Injili ya Yohana sura ya 4

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Yesu na mla watu 4:1-42

Hadithi kuhusu mazungumzo kati ya Yesu na mwanamke msamaria ni ya kufurahisha na ya kupendeza. Mazungumzo yanalenga juu ya mwanamke kutoolewa. Yesu hata hivyo anakubali kuzungumza naye, na mwisho wa majadiliano si kuwa tu Yule mwanamke msamaria bali hata Wasamaria wanamjia. Hivyo, mwinjilisti anaruhusu kuwa watu duni na watu wasio na hekima kuwa lengo la Yesu katika hadithi hii.

Umuhimu wa habari hii kuwa inaandaliwa Samaria, Yesu anaaga Judea kuelekea Galilaya. Ikiwa mtu anataka kuvuka ukingo wa mto jordani ilimlazimu avukie kupitia Samaria. Hii ilikuwa pigo kwa Wayahudi kwa kuwa wao hawakuelewana na wasamaria.

Hawakujulikana walikotoka Wasamaria, iwapo maana asilia ni ya kweli - eti Wasamaria ni mchanganyiko wa watu waloishi Israeli baada ya kuvamiwa katika mwaka wa 722BC. Wasamaria walijiona kuwa Waisraeli halisi. Lakini Wayahudi waliwachukulia kama wakosa dini.

Kulikuwa na hekalu katika mlima Gerizim ambalo lilipingana na hekalu la Yerusalemu. Wayahudi walikuwa wameliharibu mwaka wa 128, lakini huo mlima ulibaki mahali maalumu pa maombi. Uhasama kati ya Wayahudi na Wasamaria uliibuka kila mara katika kipindi cha Yesu, na damu ilimwagika wakati wa waumini wa Kisamaria walipotofautiana. Wayahudi wa mafundisho sahihi waliwadharau Wasamaria na wakakataa kushirikiana nao. Sasa Yohana anatueleza kuwa Yesu alifanya kinyume lakini alikubaliwa pale.

Watu wengi ambao wameelezea kisa hiki, wameeleza ni jinsi gani huyu mwanamke anakwenda kisimani katika majira ya saa sita alasiri wakati jua ni kali, na yeye ametoka nje ya mji. Yawezekana hii imefananishwa na yale Yesu anayaona maishani mwake. Huyu mwanamke ni mwenye dhambi ambaye amekataliwa na jamii yake. Ni bora kwa huyu mwanamke mla watu angejiepusha na shughuli za kila siku hapo kisimani, wakati wa kila siku. Hata Yesu alikuwa na sababu ambazo zingemfanya asimsogelee, lakini kando na hayo anaanza mazungumzo na huyu mwanamke. Mwanamke huyu alishangaa sana, katika sehemu za mashariki ya kati, maji ni kitu cha maana, katika mazingira, mazungumzo yanafanyika maeneo ya kisima kikuu ambacho kilichimbwa na Yakobo miaka mingi iliyopita.

Mafundisho ya Yesu kuhusu maji ya uzima ni ya kushangaza. Mwanamke huyu anashindwa kuyaelewa na alikuwa na mafikirio kuwa yale maji yaliyokuwa yanaongelewa yalikuwa na nia iliyojificha. Maji ambayo Yesu anazungumzia ni tofauti kabisa. Yesu hayataji lakini msomaji wa injili anaelewa. Yesu anamaanisha mwangaza, ukweli na zawadi ya uhai utokao kwa Mungu. Yeyote anayekutana na Yesu atapata maana kamali ya uhai na hatatamani kitu kingine chochote.

Kama manabii wa Agano la kale, Yesu anaangalia kamili ndani ya moyo wa mtu kupitia kwa hadithi hii ya uongo ya Yule mwanamke. Anabadilisha mjadala kutoka kwa maisha yake hadi mahali pazuri na kuingiza mapigo ya zamani. Mungu atatumikiwa wapi, Gerizin au Jerusalemu? Jibu ambalo Yesu anatoa ni la kawaida kabisa katika injili ya Yohana, sio huko au hapa bali ni katika Roho na kweli. Haya maneno ni kweli tukizingatia uharibifu wa Jerusalemu. Hata wakati hekalu la Jerusalemu lilipoharibiwa bado Mungu alipata kufikiwa kwa maombi. ”Kwa roho na ukweli” - Ni kinyume cha mawazo kuwa ibada ifungwe katika sehemu moja tu. Tunaposoma katika Injili ya Yohana, tunajua kuwa inamaanisha kuwa tunapounganishwa na Mwana, Baba hupewa huduma ya kweli, haijalishi msaada unahitajika wapi.

Mazungumzo yanamalizika wakati Yesu anajitambulisha kwa mwanamke kuwa yeye ndiye Kristo Masihi. Jukumu lake mwanamke kama mwangaza ulianza palepaLe.

Wakati Yule mwanamke anakwenda na kutorudi na Wasamaria wenzake, ni wakati wa majadiliano. Yesu anaongelea kuhusu kutumwa. Yesu haitaji chakula wanafunzi wake nao walishindwa kuelewa kwa maana chakula chake ni kufanya mapenzi ya Mungu. Mapenzi ya Baba yake. Kama vile Baba alivyomtuma mwanawe naye anawatuma wanafunzi wake.

Hakuna ukosefu wa kazi na kukaaka na kungojea. Kungojea kitu kila siku kunahitaji uvumilivu, kupanda na kuvuna. Kilichowaumiza maskini ni njaa na upungufu. Sasa wanafunzi hawakutaka kungoja. Yesu alikuwa amekwisha kupanda sasa jukumu la wanafunzi ni kuvuna. Maneno hayo siyo yalitumiwa tu wakti ule hata wakat ule ujao. Kifo cha Yesu na ufufuo wake unapohubiriwa matokeo yake hayatakiwi kusubiriwa hata siku ile ya mwisho ya hukumu. Anayeshika neno anamfahamu Mwana na hutoka mautini hadi uzimani. Haya ndiyo yanatokea kwa mwenye dhambi na wale Wasamaria waliodharauliwa.

Imani halisi 4:43-54

Aliporudi Galilaya Yesu alipokelewa kwa heshima kuu (Marko 6:1-6) wakati wa kukataliwa ulikuwa umekwisha.

Hadithi kuhusu mfanyakazi wa mfalme aliyeishi kaprenaumu inatufanya tuwaze ikiwa inalinganishwa na ile ya Mathayo 8:5-13 na Luka 7:1-10, katika maelezo haya ni kuhusu maskini na wala hayaelezwi hapo.

Kiina cha maelezo haya ni jinsi huyu afisa alivyomwaamini Yesu . Na majibu ya Yesu kwa huyu mtu kuhusu kusaidiwa ni ya kiburi. Yafaa mtu kumwamini Yesu sio tu kwa ajili ya miujiza, ishara au maajabu bali ni kwa neno tu, hata hivyo Yesu anayasema maneno na huyo mtu anayapokea kwa furaha. Hata kuamini hapa kunamaanisha kuwa mtoto wa Yule afisa alipona kabisa. Anaporudi kutoka Kana kuelekea Kaprenaumu, huyu afisa anakutana na watu wanaomletea habari njema, mwanae aliponywa pale tu Yesu alipozungumza maneno yake. Sasa baba yake aliamini pamoja na wale wengine. Kuamini nako kulikuwa na maana tofauti. Hata ikiwa Yohana haelezi, tunaelewa kuwa imani yake inamwangazia Yesu kama mtu.

Hapa tunafundishwa kuhusu ubinadamu wa Yesu na huduma yake. Yesu ni Mwana wa Baba anayetuongoza, kutoka kwa uongo hadi ukweli, kutoka kwa kifo hadi uzimani.