Uumbaji

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

1. Uumbaji kiini cha fundisho la ukristo

Bibilia imeanza na uumbaji na kumalizia na uumbaji. Kutokana na imani ya Ukristo dunia ina mwanzo wake na mwisho wake. Kati ya nyakati hizi mbili dunia ipo mikononi mwake Mungu,ambaye ameumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana kutoka pasipo kitu mpaka kuwepo na kitu. Yeye ni wa pekee na Mungu pekee - ambaye uwepo wake hauna mwisho wala mwanzo.

Kuamini katika uumbaji ni kiini cha fundisho la Ukristo. Katika hilo mwanadamu anatafuta nafasi mbele ya Mungu mtakatifu. Inatuongoza kuelewa kiini cha ujumbe wa Bibilia. Katika Bibilia Mungu anasema,ambaye amemuumba mwanadamu na ambaye anaita kila mwanadamu. Ukristo unaamini kwamba fundisho la uumbaji linatufundisha sisi vitu vingi na hapa nitatoa baadhi ya kiini chake.

Kanisa la kikristo ambalo linaamini katika uumbaji kwa kuamini Mungu ambaye ni mwenye nguvu katika ulimwengu mtawala asiye na mshindani. Hata kama uovu unatawala wala dhambi ya mwanadamu haiwezi kufanya hata kitu kidogo kuharibu nguvu ambayo ipo duniani mwote iliyopo mkononi mwake.

Mungu ambaye aliumba ulimwengu kwa neno lake, atafanya historia kufikia mwisho kwa neno lake. Kipindi cha agano la kale. Kipindi hiki chote cha nyakati ya utawala wake. Kipindi cha agano la kale, waamini walioamini katika hili, walikwenda katika safari ya hatari na walitegemea juu ya muumbaji mkuu.

‘’Nitayainua macho yangu nitazame milima;msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu ukatika bwana aliyezifanya mbingu na nchi.”
(Zaburi 121:1-2, SUV)

Tokea kipindi cha ufunuo, wakristo walioteswa walitegea katika hili na waliomba kurudi kwa Bwana na kutoa haki kwa watu wake.

”Na alipoifungua mihuri ya tano nikaona nchi ya madhahabu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu na kwa ajili ya ushindi waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema Ee mola, mtakatifu, mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu, kwa hao wakaao juu ya nchi?”
(Ufunuo wa Yohana 6:9-10, SUV)

Katika taabu ni vigumu kutegemea juu ya Mungu muweza wa yote. Hata hivyo kuna chanzo kikubwa cha tumaini hata sasa.

Sehemu ya pili kuamini katika uumbaji ni kuamini katika ukweli ya kwamba Mungu anatunza kila mtu. Mwaamini mmoja katika agano la kale alisujudu kwa Mungu,ambaye alijua mwimbaji wa zaburi tayari alipokuwa katika tumbo la mama yake, ambaye alijua kila siku kitu kabla hakijaja.

”Maana wewe ndiye uliye niumba mtima wangu,uliniunga tumboni mwa mama yangu. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu na nafsi yangu yajua sana, mifupa yangu haikusitirika kwako,nilipo umbwa kwa siri, nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; macho yako yaliniona kabla sijakamilika,chuoni ziliandikwa zote pia, siku zilizo amriwa kabla hazijawa bado,Mungu fikira zako zina dhamani nyingi kwangu, jinsi ilivyokubwa jumla yake;"
(Zaburi 139:13-17, SUV)

Kila mwanadamu amefanywa kwa njia ya kutisha ya ajabu. Ni hakika kwa sababu ya hii kila mwanadamu ni wa thamani, iwe ni mwanamume au mwanamke mtoto hajazaliwa au mtu mzee, mweusi au mweupe, mwenye afya au asiye jiweza, mkristo au mwislamu. Utu wa mwanadamu ni wake mwenyewe. Kiasi cha dhambi hakiwezi kufifisha upendo wa Mungu. Kila mtu ni mpenzi wa Mungu na kila mmoja ameitwa naye. Neno la Yesu ambalo kuhusu Mungu anatunza watu anawajua vizuri na anawagusa.

"Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?  Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake."
(Mathayo 6:25-34, SUV)

Kutokana na sura ya kwanza ya Bibilia, Mungu amempa mwanadamu utume:

”Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha mkawatawale, samaki, wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”
(Mwanzo 1:28, USV)

Utume unaofanana na huo kwa mwanadamu unaweza kupatikana katika zaburi ya 8 . Mungu amempa mwanadamu nafasi ya kipekee katika uumbaji wake. Ina maana heshima kubwa lakini pia wajibu mkubwa. Mwanadamu yupo katika njia “Mtunzaji katika shamba la Mungu.” Tunayo haki kutumia uumbaji lakini sio wetu. Kama ilivyo, kila mtu ameumbwa na Mungu, hivyo, ni mtumishi wake, kila mmoja atakutana na kutoa hesabu ya maisha yake. Kutokana na imani ya Kikristo hakuna hata mmoja anaweza kustahimili hukumu pasipo kutegemea juu ya Kristo aliyeleta neema na msamaha wa dhambi kwa kila amwaminie yeye.

2. Biblia na sayansi ya asili

Baada ya chapisho la Asili ya Viumbe la Charles Darwin, kumekuwa na mjadala kati ya ukristo, ambao kwa kweli haukuweza kufikia mwisho. Kipindi cha mwisho katika nusu ya karne mijadala ya sayansi ya asili imeendelea na pia majibu ya makanisa ya kikristo kutafuta ukweli imekuwa ni tofauti. Tatizo kubwa ni rahisi kulitengeneza, sura ya kwanza ya Bibilia inatuambia jinsi sisi Mungu alivyoumba Dunia kwa siku sita. Sayansi ya pili kwa upande mwingine wanamtazamo tofauti kwa asili ya ulimwengu, hatua ya mwanzo ya sayari na maendeleo ya mwanadamu, Elimu ya kisasa ya nyota na Elimu ya viumbe inatuambia hadithi tofauti kuliko Bibilia kutokana na wanasayansi walio wengi, fundisho la mabadiliko, ni maelezo mazuri kwa asili ya wanadamu.

“Mungu hakuumba mwanadamu lakini mwanadamu alimuumba Mungu” - Uanzishaji huu toka karne 19 Mfilosophia Mjerumani alieneza wakati wa komunisti walichukua kama maneno yao ya asili, Dini si tu uongo lakini ni hatari kwa sababu inapuuzia mabadiliko. Dini ni chaguo la wengi ”Maana inapunguza maumivu wakati mkato mkubwa wa upasuaji unapohitajika".

Nadharia hii ya mabadiliko kwa hiyari imekuwa ikitumika kama kubadilisha kwa dini na kuongoza watu kumwacha Mungu. Wengi wanarudia msemo huu au kauli mbiu hii. ”Siamini katika Mungu,Ninaamini katika mabadiliko.“ Kutokana na imani yetu ,kila mtu ambaye ameacha dunia kwa kuamini imani hii atakutana na muumba wake na atatoa hesabu ya maisha yake kwa Mungu.

Fundisho la mabadiliko pasipo Mungu hakika si la Mungu. Hata hivyo si kila mtu ambaye anajitoa kwa fundisho la mabadiliko anatumia kama silaha juu ya imani. Baadhi ya wakristo wanafikiri wanaweza kujumuisha fundisho la mabadiliko pamoja na imani zao, wakati mwingine hapana.

3. Je ni vipi mabadiliko yatathaminiwa?

Wakristo wanaosimamia msimamo wao wamejibu mashambulizi ya kafri kwa pigo la fundisho la mabadiliko, na mapigo yake. Kutokana na uhakiki wake, mnyororo mzito wa mabadiliko ni ngumu na pia haiwezekani, kuuwakilisha na umekosa muunganiko tokea wakati hadi wakati kwa kuwa umewakilishwa, katika maelezo ya sinema. Kwa nyongeza halina fundisho lote kwa uwazi, linachotegemea ni kwamba uwezekano wa maisha na maendeleo yake kwa ukubwa na utofauti. Na utajiri tunajua sasa ni kitu kidogo sana.

Na wakati mwingine tuna sababu ya kushughulika kwa ubora uhakiki wa Kristo. Mabadiliko na asili ya ulimwengu umesomwa sana katika vyuo vikuu katika ulimwengu mzima. Wakati mwingine haya mashindano yanatengeneza ushawishi wa uongo kwamba hawa wanasayansi ni wajinga au wanaongea pasipo kufikiria vizuri je: Je! lakini ni ukweli muafaka wa ulimwengu mzima ujinga wa kutokuwa na Mungu na je, kuna ukweli pale na maazimio kufanya kukae kimya kukubali vitabu?

Lazima tukubali kwamba kuna eneo la imani na cheo cha sayansi, yote kwa pamoja yanakubalika. Imani haitegemei juu ya mjadala lakini inategemea juu ya neno la Mungu. Sayansi, kwa upande mwingine, inajiridhisha kwa ukweli kwamba inajichanua kwa sababu za kibinanabamu. Si kila wanasayansi wa Asili hawana Mungu na si wote wanaoamini fundisho la mabadiliko hawana Mungu. Katika mazungumzo ya uwazi wakati wote maunganiko hayo yaonyeshwa. Kwa upande mmoja yule anayeongelea sayansi ya Asili apinge Ukristo, na upande mwingine kwa wale wanaopinga pasipo kujali. Ubora wa maelezo yao, kinachobakia katika maazimio kidogo ni uchunguzi wa makini ambao hauna kusudi kwa haya malengo,vizuri kama vile uchunguzi wa Kikristo. Mmojawao alifupishe sentensi kwa urahisi kama hivi ‘Mungu aliumba dunia’. Sasa tunajribu kuangalia vipi ilitokea.

Siku moja nilikutana na Mvulana na Msichana. Walikuwa wamechumbiana wiki chache. Wote walikuwa wanafahamu kuhusu Ukristo lakini pia watakua madaktari, walio na elimu Imara ya sayansi ya asili. Nini mchumba wake anaona wakati akiamwangalia bwana arusi wake­­­­­­­­­­­­­­­­­? Mkusanyiko wa viashiria vilivyobaki kutokana na mabadiliko ya mwili. Hii pia ni mtazamo sahihi. Lakini kwa bahati huu siyo mtazamo aliokuwa nao; Pia alimwona mpendwa wake pamoja naye aliyependa kushirikiana naye kwa maisha yaliyobaki.
 Wakati wote kuna mitazamo mingi ya kuangalia vitu. Ulimwengu na asili yake unaweza kutazamwa kutoka mitizamo miwili. Sayansi itaangalia kutafuta ni kwa umbali gani inaweza kupata. Na Ukristo utainama chini kwa muumbaji mkuu na kuangalia sehemu yake mwenyewe. Mitazamo yote hiyo miwili ina maana ya utume kwetu.

Nadharia ya mabadiliko ni sayansi ya natharia na ni lazima iwe katika uwanja wa sayansi na katika vyombo vya sayansi. Ndani ya ulimwengu wa sayansi, nadharia nzuri wakati wote inachukuwa nafasi ya iliyo mbaya, hata kama itatokea taratibu.

Angalia nyuma, Imani ya kikristo kwa karne nyingi wakipinga juu ya sayansi na kuchunguza katika njia tofauti; Kuna wakati, walikataliwa kabisa na hekima ya kibinadamu isiyo na umuhimu, ila wakati mwingine waliletwa kama hivyo. Hata hivyo kwa sehemu nyingi kulikuwa na baadhi ya vitu vya uhusiano kati ya Imani ya ukristo na sayansi. Kufafanua huu uhusiano ni utume kwa kila kizazi na umejaa Hekima inayohitajika kwa huu Utume.

4. Ni kwa jinsi gani imani inakuwa jinsi ilivyo?

Hazina moja ya Imani ya Kilutheri ni hakika kwamba mwanadamu hawezi yeye mwenyewe kuwa mwamini. Wala hawezi kubakia katika Imani hata mara moja kwa nguvu zake mwenyewe. Ni Roho mtakatifu anaweza kuamsha imani ndani ya Kristo katika moyo wa mwanadamu.

Mapingano ya wakristo juu ya nadharia ya mabadiliko wakati mwingine yana kitanguliza cha tabia; Inaamini kwamba mtu ambaye anaelewa nadharia ya mabadiliko kama uwongo unaokuja kwa waamini. Hata hivyo kuweka nadhiria moja ya sayansi pamoja na nyingine haitafanya moja ya Ukristo. Hoja za mwanadamu zina lengo lao wenyewe, lakini haziwezi kumfanya mtu kuamini ndani ya injili ya msalaba. Imani ni zawadi ya Roho mtakatifu, na inatoa kuzaliwa kwa upya kwa hiyo kupitia Neno na sakaramenti popote na popote atafanya.

5. Sujudia hekima

Sayansi inajisifia kwa utengemezi wake na kujitawala. Sifa moja ya sayansi haiangukii/sujudia /shuka chini mbele ya mtu yeyote au kitu chochote. Sayansi ya mwaka 1900 ilikuwa imezungukwa kwa anga la matumaini; mwanadamu anaweza kutatua matatizo yake katika huu ulimwengu kwa msaada wa sayansi na teknologia. Kipindi cha miongo iliyopita Imani hii imekuwa ikipata wakati mgumu. Furaha lakini imevunjavunja, upweke na mazingira kupelekea uharibifu.

Mwanzo wa Agano jipya, tunaambiwa kwamba watu wenye hekima kutokea mashariki walikuja katika hori alimolazwa mtoto Yesu. Hawakuja hata kidogo kwa hekima kusujudia mbele ya Mtakatifu, katika tofauti ya kazi waliopewa tendo na nyuso zao zilizonyesha raha na furaha ya ugunduzi.
 Pembeni mwa matarajio yaliyovunjika, malazi na wembamba wa sayansi tunahitaji hekima ambayo unaweza kusujudu mbele ya muumbaji mkuu.