Wewe ni nani Mungu?

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Oscar Olutu

1. "Hakika , wewe ni Mungu uliyejificha"…

Hakika nimekuwa kama mnyama wala si Mtu
Wala sina ufahamu wa mwanadamu;
Wala sikujifunza hekima, wala sina maarifa wa kumjua Mtakatifu.
Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini?
Ni nani aliyeshika upepo kwa makonzi yake?
Ni nani aliyekamata maji ndani kwa nguo yake?
Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi?
Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe kama wajua?
Kila neno la Mungu limehakikishwa;
Yeye ni ngao yao wamwaminio.
Usiongeze neno katika maneno yake; 
asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo"
(Mithali 30:1-6 SUV)

Kwa wengi Mungu amebaki kuwa siri kubwa, haijalishi ni kwa uangalifu gani tunamdhani au kumfikiri na kuzungumzia juu yake; Yeye anaonekana kuwa juu ya mafikirio yetu hatuwezi kumwona yeye au kumnakilisha (kuchora picha yake) halisi. Hatuwezi kujadiliana naye au kuuliza uchaguzi wake juu ya kitu chochote, yeye haeleweki, yuko mbali tena sehemu ya mbali sana, je! Mungu ni wa kweli? Tunajaribu kutafuta ukweli lakini hatuelewi.

Hapa tunakutana na msingi mmoja ndani ya imani yetu ya Kilutheri. Katika ufahamu ya jumla ni kwamba, “Mungu ni wa siri” na anafikiwa tu pale yeye anataka kufikiwa. Mungu yupo mbele ya ufahamu (wetu) mwanadamu kwa sababu alitaka kugeuza mgongo wake juu ya dhambi ya mwanadamu na kujificha kutoka kwetu. Kiongozi mmoja wa kanisa siku moja alisema,” Huwezi kumshika ndege njiwa kama yeye hataki kushikwa “ Hivyo ni vipi unaweza kufikiria kuwa unamshika Mungu, kama yeye hataki kutafutwa au kupatikana?

Ayubu aliyepata mateso ndani ya Biblia alisema,

kwa yeye awajua watu baradhuli; Huona na uovu pia hata asipohufikiri, Lakini mpumbavu aweza kupata ufahamu, ingawa mwanadamu huzaliwa kama mtoto wa punda-mwitu, wewe ukiuweka moyo wako kwa uelekevu na kumnyoshea mikono yako; ukiwa huna uovu mkononi mwako, uweke mbali nawe, wala usikubali upuuzi kukaa hemani mwako; hakika ndipo utakapopata kuinua uso pasipo hila, Naam, utathibitika, wala hutakuwa na hofu; kwa kuwa utasahau mashaka yako; utayakumbuka kama maji yaliyokwisha pita; na maisha yako meupe kuliko adhuhuri;lijapokuwa giza; litakuwa kama alfajiri. Nawe utakuwa salama, kwa sababu kuna matumaini, naam utatafuta- tafuta, kando yako, na kupumzika katika salama, tena utalala, wala hapana atakayekutia hofu, Naam, wengi watautafuta uso wako. Lakini macho ya waovu yataingia kiwi nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho”
(Ayubu 11:11-20 SUV).

Hatutaweza kamwe kuelewa Mungu mwingine Zaidi ya mmoja ambaye alijifunua yeye mwenyewe kwetu kwa njia ya Neno lake, badala yake hakuna hata mmoja wetu anaweza kumkariabia au kumfahamu Mungu aliyejificha. Hata hivyo mtu akijaribu hivi, yeye atashindwa, kwani atachanganyikiwa na mwishowe atapotea na kumchukia Mungu ambaye alifikiria amempata lakini kumbe alijiumbia Mungu wake mwenyewe.

Hata hivyo Mungu wa kweli anaishi na anapatikana, ni mwenye rehema na hakika anasikia maombi yetu, yeye ni wa kweli, si wa mafikirio ya uongo. Ni vigumu kwa mwanadamu kumtafuta yeye, lakini yeye anaweza kukutafuta. Kama tunataka haya yatoka kwetu sisi wanadamu wadogo lazima tusikilize kwa makini ni nini Mungu mkuu anasema.

Lazima tumtafute yeye ndani ya sehemu ambayo yeye anataka tumtafute, na si wapi anapenda kujificha, Ni bibilia tu itakuongoza kuishi na Mungu wa kweli na sio mfano wa Mungu aliyefanywa kwa sura ya Mungu. Pasipo neno lake utalazimishwa kuishi na akili iliyochanganyika na kamwe haiwezi kusuluhishwa na mwanadamu yeyote.

“Kila neno la Mungu limehakikishwa;
Yeye ni ngao yao wamwaminio.”
(Mithali 30:5 SUV)

2. "Kweli mbili”

Kuna kweli mbili za ukweli ndani ya ulimwengu;

Ya kwanza; Ni inayoonekana, inayogusika, na kusikika,
Ya pili, imeelezwa kwa neno la Mungu.

Bibilia inatueleza jinsi baadhi ya watu ambao walikuwa na nafasi ya kuangalia juu ya ukweli wa vitu vingine, maneno yao yanaonyesha mshangao, kuheshimu, kutamani na kutia hofu ya mwanadamu mdogo mbele ya Mungu Mkuu na Mtakatifu.

“Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.
 Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelefu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa“
(Danieli 7:9-10 SUV).

Kama nilivyotaja, baadhi yao wamekutana na huyu Mungu mkuu na mtakatifu, Mmoja wa hao watu ni Nabii Isaya, ambaye alijikuta katikati ya huduma ya kanisa kubwa lakini alilia kwa mashaka mengi, kwa sababu alitambua kwamba yeye kama mwanadamu mwenye dhambi kamwe hafai kukaa katika kundi hilo la roho zilizo safi wala kusimama mbele ya mtakatifu.

“Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.
 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.
 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.
 Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi.
 Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi. ”
 (Isaya 6:1-5, SUV)

Hata hivyo kuna umbali zaidi kwa wale wote walioguzwa na Mungu kwa njia ya makubaliano lakini kwa ajili ya kuwafanya wao kuelewa jambo fulani la muhimu, kwamba; Mungu ni mtakatifu na mimi ni mdhambi, na mbele ya Mungu nafsi ya kila mmoja ni kusimama katika sehemu ya mwenye dhambi na mwadamu wa kuangamizwa.

3. "...“Ee Mungu wa Israeli Mwokozi”

Mungu hakubaki tu pale katika ukuu wake kuona jinsi gani sisi wenye dhambi tungewza kuuchukulia ulimwengu huu wenye dhambi. Hata hivyo Mungu hakusubiri mpaka sisi sote tuishie katika uaribifu badala yake alitujali akaja karibu nasi, kwa kuwa alitupenda alitenda hivyo kwa kumtuma mwanawe kwetu kama bibilia inavyosema,

“Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.
Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.
Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure.
Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia,
Siku ya wokovu nalikusaidia;
tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.”
(2 Kor. 5:19 - 2 Kor 6:2 SUV)

Kuna mambo mawili katika kiini cha Ukristo, kwamba kinaweza kuwa kigumu;
Cha kwanza ni kipana sana
Cha pili ni chembamba.

Kile kipana kinatuambia hivi matengano, Mungu atamkubali kila moja katika ulimwengu kwa sababu ya Yesu Kristo;
na kile chembamba kinasema kwamba hakuna neema nyingine ipatikanayo zaidi ya Yesu na kazi yake.

Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima;
mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
(Yohana 14:6 SUV)

Sehemu pana inaweza kuwa ngumu kukubalika kwa sababu inaonekana ni rahisi sana. Hata hivyo neema ya Mungu ni hakika na bure, vinginevyo isingekuwa neema hakika. Mungu alikuwa ndani ya Kristo na alifanya upatanisho na ulimwengu.

Sehemu pana inaweza kuwa ngumu kukubalika kwa sababu inaonekana ni rahisi sana. Hata hivyo neema ya Mungu ni hakika na bure, vinginevyo isingekuwa neema hakika. Mungu alikuwa ndani ya Kristo na alifanya upatanisho na ulimwengu,

Kwa mtazamo mwepesi sehemu nyembamba badala yake inaonekana kuwa na neema ya Mungu hakika tu ndani ya Kristo na si mahali pengine? Ukweli hivi ndivyo ilivyo hakika. Kristo na ndiye njia ya kwenda kwa Mungu. Yeye ndiye njia pekee kwenda kwa Mungu. Kuna njia moja tu ya kuuona upendo wa Mungu, uso wa Mungu (Baba) na hivyo imeunganishwa katika Yesu Kristo. Yeyote ambaye amemkataa Kristo hana wokovu, yeye ambaye hapiti mlangoni hawezi kutoboa ukuta wa mawe.

Sehemu zote mbili ni kweli, kamilifu na Neema ya Mungu ya bure katika Kristo na tu ndani ya Kristo.

Katika kipindi cha majira ya joto nilichukua Muda kufka ufukweni mwa bahari huko Finland archipelago. Mara nyingine Mtu hudodosha simu yake ndani ya maji, kwa maana hiyo simu huwa imepotea moja kwa moja lakini mashine ya boti inaweza kuharibika na kufa kabisa. Yote ni matukio ya kuchukiza, lakini yaliyopita yamepita. Faraja iliyobaki inategemea ukweli wa Bibilia inavyosema juu ya Mungu.

“Atarejea na kutuhurumia, atayakanyaga Maovu yetu nawe utazitupa dhambi zao zote katika vilindi vya bahari, wewe utamtimilizia Yakobo kweli yako; na Ibrahimu rehemu zako ulizowaapia baba zetu tangu siku za kale”
(Mika 7:19-20 SUV)

Wakati Mungu atatupa dhambi zetu zote ndani ya kina kirefu cha bahari kwa ajili ya Kristo hakuna Mtu anaweza tena kuzichimba, kuja juu tena si mwanadamu, wala si shetani au Malaika.

4. Amini – hii ni nini?

Ukristo umejumuhishwa katika vipimo tofauti, mojawapo ni KUAMINI uhakika katika Mungu mwema.

Ebu chukua muda kufikiri juu ya mtu mmoja unayemwamini, kama unaweza kumtaja au kutaja wachache katika maisha yako uliyonayo, nani unaweza kumtaja na ni kwa nini?

Ebu fikiria hadithi hii, unatembea mtaani wakati huo anatokea mtu anakuja mbele yako na kuuliza juu ya kadi yako ya benki na kutaka neno la siri (Namba ya siri). Nina mashaka husingempa huyo mgeni. Lakini je kuna mtu unayemwamini zaidi ungeweza kumpa yeye? Mimi mwenyewe hakuna ugumu wa kumpa mwanangu kadi ya benki aende kujaza gari mafuta, kwani hataweza kutumia vibaya. Labda unaweza kufikiria mtu mmoja unayemwamini wakati wote kuamini juu yake kunavyokuwa , taratibu, mwaka kwa mwaka, inakuwa na Imara wakati wa magumu na mtu uliyemwamini kamwe hasikuangushe.

Hivyo kujiamini katika Mungu kunavyokuwa, kidogo kidogo, ekaristi kwa ekaristi, wimbo kwa wimbo, matatizo kwa matatizo. Sijui ni wapi alinichukuwa mimi na ni kwa nini, lakini najua hakika alifanya, kamwe hakunikataa, hakunisahau au kuniacha mimi mwenyewe, zaidi aliwavumilia wadhambi kama mimi kwa miaka mingi hata karne na karne na anaahidi kuniongoza mpaka nyumbani. Hivyo nimejifunza kumwamini yeye na niko tayari kufanya. Baba hawezi kamwe kumwacha mwanawe.

5. Mungu ni nani basi?

Mungu ni wa siri kubwa, mtakatifu aliyejificha, asiyeeleweka, ambaye hana dhambi wala giza. Lakini amekuja karibu na wanaadamu wenye dhambi kwa njia ya Kristo na ni pendo la ndani la Mungu Baba kwa wanadamu katikati ya wadhaifu wote, dhambi na maswali yasio na Majibu “Mwanga umekuja” kutoka katika neno la mitume:

Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu"
(1 Petro 1:8 SUV)