Yesu ni zawadi na mfano wa kuigwa

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Watu wengi wanaongea kuhusu Yesu, lakin ihawataki kuwa wakristo, zaidi wanataka kuwa watafutaji, wanakubaliana kwa nguvu sana kwamba mafundisho ya Yesu ni ya haki na yanaweza kuwa mazuri kufundishwa na kuishi kama yeye.

Watu hawa wanaweza kuwa hata na mafikirio ya kujishusha sana mbele ya watu wengine. Lakini ni wapi wanapata makosa kama haya? Hawawezi kuona hakika maelezo yote yaliyo hapo juu.

Yesu ana maana mbili kwetu wakristo, moja kama zawadi na ya pili kama mfano wa kuigwa, pasipo kugundua hayo mtafutaji atabakia kwenye mawazo yasiyotosheka.

Yesu ni zawadi

Tunaposema Yesu ni zawadi tuliyopewa tuna maana hii; Alizichukua dhambi zetu na kutufanya watoto wa Mungu, hata kama hatukustahili hivyo ninaweza kuwa mwenye dhambi na msafi kwa sababu Yesu amechukua matendo yangu ya udhaifu juu ya msalaba wa golgota. Na kwa nyongeza zaidi atatembea nami kila siku katika maisha yangu na hatachoka kunilinda, kunisamehe na kuniinua.

Hii ni zawadi ninaabudu wakati ninafurahia sakramenti ya ubatizo, chakula cha Bwana au maungamo na kila saa ninapofungua biblia. Wakati huo hakuna madai ni Mungu tu anatoa kwa upendo wake

“Kwa kuwa hamkupokea roho ya utumwa iletayo hofu: bali mlipokea roho yakufanywa wana ,ambayo kwa hiyo twalia Aba, yaani baba."
(Warumi 8:15 SUV)

Yesu ni mfano wa kuigwa

Tunaposema kuwa Yesu kwetu ni mfano wa kuigwa tuna maana hii; wakati Yesu alipokuja chini kutoka katika mng”ao wa utukufu wa Mungu akaja katika ulimwengu huu mchafu na kutoa maisha yake kwa ajili yetu alikuwa mfano kwa wafuasi wake wote. Yesu aliyaona maisha yake si kitu aliponiokoa mimi mwenye dhambi, kwa hiyo ina maana wajibu wangu ni kuacha maisha yangu ya ubinafsi na kumpenda jirani yangu kama nafsi yangu. Huu upendo si , tu wa nadharia zaidi una Kristo pale juu msalabani kama unavyoendelea kuwa mfano wa kuigwa ambaye alijitoa kafara kwa ajili ya wenye dhambi na zaidi aliomba juu ya msalaba kwa wale wote waliomsulubisha. Nimesamehewa mara nyingi hivyo mimi sina sababu ya kutosamehe na kuwa mchoyo au kudharau wengine

“Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.
(1 Yohana 4:19 SUV)

Zawadi mfano wa kuigwa, na utaratibu wao sahihi

Hivyo Yesu ni vyote zaidi, na mfano wa kuigwa. Watu wengi wanamchukulia kama barua, hili halijatumika kwa vyovyote, kama hawajaelewa ile ya kwanza na zaidi, Yesu ni zawadi kwetu. Watu wengi wana mashaka kwa kushanga mbele ya mkuu wa mfano wa kuigwa. Hawa wanajumuishwa, kwa mfano Wahindu, Budha, ambao wanaabudu sanamu lakini hawajampata Kristo wa kweli, Yesu kama mtu amebaki siri mpaka alipojitambulisha kwetu kama zawadi. Baada ya hapo moja kwa moja amekuwa mfano kwetu pia.

Yote katika yote kwanza Yesu ni zawadi kwetu, na ya pili mfano wa kuigwa.

Kama tutamchukulia yeye kama mfano wa kuigwa tu, hatutaelewa Kristo wa kweli na hakika tutabaki nje ya ukristo.

Mimi ni mkristo kwa jina baada ya Kristo, kwa sababu Yesu alinifanya kuwa mtoto wa Mungu. Maisha yangu yaliyobaki ni kitu kikubwa, yananivuta kutamani kujifunza kutoka kwa aliyemkuu wa kuigwa Yesu.