Sheria ya Musa na wakristo

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Emmanuel Sitta Samwel

Biblia, kitabu kitakatifu cha wakristo kinajumuisha sehemu mbili: Agano la Kale na Agano Jipya. Baadhi ya waalimu wamefundisha kwamba Agano la Kale lipo si kwa ajili ya Wakristo, lakini mafundisho haya moja kwa moja yalikataliwa na wakristo wa kwanza na makanisa ya siku nyingi. Hadithi za Abrahamu, Isaka na Yakobo, na sehemu ya historia ya watu wa Mungu na kitabu cha Zaburi kimekuwa ni sehemu ya huduma za jumapili za kanisa tangu mwanzo.

Lakini vipi kuhusu sheria ya Musa na amri zake? Mtume Paulo, alikataa dhahili wazo kwamba wakristo wapagani lazima watii sheria ya Musa. Alifundisha kwamba sheria ilitolewa kwa ajili ya watu wa kiyahudi. Baada ya miongo michache mtazamo huu ulishinda na hakukuwa na upinzani. Mambo yalikuwa ni magumu na yalistahili kuangaliwa kwa karibu zaidi.

Tunamanisha nini kuhusu neno “sheria”?

Kwa kuanza ni vizuri kutambua kuwa neno “sheria” linamanisha mambo mengi tofauti tofauti, ndivyo ilivyo hata katika Biblia na kwingineko. Inamanisha sheria, amri, au mazoea. Wayahudi hawakutenganisha kati ya sheria iliyoandikwa na sheria isiyoandikwa kutoka kwa mwingine kwa umakini kama sisi tunavyofanya. Hivyo wakristo walirithi maana mbalimbali kwa ajili ya neno, kutoka vyanzo mbalimbali. Hii imesababisha na bado inasababisha baadhi ya machafuko. Tunaweza kutambua angalau njia zingine kama zifuatavyo:

1) Sheria ina maana ya ya vitabu vitano vya kwanza vya Biblia, vitabu vya sheria (maana yake vitabu vitano). Kama chombo hii inamanisha kwa mfano pamoja na taarifa za Ibrahimu (Rumi 3:31). Baada ya kuzungumza kuhusu Agano la Kale mtu anaweza kutenganisha “sheria” (yaani vitabu vya sheria) manabii na maandiko au “sheria na manabii.”

2) Sheria ina maana ya sheria yote, ambayo Bwana aliitoa kupitia Musa (Gal 3:17) au sehemu mojawapo. (Gal 5:2-3).

3) Sheria maana yake ni njia ya kawaida ya maisha ya wayahudi. Kwa maana hiyo kwa mfano mwanahistoria aitwaye Josefos, alisema kuwa sheria inahitaji kwamba watoto hufundishwa kusoma. Hii haikuwekwa pamoja katika sheria ya Musa, lakini ilikuwa desturi ya Wayahudi.

4) Sheria ni utawala wa vitisho ambao unatoa hukumu kwamba, mwenye dhambi anahitaji kuwa huru (Warumi 7).

5) “Sheria” maana yake ni mapenzi ya madai ya Mungu. Hasa katika imani ya Kilutheri, inamanisha kinyume cha neno “injili”; sheria inamaana ya mambo Mungu anahitaji na hiyo haitupi sisi chochote. Injili maana yake ni mambo yote Mungu anayotupa sisi kwa sababu ya Yesu Kristo-na hiyo haitudai sisi chochote. Dhana hizi mbili ni moja ya masuala mengi mhimu katika imani ya Kilutheri.

6) Sheria inamaana ya kanuni za maadili zilizotolewa kwa Wakristo (“sheria ya upendo” Yakobo 1:5)

Hivyo, tunaona ya kwamaba neno moja linaweza kumanisha mambo mengi tofauti. Siyo jambo la kushangaza kwamba wengi huchanganyikiwa na suala hili. Hata hivyo utafiti wa mambo unahitaji uvumilivu.

Wayahudi wakati wa Yesu na sheria

Katika wakati wa Yesu, sheria ilikuwa chanzo kikuu cha kiburi na furaha kwa wayahudi. Kuishi kwa mjibu wa sheria, kulileta tofauti kati ya Wayahudi na watu wengine yaani wapagani. Sheria ilikuwa si kuchukuliwa mzigo lakini furaha kubwa na zawadi. Mtazamo huu unaonyeshwa, kwa mfano katika Zaburi 119:92: “kama sheria yako isingekuwa furaha yangu, wapendwa wamepotea katika taabu yangu”.

Waalimu wa Kiyahudi wametofautisha mamia ya amri katika sheria. Kila mojawao ilifuatiwa na maelezo ya jadi. Yesu alisema kwa kurejea jambo hili akilifananisha na kama “mafundisho ya mila ya wazee”.

Mfano: Sheria ya Musa (Kutoka 25:3) inakataza kuwaheshimu Waisrael kwa kuwapa zaidi ya mapigo 40. Kwa mujibu wa mafundisho ya jadi sheria ililindwa kutokana na uharibifu, kwa hiyo adhabu ya kiwango cha juu ilikuwa mapigo 39. Mtume Paulo anaeleza hili katika barua yake kwa wakorintho (2kor 11:24). Hawakuwa na huruma kwa mtu ambaye angepaswa kuadhibiwa, lakini walikuwa makini wasikose sheria takatifu ya Mungu. Sheria ilikuwa “inalindwa kwa uzio” ili isiweze kuvunjika, hata kwa ajali. Kwa njia hiyohiyo, Farisayo ambaye Yesu alielezea, alitoa zaka ya kila kitu alichokizalisha, na zaidi ya yote aliyonunulia, lengo lake ni kuwa na uhakika (Luka 18:12). Ilikuwa bora kulipa zaka mara mbili, kuliko kutolipa kabisa.

Kwa kila amri, kuna mafundisho Fulani ambayo inalezea. Mamia haya ya amri, yalihusishwa na maelfu na maelfu ya mafundisho, na kwamba mtaalamu halisi alipaswa kufuata. Hivyo inaeleweka Kama Farisayo alihisi kuridhika sana juu ya sheria na utaalamu wake. Kwa myahudi, sheria ilikuwa msingi wa utambulisho wa kitaifa. Ilijumuisha sheria ya kijamii, sheria ya maadili na maagizo ya kumwabudu Bwana.

Mataifa (Wakristo wa kipagani ) na Sheria

Baada ya kifo na ufufuko wa Kristo, msingi ni kwamba Wayahudi wataitii sheria, hata baada ya kuanza kumwamini Masihi. Wengi walidhani kwamba Wayahudi wanapaswa kutii sheria pia. Walifikiri kwamba wapagani wanngekuja kwa Kristo kwa njia ya Kiyahudi. Hii inamanisha kuwa watu walihitaji kutii sheria ya Musa na kwanza, kutekeleza kutahiriwa kwa wanaume. Basi baada ya hapo mtu angeweza kuwa Mkristo.

Mtume Paulo na Barnaba walifundisha tofauti. Katika safari yao ya umisionari (Mdo 13-14) walihubiri injili kwa mataifa, lakini hawakuwaomba kufuata sheria ya Musa. Kitu ambacho Mungu alifanya katika Kristo ilikuwa ya kutosha na ilikuwa inayomilikiwa kupitia ubatizo. Hivi karibuni kulikuwa na mgogoro ambapo Luka anaeleza katika njia ifuatavyo:

"Wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka. 2. Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee kwa habari ya swali hilo”.
(Matendo 15:1-2)

Mtazamo huu wa Paulo unaweza kusomwa katika barua kwa Wagalatia:

“10. Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye. 11 ni dhahili ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria kwa sababu“ mwenye haki ataishi kwa imani.”
(Wagalatia 3:10-11)

“Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.”
(Wagalatia 5:4)

Katika mkutano wa mitume, maoni ya Paulo yalishinda. Kulingana na injili ya Luka, maoni yaliundwa na Petro na Yakobo. Petro anasema kama ifuatavyo:

“Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua”.
(Matendo 15: 10)

Yakobo anasema:

“Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi; Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa”.
(Matendo 15: 19)

Kuna maelezo mafupi yaliyotolewa katika mkutano wa Mitume, ushauri ambao huwawezesha Mataifa kuishi pamoja na wayahudi. Ninaelewa kuwa, kwa mfano, maelekezo ya kutokula wala kutokunywa damu ni halali kwa haraka kama mimi nikiishi kati ya Wayahudi. Ikiwa mtu hakubaliani, mwache yeye asile. Haya ni maelezo ambayo hayapingani na wazo kuu: Wamataifa (wasio Wayahudi) hawana haja ya kufuata sheria ya Musa. Wayahudi hufanya lakini si njia ya wokovu kwao. Watu wachache tu hupuuza maneno ya Paulo, Petro na Yokobo na kujaribu kukaa kama mataifa mengine chini ya sheria ya Musa. Baada ya muda watahukumiwa kwa sababu hiyo, kwa sababu maneno ya Paulo hayapaswi kuchuliwa kwa wepesi.

Kwa hivyo, sheria imefutwa?

Msingi wa jambo hili uko wazi: Sheria haikupewa watu wa Mataifa (wasio Wayahudi) na hivyo hatuna haja ya kuitii.
 Ni muhimu kusisitiza, kwamba neno “Sheria” hapa , linamaanisha Sheria ya Musa. Ikiwa tunazingatia maana nyingine kadhaa ya neno “Sheria”. bado inatumika. Kwa mfano kuna mapenzi ya Mungu ya kudai na Wakristo wanawajibu wa kufuata mapenzi yake. Lakini hili ni jambo ambalo litajadiliwa baadaye.

Agano Jipya linaeleza waziwazi, kwamba mataifa hayafungwi na sheria ya Musa na hii ni wazi kuwa ni hatua yetu ya kuanzia. Wakati huo huo, Agano jipya mara kwa mara linaelezea amri ambazo Mungu alitoa katika Agano la kale (Kwa mfano Mt. 5: 21, 27) kwa hiyo, tunaweza kuelewa kwamba sheria zote hazikufutwa. Tunapojaribu kuelewa sehemu ambazo ni za kwetu na ambazo siyo, hatua ya mwanzo ni kile Paulo alichofundisha: sheria siyo kwa ajili yetu. Ikiwa kila kitu kinasemekana kudumu kwetu, mtu anayedai hayo , anahitaji kuwa na uwezo wa kuhalalisha mahitaji yao. Hakuna mtu anayeweza kuchagua sehemu ya sheria, kama inavyopendeza, kwa mfano amri ya kula chakula, na kusema kuwa inakaa kwa wote. Mtu lazima awe na uwezo wa kudhibitisha kwa nini hii ingekuwa bado kwetu, na hata zaidi, Roho Mtakatifu anahitaji kuidhinisha katika mioyo ya wasikilizaji, kwamba mafundisho ni sahihi. Vinginevyo mwalimu ni roho ya mwituni na ni mtumwa wa dhamiri.

Tunaweza kutambua maeneo yafuatayo:

1) Kwa mujibu wa barua kwa Waebrania, Kristo na dhabihu yake alifanya mbadala wa dhabihu nyingine zote, ambazo zilikuwa tu kivuli cha mema ambayo yangekuja. Kwa njia hii, sheria zote za dhabihu zimeharibiwa kuhusu Wakristo. Ndio sababu sikujaribu kwenda hekaluni kutoa dhabihu ya njiwa vijana wawili, baada ya mtoto wangu kuzaliwa. (Luka 2:24).

2) Kulingana na Yesu (Mk 7:15), vyakula vyote ni safi na Paulo anaheshimu hili (Rumi 14:14). Hii ndiyo sababu tunaweza kula nguruwe na nyama, hata kama sheria ya Musa inakataa vyote kwa pamoja (Lawi 11:7-12). Ni vyema kwa Wakristo kuwa rahsi kuzingatia kile wanachokula, ili wasiumize dhamiri ya mtu mwingine, lakini chakula peke yake haimfanyi Mkristo kuwa mchafu, si zaidi ya manufaa ya kula peke yake.

3) Kwa mujibu wa sheria ya Musa, kwa mfano, kuhusu tendo la kingono (Lawi 15:16-18) linaongoza kwenye uchafu wa kidini, pamoja na hedhi na kugusa mtu aliyekufa. Hizi hazihusiani na dhambi – kinyume chake, ni sawa kama sitamzika baba yangu. Lakini kwa mujibu wa sheria ya Musa, mtu anahitaji kuoga na kuepuka kuwa na watu wengine hadi jioni ifuatayo kwa sababu wao ni wanajisi-hii haiwahusu Wakristo wa kipagani.

4) Sheria ya Musa pia ilikuwa sheria ya jamii ya Israeli. Kwa sisi sio; ikiwa tunapigana, tunaadhibiwa kulingana na sheria zetu za kitaifa, ambazo siyo tatizo kwetu. Wachache wamedai utekelezaji wa kumbukumbu la torati (Kumb 25:5-6).

Sehemu hizi tofauti za sheria zimekwisha kufutwa. Hata hivyo, tunaweza kufanya orodha ya sehemu nyingine za sheria ambazo zinahusu pia mataifa.

  1. Sheria ya maadili, msingi ambao ni amri kumi, inatumika. Kwa mfano, si lazima ni ue mtu yeyote, wala kuvunja ndoa yangu, wala kusema uongo. Wakristo wa kwanza walifanywa kwa mjibu wa sheria ya maadili. Hii inaweza kuonekana katika orodha ya wema na ubaya katika Agano jipya, kwa mfano, katika 1Kor 6:9-11 na Gal 5:16-26.

  2. “Sheria”, kwa maana ya “mapenzi ya Mungu”, inamatumizi yake ya kiroho ambayo Paulo anayazungumzia katika barua yake kwa warumi 3:19-20: “Sasa tunajua kwamba kila kitu ambacho sheria inasema, inasema kwa wale ambao ni chini ya sheria, ili kila kinywa kiwekewe na dunia nzima ikawajibika kwa Mungu. Kwa hiyo hakuna mtu atakayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa matendo ya sheria. Badala, yake kupitia sheria tunapata ufahamuwa dhambi zetu.”

Yanapokuja maswali ya pekee, kila Mkristo anapaswa kusikiliza dhamiri yake mwenyewe:
 Wengine wanafkri kwamba mitume 15 huzuia matumizi ya damu kama lishe, na ni vizuri kufikiria katika njia hii.
 Madhehebu mengi huwaomba waumini wao kutoa zaka: agano jipya halitoi ombi hili, lakini tunatakiwa tusiwe na tamaa na tunashauriwa kutoa mengi na nje ya mapenzi yetu ya bure. Hata hivyo, hakuna mtu anayeweza kulipa zaka.  Agano la kale linamuzuia mtu kuchanjwa chale (Walawi 19:28), wakati agano jipya halikusema juu ya jambo hili, lakini katika watu wa Agano Jipya wanaonya, mara kadhaa, sio kulipa kipaumbele kwa maonyesho yao. Mara kwa mara wanaume wanapaswa kuwa na nywele zao kama inavyohitajika katika sheria ya Musa (Walawi 19:27), ingawa mahitaji haya hayatii katika aina yeyote ya kufukuzwa iliyotolewa hapo juu.

Katika maswali haya maalumu, hebu tuache kwa ufahamu na dhamiri safi utumishi wa Mkristo wa kuwaambia watu nini kilicho sahihi na nini kisicho sahihi.

Historia ya kanisa

Sehemu ya Mataifa ya kanisa la kwanza hivi karibuni ilikua kwa kasi kubwa kuliko sehemu ya Kikristo ya Kiyahudi. Mafundisho ya Mtume Paulo juu ya sheria yalianza hivi karibuni. Ukosefu wa mjadala mzuri uliongozwa na hali ambapo kila mtu alikuwa amesahau mgogoro uliokuwepo (ulioelezwa katika barua kwa Wagalatia na katika Matendo).
 Ilikuwa ngumu kuelewa kwamba amri ni sehemu ya kitabu kitakatifu lakini haikuhusika kwa ajili yetu. Barua ya kwanza iliyoandikwa kwa jina la Barnaba, hujitahidi kuwaweka Wakristo huru kutoka kwa utiifu wa sheria ya Musa. Kwa bahati mbaya barua hiyo inabadilisha tafsiri halisi na ufafanuzi wa kiroho. Katika Karne ya nne (kwa mfano wakati wa Clement na Alexandria) sehemu za sheria zilichukuliwa badala ya kiholela na wasikilizaji walipaswa kutekeleza sheria hizi. Hali hiyo ikawa mchanganyiko zaidi, na katika karne ya tano baadhi ya Mataifa walianza kudai kwamba sheria za Kiyahudi za usafi kulingana na sheria ya Musa, zifuatwe. Madai haya yalikanushwa (mfano na . Didaskalia), lakini watu hawakukumbuka kwamba barua ya Wagalatia ilizungumzia kuhusu mada iliyokuwepo. Barua kwa Wgalatia ingekuwa imewasaidia sana.

Luther na sheria

Martini Luther alikataa jitihada kubwa za kutuliza mahubiri na mafundisho ya sheria katika kanisa. Hapa, ni mhimu kuelewa kwamba kwa Luther, “sheria hasa inamaanisha “mapenzi ya Mungu” na siyo Sheria ya Musa na sheria za usafi. Mjadala ulioelezwa katika barua kwa Wagalatia ulifanyika karibu miaka 1500 iliyopita, na matokeo yake yalieleweka. Badala yake, tatizo ilikuwa kwamaba baadhi walijaribu kutuliza mapenzi ya Mungu ya kudai: kulingana na Luther, hii ilikuwa njia ya kupoteza Injili pia.

Baadaye Watheolojia wa Kilutheri walieleza matumizi matatu, au sababu, katika sheria:

Sheria imetolewa kwa watu kwa sababu tatu tofauti:
1. Inawaweka watu wasiojizuia na watu wasiowasikivu nje na chini ya nidhamu,
2. Inawafundisha watu kutambua dhambi zao,
3. 3. Kwa Wakristo ni mwongozo wa kutosha, ambao wanapaswa kuandaa na kuelekeza maisha yao yote-kwa sababu hawajapata kuondoa mwili.

Matumizi ya mara kwa mara ya sheria kama hatua ya pili inavyoelezea, inajumuisha pamoja na mafundisho ya Injili, husababisha matumizi ya tatu ya sheria. Mkristo ana wajibu wa kusikiliza sauti ya Mungu –kwa hili, imani ya Kilutheri hufuata, kwa mfano, sura ya sita ya Waraka kwa Warumi – lakini Mataifa au Wakristo wa kipagani hawajafungwa taratibu na kanuni katika Sheria ya Musa.