Biblia inafundisha nini kuhusu ubatizo?

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Katika uwakilishi wangu huu nitaangazia kuhusu swali la ubatizo na kusudi kutoa ufupisho wa kifkra kuhusu jambo hilo. Kusudi lake ni kuzungumza na wale wote wanaokataa Ubatizo kama chombo cha neema, mfano, dhambi zinasamehewa katika ubatizo. Mkazo wangu utafuata sana tamaduni za uwelewa wa Kilutheri.

Kwa asili uwakilishi huu ni mazungumzo ya amani. Kusudi ni kwamba msomaji atulie mpaka ukurasa wa mwisho na kufikiria juu ya ipi kati ya maandiko haya anaweza kukataa. Baada ya kufikiria anaweza kutazama juu ya hizo maana kwa sababu katika huu uwakilishi kuna baadhi ya mafikirio mengi sahihi. Kati yake, mingi ni mifano kutoka agano la kale, “Ubatizo wa Yohana” (Matendo ya mitume 19) na matukio mengi muhimu ya ubatizo kwa mfano ndani ya matendo ya mitume pasipo kuiondoa.

1. Mwanadamu amepotoka kabisa

Swali la ubatizo haliwezi kueleweka pasipo kuliweka katika uzio mzuri: Msingi wake ni juu ya wanadamu wote kutengwa kabisa na Mungu.

Katika sura ya kwanza ya kitabu cha Warumi kinatuambia juu ya msingi muhimu, rahisi na huzuni, Mwanadamu alitakiwa amjue Mungu na kumtumikia, kwa sababu ya ufunuo wa jumla, lakini mwanadamu hakufanya hivyo, lakini aligeuka nyuma juu ya Mungu na kuanza kutumikia miungu (sanamu). Kutokana na hilo Mungu aligeuka nyuma juu ya mwanadamu na kumwacha katika dhambi. Hii ndiyo sababu ulimwengu upo jinsi ulivyo, sehemu isiyo na tumaini, ya dhambi na giza.
Hakuna hata mmoja hapa katika hali yao ya ”kimwili” (mfano kama walivyo anguka wenyewe) anamtafuta Mungu, na kwa nyongeza Mungu amejificha mwenyewe kwa mwanadamu na hamruhusu hata mmoja kumtafuta yeye. Mungu ni Mungu aliyejificha. Hata kama kwa haki ya mwanadamu haiwezi kumleta yeye karibu na Mungu, lakini inampeleka zaidi mbali na Mungu.

Hivyo msingi ni mwanadamu kutengwa kabisa na Mungu. Kiini cha ujumbe wa Bibilia ni kwamba, Mungu wa upendo amemgeukia mwanadamu aliyeanguka na ulimwengu ulioharibika, na aliandaa ukombozi kwetu ndani ya Kristo.

Alitayarisha njia kwa Kristo kwa kumchagua Ibrahimu na Kutengeneza watu wakae kupitia yeye na kutangaza mapenzi yake kwa Musa na manabii. Hivi ndivyo njia ilivyofunguka kwa Mwana wa Mungu kuingia ulimwenguni. Hivi ndivyo mwangaza ulivyongaa katika giza na Mungu alimfikia mwanadamu. Hii yote ni kuhusu tendo moja kubwa la upendo wa Mungu. Hii iliandaliwa katika agano la kale na ilitimizwa juu ya Golgota na katika ufufuko, na mitume na wafuasi wake, kanisa lote la Kikristo walifanywa kusikia hilo. Kwetu sisi tendo la neema ya Mungu imekuja katika neno la Kimitume na ndani ya Sakramenti Takatifu ya ubatizo na Sakramenti ya meza ya Bwana.

Hivyo baada ya anguko kila mwanadamu anazaliwa mwenye dhambi katika ulimwengu huu (Zaburi 51:7) acha maisha yake pasipo Mungu na kuishia katika uharibifu wa milele. Kwa kufikiria kwa mfano kwamba watoto wote wamefanywa wa mbinguni hata pasipo Kristo ni kazi ya mawazo ya binadamu na haizingatii Bibilia. Wokovu pekee ni kwamba Mungu ameukaribia ulimwengu huu ulioanguka kwa njia ya Kristo, na alitimiza kazi yake ya ukombozi. Wewe kama mwanafunzi wa Yesu umeokolowa na umekuwa mwanafunzi wake katika ubatizo:

Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
(Mathayo 28:18-20, SUV)

2. Ubatizo ni nini?

Bibilia imeeleza ubatizo katika njia tofauti.

a. Kuzikwa na kufufuka. – Warumi 6

Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi. Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye;
(Warumi 6:1-8, SUV)

Kupitia sura za kwanza za Warumi. Paulo anakazia juu ya neema isiyo na masharti kwa ajili ya Kristo. Baadae anahusisha uwezekano wa kuleta mabishano,Ni kwamba Wakristo wanaruhusu watu kutenda dhambi kama vile wanavyopenda. Jibu ni lakushangaza. Hasha! Kwa sababu umeshabatizwa;

Nini kinachofuata, ni uwakilishi mkubwa kuhusu vipi ubatizo una maana ya vitu viwili:

Cha kwanza, ni zawadi ya Mungu ambayo inatengeneza muunganiko na kifo cha Kristo na ufufuko na utukufu wa Mungu.
Cha pili ni kwamba ni wajibu wa Mkristo ambaye amebatizwa kuishi kama mtoto wa Mungu.

Ubatizo una maana kwamba maisha ya zamani yalizikwa katika kifo cha Kristo, na kutoka katika kaburi la ubatizo tumefufuka kiumbe kipya ambacho kimeunganishwa kwa ufufuko wa Kristo, utu upya Mungu ameutengeneza ndani yetu. Huu ni wajibu wa aliye batizwa yaani Mkristo kuishi maisha ya Usafi ya utakaso, kila siku kuuvua utu wa kale na kuuvaa utu mpya. Hiki ndicho kitu Paulo anasisitiza kupitia sura zote ambazo zina utajiri hakika ukizisoma.

Hii ina msingi juu ya mtindo ambao Paulo kwa nguvu nyingi anafundisha pia mahali pengine. Kuna “utu wa kale”na “utu mpya”.
“Utu wa kale“ ni mtu kama yeye mwenyewe pasipo neema ya Kristo (Warumi 6).
“Utu mpya“ una simama kwa nafasi mpya kama Mkristo aliyekombolewa na Mungu. Maisha ya Mkristo ni kuhusu kabisa kufanya maamuzi kuhusu hii njia ya kuuvua utu wa kale na kuuvaa utu mpya.

”Mvue kwa habari ya mwanendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kufuata tamaa zenye kudanganya,na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu, mkavae utu mpya,uliumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli."
(Waefeso 4:22-24, SUV)

"Msiambiane uongo,kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale,pamoja na matendo yake, mkivaa utu mpya ,unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba“.
(Wakolosai 3:9-10, SUV)

b. Kuzaliwa upya (Yohana 3:5 na Tito 3:4-6)

"Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.
Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.
Nikodemo akajibu, akamwambia, Yawezaje kuwa mambo haya?
Yesu akajibu, akamwambia, Je! Wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu? Amin, amin, nakuambia kwamba, Lile tulijualo twalinena, na lile tuliloliona twalishuhudia; wala ushuhuda wetu hamwukubali. Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni? Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu. Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu."
(Yohana 3:1-18,SUV)

“Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa nyingi, tukaishi katika uovu na husuda, tukichukizana na kuchukiana. Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipovumiliwa, alituokoa, Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi: bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu, ambaye alitumwagia kwa wingi kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu: ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.”
(Tito 3:3-7, SUV)

Sura ya tatu ya Yohana imejumuisha vitu vingi vya msingi kama kiini cha sura sita za kwanza za kitabu cha Warumi. Hadithi ya Nikodemu lazima ichukuliwe kwa ujumla wote. Nikodemu, mtu maarufu na mtu mwenye haki, anakuja kwa Yesu na kutafuta njia ya kwenda kwa Mungu. Yesu anamwambia anatakiwa azaliwe tena.

Ni imawazo sawa kama Warumi 1, Haki ya mwanadamu mwenyewe haitoshi kutengeneza maisha mapya. Kile kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, Na hakiwezi kurudi katika roho. Tendo la Mungu linahitajika. Yohana anafupisha hii kwa kuita injili ya ufupisho. Hivi ndivyo Mungu anatengeneza maisha mapya katikati ya kifo. Alihitajika kuzaliwa tena "kwa maji na Roho.”

Neno “kuzaliwa tena”limetokea tu mara chache katika Agano jipya. Baadhi ya madhehebu yanafundisha kwamba, hii na kuongoka. Wakati neno linapofundishwa kwa mazingira mapana na kwa kuhusianishwa na maneno mawili, maisha na kifo, vifungu vingi maigizo yanaongezeka. Hata hivyo kuhusu tendo kubwa la wokovu la Mungu,ambalo pia lilizungumziwa katika kitabu cha Warumi. Alileta uzima katikati ya kifo na mwanga kwenye giza.

Hapa tendo la Mungu ni chombo kikubwa. Vitu vingi ni sehemu ya hili tendo, mfano kuleta uzima katikati ya kifo kama vile kifo na ufufuko wa Krisho juu ya Golgota, kuitwa kwa tendo la Roho Mtakatifu, Baraka ya kanisa pamoja na zawadi ya Mungu - na ubatizo Mtakatifu, vifungu vyote vilivyo tajwa vinaunganisha ubatizo pamoja na zawadi ya maisha mapya, mfano, kuzaliwa tena.

c. Kuwa mmoja wa mwili wa Kristo (1 Kor 12:12-13)

"Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja."
(1 Kor 12:12-13, SUV)

Msingi wa mtu kuwa mali ya Kristo si juu ya zawadi ya utukufu wa kiroho amepokea, na si kitu chochote ambacho kwamba kipo ndani yake mme/mke. Ni kile ambacho Roho Mtakatifu kwa yule aliye batizwa ndani ya jamaa ya mwili wa Kristo (12:12-13 SUV). Baada ya hayo Roho Mtakatifu anampa kila mshirika kwa sehemu yake na kazi yake anatia alama kwa tofauti lakini zinazo fanana.

Ina maana - kama nilivyokuwa nimesema kwa uzuri kwamba ubatizo ni kama kubarikiwa kwa mchungaji, kabla ya hapo kila Mkristo ana utume wake mwenyewe katika ulimwengu. Lakini kuwa wa Kristo si Mkristo juu ya zawadi tofauti au utume, lakini ni juu ya tendo la neema ya Mungu,ambayo imepokelewa katika ubatizo.

d. Mvaeni Kristo (Galatia 3:26-29, SUV)

“Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. Na kama ninyi ni Wakristo, basi mmekuwa uzao wa Ibrahimu na warithi sawasawa na ahadi."
(Galatia 3:26-29, SUV)

Tatizo kubwa kuhusu waraka kwa wagalatia ilikuwa na uhusiano baina ya Wakristo Wayahudi na Wakristo wa Mataifa. Paulo alifundisha kwamba wapagani wanaweza kuja kuwa wototo wa Mungu tu wakimwamini Kristo. Hata hivyo sasa kulikuwa na waalimu wamekuja Galatia ambao walifundisha wakristo wa mataifa si Wakristo wa kweli mpaka watakapo anza kufuata sheria ya Musa na wawe wametahiriwa.

Katika sura ya tatu ya Wagalatia Paulo anasema kwamba Mungu ametoa Baraka yake kwa Ibrahimu na uzao wake kwa mtu mmoja tu. Vipi tunaweza kuwa sehemu ya hii Baraka? Hivi ndivyo Paulo anajibu kuhusu hii “ mbegu” ni kwa mtu mmoja ambaye ni Kristo. Wakati tunapobatizwa katika umoja wake tulivikwa ndani ya Kristo na tuliunganishwa katika wamoja katika wakristo wote na kabla ya yote Kristo tumekuwa mwili wake. Katika hatua hii,haijalishi ya kwamba nani amezaliwa Myahudi na ni nani alizaliwa Myunani, Tangu tendo la Mungu limetoa kwetu neema, na ubatizo umetolewa kwetu wenyewe.

e. Ubatizo ni Agano la dhamira safi (1 Petro 3:20-22)

"Watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, Safina ilipokuwa ikitengenezwa, ambamo ndani yake wachache, yaan, i watu wanane, waliokoka kwa maji. Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unao waokoa ninyi pia siku hizi: (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili: bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu, ) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake."
(1 Petro 3:20-22, SUV)

Petro anaufananisha ubatizo na safina na mafuriko. Ubatizo ni kama meli ambayo inaelea popote itakapokuwa mafuriko yanakufikia. Muhimu si kwamba mwanadamu anahaidiwa kukata tamaa juu ya maisha yake ya uchafu - hata hivyo hii pia ni muhimu kutokana na warumi 6 - lakini kwamba Mungu amefanya agano la dhamira safi. Neno la Kiyunani “Eperotema” lina maana ya swali au mkataba ambao mtu mdhaifu kwa sehemu wanahoji wakati wanauliza. Hivyo mkataba au agano la dhamira safi mwanzo unamaana kwamba Mungu ametoa msamaha kwa mwanadamu na dhamira safi,ambayo mwanadamu kwa shukrani amekubali.

3. Ubatizo unaokoa na hauwezi kuokoa

Katikati lakini kila mara kifungu kinachosahulika na 1 Kor 10:1-11 wakati Paulo analinganisha watu kwa agano jipya kwa watu walio angahika wa agano la kale kutoka misri mpaka nchi ya ahadi. Hata hivyo kila mmoja alibatizwa kuwa wa Musa katika bahari lakini hawakuweza kufika nchi ya ahadi kwa sababu walishindwa kuamini.
Je;Mungu aliwaokoa hawa watu kutoka misri na kutoka katika mikono ya jeshi la Farao?Ndiyo alifanya kwa sababu aliwaongoza katika safari kuelekea nchi ya ahadi. Je;alifanya hivyo? No, Kwasababu walishindwa kuamini.

Hata katika ubatizo kila mtu ambaye amebatzwa amepokea kweli na tendo kamili la wokovu la Mungu ambalo tunaweza baki salama juu yake. Hata hivyo, hatuko kule bado, na njia ya mbinguni ni ndufu na hatari.

4. Mambo muhimu zaidi

Zingatia juu ya nini nimesema kabla, nitawakilisha mijadala michache ambayo wanaojadili, wanaweza taka kuchukua sehemu juu yake kama mambo haya yatakubaliwa matatizo mengine yatasuluhishwa. Lakini kama mambo haya yatasababisha kutokuelewa,itakuwa zaidi likely recur as the mjadala unaendelea. Hivi ndiyo kwanini ni vizuri kuzama sisi wenyewe katika maandiko yafuatayo:

(a) Kila mtu pamoja na watoto juu yake mwenyewe kabisa wako ndani ya dhambi na wanaokolewa tu kwa tendo la Mungu.

(b) Mungu ameweka ubatizo kama njia ya wokovu na, kwamba hii ndiyo sababu wokovu ni lazima hata kwa watoto. Hata hivyo Mungu hajafungwa kwa hiyo, kwamba hawezi kuokoa mtu ambaye hajabatizwa – Mungu yuko huru.

(c) Ubatizo ni zawadi ya Mungu kwetu sisi ambayo hakika na kweli ametupa sisi, ambayo tunahitaji ili tuweze kufika mbinguni. Swali kubwa katika ubatizo ni Kristo yupo au lah;na tumesamehewa dhambi zetu au hapana. Kama hapana, basi ubatizo hauna maana. kama ndivyo, hili ni tendo la Mungu ambalo sisi sote tunahitaji.

(d) Kwa nyongeza kuwa katika zawadi, ubatizo pia ni wajibu. Katika ubatizo tunajizoeza kuelekea mbingun, i lakini bado hatujafika pale bado. Wengi wao ambao wamekuwa wamebatizwa wanapotea njiani kwa kumkataa Bwana. Lakini tunayo ruhusa ya kutembea kuelekea mbinguni pamoja na watu wa Mungu na kuwa sehemu ya watu wa Mungu tayari hapa na baadaye kule Mbinguni.