wale waliokuja kusikia mafundisho yake maelfu kwa maelfu. Katika kipindi cha Wapalestina walikuwa na historia juu ya Yesu Kristo Kama nilivyokwisha kusema kuwa, wale wote waliosikia mafundisho yake walisika mengi zaidi ya tunavyosoma katika Agano Jipya sasa. Hii ina maana kwa wanafunzi wake tu zaidi wale mitume kumi na wawili.

  2. UTAMADUNI WA KUSIMULIWA.
    Baada ya kifo cha Bwana Yesu na ufufuko wake. Kizazi kilichokuja kilisimuliwa habari zake. Katika kanisa la kwanza la Jerusalemu mitume walijua kile kilichotokea. Masimulizi yao kuhusu kuhubiri injili kulisababisha kuzaliwa kwa kanisa. Katika Injili kiini chake kilikuwa ni kuzaliwa kwa Kristo, kifo, na kufufuka kwake.

  3. UTAMADUNI WA MAANDISHI
    Idadi ya watu wote, ambao walimsikia Yesu mwenyewe akisema walianza kupunguza, na kwa sababu hiyo maneno ya yesu yalianza kunakiliwa. Hatuwezi kujua ni namna gani ya kunakili maneno ya Yesu yalikuwepo kabla ya kuandika Injili. Hata hivyo, moja ya nakili hiyo imekuwa ikiitwa “chanzo cha LOGIA” ambayo imekuwa ikitumiwa na mwinjilisti Mathayo na Luka.

  4. INJILI TIMILIFU
    Waandishi wengi wa Injili walikuwa na vyanzo vingi tofauti kwa jinsi walivyokuwa wanaandika kuhusu Yesu. Mwaandishi wa Injili ya zamani Marko, alikusanya mengi kutoka utamaduni wa masimulizi, Dhahiri kabisa ukilinganisha na mafundisho Ya mtume Petro ikiwa kama yote aliambiwa kupitia mtume Petro. Mathayo na Luka wao tayari walijua Injili ya Mrko na waliongezea katika vyanzo vyao wenyewe. Mwandishi kijana mdogo wa Injili, Yohana, kiikweli alijua kazi za watangulizi wake, lakini aliandika Injili yake katika mtazamo wake. Hivyo Injili zote nne zimeunganisha utajiri mkubwa wa sura ya maisha ya Yesuwa Nazareti mafundisho yake na umuhimu wa sadaka yake ya kafara kwa dhambi zetu.

Injili zote nne inawezekana ziliandikwa kati ya miaka ya 60 - 90/100 AD. Kwa mfano miaka ya 40 - 60/ 70 baada ya kifo na ufufuko wa Bwana Yesu. Ebu tujaribu kufikiri jaribio hili: Unaweza kumpata mtu anayeweza kukuelezea tukio lililotokea miaka 40 iliyopita? Hakika hata kipindi cha miaka 70 inawezakuwa ngumu kuweka kumbukumbu ya yaliyotokea. Injili zilizoandikwa mapema zilikaribia na kipindi cha Yesu ambazo zimefanya masimulizi yao yawe yanakaribiana.

Pia injili zingne ambazo si mali ya agano jipya zimekua zimeifadhiwa. Ziliitwa Apokrifa zilizotokea nje ya kanisa na kwa usahihi baadaye kwamba injili nne (4) zillikubaliwa kuwa injili. Zilikua na vyanzo vibovu. Zilitupiliwa nje kutoka katika Agano jipya kwa sababu nzuri.

Matendo ya Mitume

Luka aliandika kitabu cha pili katika mwendelezo wa injili yake akieleza ni vipi injili ilikuja Rumi. Hiki ni kitabu cha kipekee katika Agano jipya. Hata hivyo nje ya Biblia tuna idadi ya namba kubwa ya hadithi kuhusu mitume tofauti, kwa mfano matendo ya Petero na matendo ya Paulo. Kwa usahihi ziliandikwa baadaye kuliko vitabu vingine vya Agano Jipya na mara kwa mara zimejumlisha hadithi za kufikiria.

Nyaraka (Barua)

Zaidi ya vitabu vya Agano jipya ni Nyaraka (barua). Zaidi ya kundi tangulizi lilianzishwa na waraka wa Paulo. Katika kiini cha hizi barua ni msamaha wa dhambi - zawadi ywa Mungu aliyoitoa kwa kwa wote Wayahudi na watu wengine wote kwa kifo na ufufuko wa Kristo. Katika nyongeza kwa haya Agano jipya inajumuisha barua (nyaraka) kutoka mitume wengine (Yakobo, Yohana, Petro) na pia barua kwa Waebrania iliyoandikwa na mtheologia mkubwa ambaye hajatajwa ni nani.

Nyaraka (barua) hizi ziliandikwa kwa uhitaji wa kweli. Katika msaada wao mbalimbali wa waasi walioliingilia kanisa na kuliharibu na kwa ajili ya kuanzisha sharika mpya zilizofundisha njia nzuri ya Mkristo ya kuishi.

Nyaraka hizi bado zinafanana na Wakristo na zilirekodi mafundisho ya kitume kuhusu Yesu. Watafiti wa mswali kuhusu waandishi wa nyaraka nyingi, wanauliza kama waandishi wake ni mmoja aliyeripoti. Vizuri kama jambo la ukweli swali hili si la muhimu.

Kitabu cha Ufunuo

Kitabu cha mwisho katika Biblia ni kitabu cha ufunuo, ni kitabu cha kipekee katika agano jipya. Kimezama sana katika maono ya nabii Yohana. Kupitia wao Mungu analifariji kanisa lake juu ya mateso. Hiki ni kitabu kilichojaa mambo na mifano. Ni vigumu kukielewa pasipo sauti ya uelewa kutoka agano la kale na agano jipya. Hii ndio maana kitabu hiki kikubwa mara nyingi kimetumiwa vibaya au isivyo sahihi kwa kusudi la kutia hofu. Kiukweli ni kitabu cha neema na faraja.

NI JINSI GANI AGANO JIPYA LILITOKEA?

Kama nilivyotaja, katika kanisa la kwanza kulikuwa na maandishi mengi ya utajiri na mwendelezo wake katika karne ya pili ya tatu wakati wanatheologia kama vile Askofu Clement wa Rumi, Askofu Ignasias wa Antokia, na Justin Maritaya walikwenda mbali sana. Hata hivyo, maandiko yao hayakujumuhishwa katika kitabu cha Agano Jipya wala kuwekwa katika Injili za Apokrifa ya Matendo ya mitume. Lakini ni nini kilijumuhishwa na nini kiliachwa?

Wakati huo wengi sehemu nyingi (mara kwa mara mfano kwa upande wa kiislam), walijaribu kuliweka wazi kanisa mpema kabisa katika karne ya nne walijumuhisha au walitoa kile ambacho hakikuitajika, ni bayana kwamba ujumbe wa asili kuhusu Yesu Kristo waliweka mambo yao. Katika sehemu mbalimbali kuna mawazo yamejumuhishwa na wale wanaozingatia kanuni kuliko Biblia.

Katika ukweli, maamuzi ya mikutano ya kanisa uliendelea kwa muda mrefu katika kanisa mahali ambapo neno lilisomwa katika huduma ya kanisa.

Mkusanyiko wa barua za mtume Paulo zilishakuwepo kabla ya miaka 100, na Injili nne zilikuwa zimeunganishwa katika nafasi zao katika karne ya pili. Vitabu vingine vya Agano jipya viligundua vitabu vyao katika majmbo yao tofuati mahali penye ukristo kwa wakati mmoja. Katika karne ya tatu na ya nne kulikuwa na majadiliano makini kuhusu mkusanyiko wa vitabu vitakataifu, lakini ililenga sana vitabu vichache (hasa waraka kwa waebrania, na Ufunuo wa Yohana).

Mkusanyiko wa kanisa (Hipo katika upande wa magharibi 393,walijiunga na utamaduni i wa usomaji maandiko na Leodikia katika upande wa mashariki kama mwaka wa 360) walijiunga na utamaduni wa usomaji mandishi matakatifu katika ibada uliokuwa umegundliwa miaka mia mbili uliopita, katika kujibu mambo kuhusu maandishi ya wazushi. Tunaamini kuwa Roho Mtakatifu aliliongoza kanisa lilipokuwa likachagua vitabu vya Agano Jipya.

Katika harakati iliyoungwa mkono kwa msimamo mkali wa kitamaduni vitabu vingi viliachwa nje katika Agano Jipya ambavyo vilijumuhisha vile vilikvyokuwa havina masomo muhimu na vilikuwa haviaminiki kuliko vya Agano Jipya. Hata hivyo maandishi haya hayalinganishwi na Biblia Takatifu.

MAANDIKO

Kwa bahati mbaya kwa wakati huu hatuna nakala halisi ya Injili iliyoandikwa na Mathayo. Lakini tunayo nakala na nakala za nakala hizi. Shida katika maandiko ya nakala ya Agano Jipya si ya kigeni, katika sayansi ya wakati huu. Maandiko yote ya zamani yako kwetu sisi kama nakala na hakuna maandiko yaliyo mengi kama yale ya Agano Jipya, na kulinganisha maandiko tofauti ni rahisi kupatamaelezo kwa mfano, yale Mathayo aliyoandika kwa wakati wake. Si kila wakati wa utatanishi maswali uibuka lakini katika shida haitumiki katika kanuni ya imani yetu.

Agano Jipya katika lugha yake halisi kiyunani imekusanywa kwa makini katika msingi wa maandiko tofauti na imejumuhisha Injili y a kimitume iliyoaminika.

TAFSIRI

Agano Jipya liliandikwa karne ya kale kwa kiyunani, ndiyo maana jukumu la mchungaji ni kulisoma andiko katika lugha halisi. Mchango muhimu wa matengenezo ulikuwa ni Biblia isomwa na kila mtu katika lugha yake. Biblia na sehemu zake imetafsiriwa katika lugha ngeni tofauti. Miaka inavyobadilika katika karne na miongo utafsiri mpya waitajika. Ulimwenguni kumejaa matafsiri tofauti, baadhi yanalenga ufasihi sahihi wakati mengine yanalenga mtiririko.
Tafsiri iliyotumika katka tafsiri hii ni ya Biblia Swahili.

KWA HIYO NI AGANO GANI JIPYA TULILONALO SASA?

Agano Jipya ni mkusanyiko wa vitabu vilivyoandikwa na wanadamu. Kila mmoja alikuwa na kumbukumbu ya neno la Yesu lililosemwa na mtu mwingine likaandikwa.

Mwingine ameandika Injili akitegemea maandishi na maneno yaliyosemwa na mtu mwingine. Haya yote yanaweza kufunzwa kitaalamu kama yalivyosemwa mwanzo, hakuna sababu ya kutia shaka utegemeaji wa Injili katika mtazamo wa kitaalamu. Lakini hii si yote. Agano Jipyasiyo tu mkusanyiko wa vitabu vilivyofanywa na wanadamu. Tunaamini Agano Jipya kama Biblia nzima, ina ufunuo wa Mungu kwetu sisi. Wakati tunaposoma Biblia, Mungu uongea nasi na kuahakikisha kila neno lake alilonena limenenwa kupitia kwa wanadamu.
Mtazamo huo hauwezi kufanyiwa utafiti wa kisayansi na yeyote.

Lakini ni nini kinachotofautisha huu mkusanyiko wa vitabu na nakala zingine za dini?

Kulingana na imani ya ukristo neno la Mungu hufanyaufanya kazi lenyewe katika mioyo ya watu, ndiposa binadamu uamini kuwa hilo ni neno la Mungu. Hakuna mwanadamu anawza kumshurutisha kwa njia nyingine yeyeote Katika Thesalonike Paulo alimuhubiri Kristo na wengi hawakukubali ujmbe wake. Lakini wachache walitambua mvuto wa Mungu katika ujumbe wa mtume.

“Kwa sababu hiyo sisi nasi tunamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa,mlipopata lile neno la ujumbe wa Mungu mlilosikia kwetu, mlilipokea si kwa neno la wanadamu, bali kwa neno la Mungu: na ndivyo lilivyo kweli kweli: litendalo kazi pia ndani yenuninyi mnao amini”.
(1Thesalonike 2:13, SUV)

Hata leo wale wanaosoma Biblia wana ufahamu kama wale ofisa waliotumwa kumshika Yesu lakini hawakutimiza jukumu walilopewa:

“Msidhani mimi nitawashitakikwa Baba; yupo anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi kwa nmaana kama mngalimwamini Musa; mngeniamini mimi,kwa sababu yeye aliandika habari zangu.”
(Yohana 7:45-46, SUV)

Kristo aliyefufuka anaishi na kutawala, na neno lake halitapita hata ingawa mbingu na nchi zitapita.