Wapi naweza pata msaada wakati naogopa kifo?

Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Kutoka Yesu mwenyewe. Ni kwmba, kwa asili tunaogopa kifo. Kifo na washirika wake- magonjwa, ajali majanga yote ni ya muovu, na si yaMungu muumbaji. Kifo kwa hakika si cha asili na hutakiwi kujaribu kuwa rafiki nacho. Paulo alisema “kifo ni adui wa mwisho. lakini kazi ya Yesu ni ushaidi mzito / imara kwamba kifo na washirika wake hawatashinda.”

Yesu ameshinda kifo, na wewe kama mtoto wake utatokea kupitia kifo kama mshindi. Sikia kwa makini wewe mwenyewe. Hakikisha unajikabidhi kwa Yesu. Atakikabili kifo chako moja kwa moja. Hata kama unaogopa kama vile watoto wadogo wanavyofanya wakipata tatizo, wanakimbilia kwa baba yao, anatuliza hali hata kama usiku ni mrefu na wa kiza (giza). Hisia mara nyingi zinashindwa, lakini Imani ambayo inaamini katika Neno la Mungu, haitashindwa.

“Yesu akamwambia, mimi ndimi huo ufufuo, na uzima aniaminiye mimi,ajapokufa atakuwa anaishi, naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa milele, je! Unayesaidika hayo?"
(John 11:25-26, SUV)

Mungu bado kifo kinaniogofya. Tafadhali uwe pamoja nami.