Injili ya Yohana sura ya 3 – Mungu anaokoa wanadamu

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Emmanuel Samwel Sitta

Maneno ya Utangulizi: Injili ya Yohana na Sakamenti

Sura ya tatu ya Injili ya Yohana inaibua swali gumu sana. Ukilinganisha na Injili zingine, Injili ya Yohana haizungumzi moja kwa moja kuhusu Sakramenti. Yohana harudii maneno ya huduma ya Ubatizo na kuelezea huduma ya Ushirika Mtakatifu. Hata hivyo, katika sura ya tatu Yesu anasema juu ya ubatizo, na sura ya sita ya Injili siyo rahsi kuielewa bila ya kuelewa kwamba inazungumzia kuhusu Ushirika Mtakatifu. Kwa nini Mwinjiristi wa nne anaongea juu ya mambo haya kwa uwazi?

Tunayo maelezo ya kufanana hata kabla: Injili ya Yohana inamtindo wake wa uandishi ambayo imekaa kisanaa zaidi. Mwandishi anatarajia wasikilizaji wake tayari wajue habari ya Sakramenti,na hujenga juu ya kazi iliyofanywa na waandishi wa Injili zingine.

Nikodemo anamtembelea Yesu 3:1-21

Kwa kusafisha hekalu Yesu alikuja kwa umma. Sasa Yohana anasema juu ya kukutana kati yake na takwimu yenye ushawishi mkubwa wa jamii yake. Nikodemo alikuwa Mfarisayo na alikuwa sehemu ya baraza la maamuzi la Kiyahudi wakati wa utawala wa Warumi. Halmashauri ya baraza hili ilikuwa ni sehemu mhimu sana ya maamuzi ya Wayahudi wakati wa utawala wa Warumi. Inahitajika kutambua kwamba vyanzo vya Kiyahudi vinamtaja mtu mmoja aliyeitwa Nikodemo. Alikuwa mtu tajiri sana katika Yerusalemu wakati mji huo ulipoharibiwa katika mwaka 70. Hatuna vyanzo vya kutatua kuwa huenda Nikodemo ni yule yule aliyetajwa na Yohana.

Somo la majadiliano ya usiku ni mfano wa Injili ya Yohana. Hakuna mazungumzo halisi yaliyopatikana kwa sababu Nikodemo hakujua mambo yanayohusiana na Ufalme wa Mungu. Alizungumzia vitu kuhusu mambo tofauti kuliko Yesu. Mara baada ya mazungumzo kuanza, Nikodemo alitulia kimya na kwa makini anamsikiliza Yesu tu. Tunakumbuka maneno kutoka katika utangulizi wa Injili ya Yohana kueleza jinsi Neno lilivyokuja katika ulimwengu wake mwenyewe, lakini wale walio wake mwenyewe hawakumpokea, wala hawakumuelewa Yeye (Neno).

Nikodemo alikuja usiku kwa Yesu kwa sababu aliogopa wayahudi. Kulikuwa na sababu nyingi za muda huo wa ajabu. Lakini pia Wayahudi walifurahia kuzungumza zaidi usiku. wakati wa usiku ulitoa hali ya hewa nzuri kwa mazungumzo.

Yesu alivunja maneno ya Nikodemo ya kujiinua na kuanzisha swali la mazungumzo yote: mtu lazima azaliwe mara ya pili-neno hili kwa Kigiriki linamaanisha kutoka “juu” uchaguzi wa maneno ni ya uhakika na siyo bahati mbaya. Nikodemo hakujua jambo mhimu lakini Yesu alijithidi kufafanua jambo hilo ili aelewe.

Mwanadamu peke yake hajitoshelezi yeye mwenyewe katika ufalme wa Mungu na kukabiliana na utukufu wake. Mtu lazima apokee maisha mapya kabisa kama zawadi. Uzima huu hutolewa kwa watu katika ubatizo, ambao si kama na ubatizo wa Yohana, bali ubatizo ambao Roho Mtakatifu hupokelewa.

Roho mtakatifu hawezi kuamriwa au kulazimishwa na mtu yeyote. Kama ilivyo vigumu kuamru na kulazimisha upepo, ndivyo ilivyo ngumu kuamru Roho wa Mungu. Hapa Yesu anazungumzia kuhusu Ubatizo wa Kikristo, lakini kwa siri na kwa mtindo wake mwenyewe. Tunaelewa ya kwamba Mungu humpa mtu maisha mapya mwenyewe kwa njia ya Ubatizo. Biblia inaelezea muujiza huu kama “Kama kuzaliwa mara ya pili”. Tulizaliwa mara ya pili kwa njia ya Ubatizo.

Wakati Nikodemo angali anasumbuka, Yesu alihusisha ubatizo na maisha mapya karibu na maisha yake mwenyewe. Ukirudi nyuma katika historia, jangwani watu wa Israel walianza kumpinga Mungu na waliadhibiwa kwa kuumwa na nyoka wenye sumu. Waliong’atwa na nyoka walikufa kifo chenye uchungu. Mungu akawahurumia watu wake na kumwambia Mussa ainue nyoka wa shaba katika ncha ya kichwa. Mtu yeyote aliyetazama, aliponywa na hakufa na sumu ya nyoka (Hesabu 21:9). Sasa Yesu ni kama nyoka huyu wa shaba. Mwana wa Mungu ambaye ni Neno aliyefanyika mwanadamu, alisulubiwa na alitukanwa na wote. Kwa njia hii anakuwa nyoka mpya wa shaba: wale wanaomtazama, wanapata uzima mpya, ambao Yesu alimwambia Nikodemo. Hawawezi kuona kifo tena. Kwa njia Hii imani katika Yesu na ubatizo zimetoka sehemu pamoja. Vyote vinahusu Mungu anavyotoa uzima katikati ya kifo. Hii ndiyo maana ya kuzaliwa upya.

Sehemu ya mwisho ya hotuba ya Yesu iko wazi kuwa kuna mambo mawili tu yanayowezekana. kuna giza na nuru, imani na kutoamini, ukweli na uongo. Upendo wa Mungu kwa ulimwengu wenye dhambi umefunuliwa ndani yake kwa kutumwa mwanawake wa pekee katika giza ili kuokoa watu wote. Sasa sisi sote tunakabiliwa na swali la maisha na kifo. Huu ni uhusiano wetu na Yesu. Hasira ya Mungu inabaki kwa wale wanaomkataa mwana pekee wa Mungu. Wale wote ambao wanaweka imani yao katika Kristo, huletwa kutoka giza hadi mwanga.

Sehemu inayochoma: Yohana na theolojia ya msalaba

Hasa katika Injili ya marko na barua za Paulo unaweza kupata kile kinachoitwa “Theolojia ya Msalaba”. Kulingana na theolojia hii Mungu huficha utukufu wake, na huficha nguvu zake katika udhaifu. Kwa wazi zaidi hii inaonekana kwa ukweli kwamba Yesu mwenyewe hufa msalabani, badala ya kuishi maisha ya utukufu na utukufu.

Kwa kushangaza Yohana anaunganisha theolojia ya msalaba na theolojia ya kushangaza ya heshima. “Yesu amefufuka kutoka chini”, anakuja kumvuta kila mtu kwake.hii hutokea kwa njia mbili. kwanza, Yesu “aliinuliwa” kutoka kwenye ardhi ili asulubiwe, na kutukanwa na kuonewa na wote. Pili aliinuliwa kwa utukufu wa Mungu kutoka ambapo yeye alipitia awali, na ambapo humvuta kila mtu amwamini yeye. Kwa maana hii, usiku wa giza umepelekwa katika utukufu, na udhalilishaji unaongoza kwa heshima na utukufu. Haya yote hutokea ili ulimwengu wa dhambi uokolewe.

Harakati mbili upande kwa upande 3:22-24

Kihistoria inavutia ukweli kwamba kwa muda, harakati zote mbili zinaanza na Yohana mbatizaji, na wanafunzi wa Yesu, waliofanya kazi bega kwa bega. Wanafunzi wa Yesu walibatiza watu pia (4:4). Hatuwezi kusema chochote kuhusu ubatizo huu. Inaonekana ilikuwa sawa na ubatizo wa Yohana ambao uliandaa kuja kwa ufalme. Mshikamano wa harakati zote mbili ulimaliza wakati wa Herode alipomfunga Yohana gerezani.

Kristo na Kanisa lake 3:25-36

Mshikamano wa upande wa harakati mbili kwa upande wa shaka ulifufua swali ambalo harakati ililipa kipaumbele. Yohana mbatizaji alitakiwa kujibu kwa wanafunzi wake wakati wanawaagalia watu wakimkimbilia Yesu. Yohana anajibu kwa mfano unaohusishwa sana na picha nyingi za Agano la kale.

Angano la kale mara nyingi linalinganisha uhusiano kati ya Mungu na Israel na ndoa (Yer 3:, Eze 16 na 23; Maneno ya nyimbo). Maandiko haya labda ni ya nyuma wakati wa Yohana, bila wivu na kinyume na furaha, kuchukua sehemu ya kusaidia. Yeye ni rafiki wa bibi harusi, msemaji ambaye aliyesaidia kumleta bwana harusi katika uhusiano mzuri na upendo wake. Sasa Kristo na Kanisa lake walikuwa tayari kuwa na ujuzi. Hii inamjaza Yohana kwa furaha kubwa ya ajabu. Picha hiyo hiyo mara nyingi inaonekana katika Agano Jipya, hasa katika sura za mwisho za mafunuo.

Tofauti kati ya mashahidi wawili ni ya kushangaza. Yohana alikuwa mwanadamu na kuchukuliwa kutoka duniani; kwa hiyo mafundisho yake pia ni ya kidunia. Yesu alikuja kutoka mbinguni na ushuhuda wake ni wa mbinguni. Ni kweli na haki, ingawa wachache tu hukubali. Yeye ambaye anamini maneno ya Yesu anaona kwamba Baba amempa mwanaye nguvu juu ya kila kitu. Bila mipaka yeyote. Kwa njia hii Yesu huwapa wote uzima wa milele. Yeye, ambaye anakataa hayo, yuko chini ya ghadhabu ya Mungu. Ushuhuda wa Yohana unarudi katika mandhari ya kawaida ya Injili ya nne: maisha na kifo (au wakati huu ghadhabu ya Mungu), ukweli wa mbinguni na njia mbaya za ulimwengu. Katikati ya wote ni Yesu, Mwana wa Mungu. Uzima wetu wote umeamua kuhusianisha na yeye.