Vita vya mkristo vya kale na vipya vinanavyoendelea

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Rev. Emmanuel Sitta Samwel

Nyaraka za mtume Paulo zinajumuisha mafundisho mengi mhimu, ambayo siyo rahisi kuyaelewa kama tukisoma kifungu kimoja tu cha Biblia. Tunahitaji kusoma nyaraka nyingi za Mtume Paulo upande kwa upande ili kuweza kuongeza uelewa wetu. Hii ndiyo hali halisi ya Biblia kuwepo na ni safari ndefu katika uvumbuzi.

Wakati huu tunajifunza nini kuhusu Paulo anafundisha juu ya “Mtu wa kale” na “Mtu mpya”. Huu ni mtazamo ambao hauwezi kufanana na mitazamo mingine. Pia tunaweza kuzungumzia kuhusu “Adamu wa kale” na “Adamu mpya” au kuhusu Mwili au roho. Mitazamo hii haiwezi kufanana, lakini kwa mapana zaidi inaongelea kitu kile kile. Mwisho tunaweza kuhitimisha katika urahisi na uhalisia wa mambo ambayo ndiyo kiini cha maisha ya Mkristo.

Pande mbili za mkristo

Msomaji anaweza asielewe hiki kitu : katika mazingira ya neno “mwili wa nyama” haimanishi lina maana ya mwili na mabaya, vilevile neno “roho” halina maana ya kitu kilichopo kwa uhalisia na ni kisafi katika sehemu ya binadamu. Aina hii ya kutenganishwa kati ya mwili na nafsi ni sehemu muhimu ya fikira za Kigriki. Lakini katika fikra za kiebrania mtu ni mmoja na hana mugawanyiko wa vipande vipande.

Paulo alimanisha kitu Fulani ambacho ki msingi ni kitu kirahisi: “Mwili” neno hili rejea kwa neno “mimi” ambalo linamaanisha ni nafsi ya mtu mmoja pekee bila kuhusisha ukombozi wa kazi ya Kristo. Pia mwili unahusisha mtu kwa ujumla wake. Lakini “Roho”inahusisha sehemu ya mwili wa mtu, lakini kama mtu aliyekombolewa, sasa ametokana na Mungu mwenyewe.

Kwa hiyo, sasa tumefikia sehemu tutakayozungumzia kwa leo. Mkristo ana pande mbili, lakini kwa asiyeamini ana upande mmoja pekee. Katika Mkristo kuna sehemu ya “mwili” na “roho”, “mtu wa kale” na “mtu mpya”, “uumbaji wa kale” na “uumbaji mpya”. Paulo ametumia maelezo hayo yote ili msomaji apate kufahamu vizuri. Katika watu wasioamini wanasehemu moja tu ambayo ni upande wa pili tu, “mwili wa nyama”, “mtu wa kale”, “Adamu wa Kale”na “uumbaji wa kale”. Mkristo anazo pande zote, na kwa maana hiyo anavita ndani ya moyo wake. Ngoja tuangalie pande hizi mbili jinsi zilivyo.

Kale/zamani na hatia

Sura ya kwanza ya barua ya mtume Paulo kwa warumi ni maelezo yake kuwa nini mwanadamu anacho katika nguvu zake mwenyewe. Neno mwili halipo lakini jambo hili liko wazi. Kwa ujumla wake mwanadamu anegeuka nyuma ya Mungu wa kweli na amechagua kutumikia miungu ya uongo badala ya utukufu wa Mungu wa kweli. Hii ndiyo sababu ya Mungu kugeuka nyuma ya mwanadamu na kumwacha katika maisha ya dhambi. Kwa hiyo kila mwanadamu ni kama amefungwa katika giza nene ambapo hakuna mwanga utakaoangaza. Dunia hii ni ufalme wa dhambi na kifo. Maisha haya ni kuishi bila Mungu. Ghadhabu ya Mungu siku moja itakutana na ufalme huu wa dhambi.suala si kuhusu matendo ya mtu mmoja mmoja, lakini kuhusu uasi kamili wa dunia nzima. Na hukumu kamili ambayo inahusishwa na hayo.

Sura ya saba katika Barua ya Paulo kwa Warumi inatoa maelezo mazito kabisa ya upande wa kale/zamani wa mtu:

"Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati."
(Rumi 7:18, SUV)

Sehemu nzima inaonyesha kwamba mtu kwa upande wa zamani hauana kitu kizuri cha kutoka kwa Mungu. Ni hali ya upotevu kabisa kugeuka mbali na Mungu na kuwa chini ya hukumu.

Sura ya tano ya Warumi inatupa kutuonyesha nakala mbili za picha za Adamu: mtu wa kwanza yuko katika dhambi, na anastahili mshahara wake wa dhambi ambao ni Mauti na jehanamu. Urithi huu yeye alitoa kwa kizazi kijacho na kutoka huko juu wamekwisha kupitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. urithi wao kutoka kwa wazazi wao na kupita wao na kwa watoto wao. Wakati chimbuko la mtoto mchanga si heshima kwa kuwakumbusha juu ya ukweli kwamba mtoto mara moja hufa. ni kweli, hata hivyo, kama ni kweli kwamba yeye hubadilishwa na dhambi na anastahili kuhukumiwa “Adamu wa zamani” “mtu wa zamani”, “mwili”tu kuwepo katika yeye sisi ni yote katika umri au jinsia watuma wa hatima ya ukiwa wa dunia hii.

Mpya na ya ajabu

Ujumbe mkubwa wa barua ya Paulo ni kwamba Mungu alimtuma mwanaye duniani kuchangia kitu kipya kabisa kwa ajili yetu. Kile kilichotendeka katika Golgotha, ni kile kilichokuwa kimepangwa katika moyo wa Baba Mungu kwa muda mrefu kabla ya dunia kuumbwa.

“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya”. Hii yote ni kazi ya Mungu aliyetupatanisha sisi na nafsi yake, naye alitupa huduma ya upatanisho; yaani, katika Kristo Mungu alikuwa akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, bila kuhesabu makosa yao juu yao, nao kuwakabidhi ndani yetu neno la upatanisho.
 Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo, Mungu hufanya rufaa yake kupitia sisi. Twaomba ninyi kwa ajili ya Kristo, mpatanishwe na Mungu. Kwa ajili yetu alijifanya mwenye dhambi, ili ndani yake sisi tupate kuwa na haki ya Mungu. Wafanya kazi pamoja na Mungu. Basi sisi hukata rufaa kwa wewe kutopokea neema ya Mungu bure”
(2 Kor 5:17-6:1, SUV)

Maana huwezi kujisaidia mwenyewe, isipokuwa Mungu mwenyewe katika Golgotha ilivyovigumu kwa mtu. Mifano mingi imeweza kuelezea kazi ya kuokoa ya Kristo, lakini labda moja zaidi inaonyesha ni hii: Ni “kiumbe kipya”. Ni kunasa kilichokwisha vunjwa kwa dhambi baada ya kuudwa kwanza. Inachukua mbali ya Adamu wa zamani na karama mpya. Ni wakati ambapo roho, kwamba zamu kwa Mungu na maisha kwa ajili yake ni walichangia kwa mtu.

Kutokuvaa hadi kuvaa

Kwa hiyo mtu ametenda dhambi katika mwili kwa nguvu yake. Mkristo amepewa zawadi kubwa na Mungu, pia amepewa roho na mwili, hivyo mwili na roho zipo katika yeye. Vita kati ya vitu hivi viwili ni endelevu, uchu na kutokuwa na huruma na mwingine. Sura ya kutofautiana lakini suala ni sawa: mwili na roho kupambana dhidi ya kila mmoja. Katika wagalatia 5 Paulo anaeleza jinsi roho inavyojenga “kazi ya roho” na jinsi mwili unavyojenga kazi za mwili”:

”basi nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtatimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho. Na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana hata hamuwezi kufanya mnayoyataka.”
(Gal. 5:16-17, SUV).

Orodha ndefu ya matunda ya roho na kazi za mwili kufuata baada ya hii. Onyo kubwa limejumuisha pamoja.

Katika barua ya Paulo kwa warumi na sura ya tatu Paulo anajibu kwa swali kama mkristo anaruhusiwa kuwa na uhuru wa kutenda dhambi, kwa kuwa kila kitu kusamehewa. Jibu ni kali: hapana, kwa sababu tumebatizwa. Ubatizo kuashilia kifo cha mtu wa kale na kuzaliwa upya kwa mtu mpya. Kwa maana hii sisi daima kurudi kwake.

”je! Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo nasi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake. mkijua neon hili ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubiwa pamoja naye ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena.”
(Warumi 6:3-6)

Sura ya tatu ya wakolosai ikanyanyua juu zaidi vielelezo vikubwa, kama ifuatavyo:

”lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote: hasira, ghadhabu, uovu, matukano na matusi vinywani mwenu. Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale pamoja na matendo yake; mkivaa utu upya unaofanywa upya ili mpate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeumba.”
(Kol. 3:8-10, SUV)

Maisha halisi ya Mkristo ni hasa haya: tumevuliwa kutoka mwili na tumevikwa katika Roho. Hii haitokei mara moja lakini tukiwa tungali tunaishi katika dunia hii. Baada ya huu “mwili”, “mtu wa kale” na “Adamu wa kale” au kwa namna yeyote neno sisi tunaloweza kutumia ni neno mtu mpya, mtakatifu katika Kristo kufika mbinguni ambako ndiko nyumbani.