Je kuna maana gani ya maisha?

Mwandishi: 
Liisa Rossi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Mojawapo ya mahitaji muhimu ya mwanadamu ni kutafuta maana ya maisha. Tunaweza kutafuta maana ya maisha kwa kutenda mema, katika watu ambao tunawapenda, kazini, katika kuendeleza maisha, katika kutafuta hekima na mengine mengi, ila katika mambo haya yote hakuna hata moja ambalo linaweza kutosheresha kabisa swali la kina lililo katika mioyo yetu.

Sehemu ya kuanzia kutafuta maana kamili ya maisha ni kutambua kuwa tumeumbwa ili katika maisha tuwe na uhusisiano na Mungu. Kadiri tunavyoishi mbali na Mungu, jambo la maana linalokosekana katika maisha yetu. Jambo la maana na muhimu ni kuishi katika maana tuliumbwa kwayo, maanake kuishi katika uwepo wa Mungu, bila dhambi au uovu ambao unaweza kututenganisha naye. Hivyo jambo muhimu katika maisha yetu ni kumfahamu Yesu, ambaye ndiye maisha ya kweli. Kwa imani katika yeye tutafika nyumbani kwa baba yetu wa mbinguni.

Hata kama hatima ya maisha yetu ya mwisho ya maisha yetu ni mbinguni, maisha yetu hapa duniani si kwamba ni bure na hayana maana. Tuna nafasi ya pekee katika kupendwa na Mungu, kumpenda and kutangaza upendo wake miongoni mwetu.

nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
(Wafilipi 3:14, SUV)

Mungu, wakati sijui au sielewi, nionyeshe njia ya kuendea.